Kitaja
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 2,836
- 1,382
Wamesha elewa kaka, sasa wengi wameshaanza kufuata mafundisho ya Kikatoliki,
Kihualisia sio mafundisho ya Kikatoliki, bali ni mafundisho sahihi ya Kibiblia na Mapokeo, sasa wanaanza kujua
1: Tumsifu Yesu Kristo (Salamu ya Kikatoliki) wao wańasema Bwana asifiwe ni lile lile tu
2: Walokole wote wanaenda kuungama/ kukiri dhambi zao kwa wachungaji wao, japo hawaliweki kwenye muktadha huo, lakini lengo ni lilelile kama la Wakatoliki
3: Sasa kila kanisa la kilokole wanatumia Mafuta na Maji kwenye maombezi yao Hizo ni traditional za Kikatoliki, siku za nyuma walikuwa hawatumii chochote zaidi ya kusema Yesu pekee ndio mwokozi
4: Kanisa kama Sabato sasa liko kwenye mjadala mzito kuhusu habari ya Utatu mtakatifu, wengine wanaamini na wengine hawaamini katika hilo, mwisho watakuja kwa Wakatoliki kujifunza na kujua ukweli
5: nk
Nikufahamishe tu ndugu yangu, Kanisa la wasabato yaani SDA nguzo yao kuu ipo katika Utatu Mtakatifu, yaani Mungu Baba, MUngu Mwana na Mungu Roho Mtakatifu. Yaani nafsi hizi tatu ndizo zinakamilisha Uungu. Hii ni nguzo kuu katika misingi ya Imani ya Waadvenstista wa Sabato (SDA). Hao walioko kwenye mjadala labda ni watu wengine ulizia vizuri.