MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Biblia inasema yule mwizi pale msalaban yesu alimwambia LEO.... Narudia tena LEO utakua nami pradisini/peponi
 
nitofauti na kwenda kwenye kile kibanda cha bikira maria na kukisujudia. Acheni kusudia sanamu mungu kakataza

Hivi hujui ugomvi Luther na Catholic? Ni baada ya kanisa Catholic kuuza hati ya msamaha
 
Kwa wale mnaosema Mungu siyo Mungu wa wafu JE wanaposema Mungu wetu ni wa ibrahim, isaka na yakobo je hawa sio wafu???? Kwa hiyo tunamwabudu Mungu wa wafu???
 
Mtarukaruka sana lakini Neno la Mungu liko pale pale. Mnyama wa ufunuo 13 na 14 ni papa, kahaba wa ufnuo 17:15 ni kanisa katoliki chini ya papa, pembe ndogo inayoazimu kubadili amri za Mungu ni papa Daniel 7:25.Chukizo la uharibifu lisimamalo mahali patakatifu alilolitaja Yesu Kristo ni mamlaka ya kirumi na upapa, Mathayo 24:15. Mtu wa kuasi, mwana wa uharibifu, yule pingamizi,ajiinuaye nafsi yake juu ya kila kiitwacho Mungu,ama kuabudiwa; hata yeye mwenyewe kuketi katika hekalu la Mungu, akijionyesha nafsi yake kama kwamba ndiye Mungu(2 Wathesalonike 2:2-4).

Ukisoma kwa makini aya zote hizi zinazungumzia kanisa katoliki chini ya papa. Ni kanisa hili pekee limethubutu kubadili amri za Mungu (Daniel7:25).Kiongozi wa kanisa hili, papa hujiita mbadala wa Kristo, "Vicarius Filii Dei", yaani Vicar of the Son of God.Na katika ufunuo 13: 18 Ndipo tunaipata ile namba 666 ambayo ni jumla ya herufi za kirumii katika cheo anachojiita papa yaani VICARIUS FILII DEI. Ndiyo maana Biblia katika ufunuo 13 inasema " ana majina ya makufuru".Ukiangalia ibada za kikatoliki papa anaabudiwa kama Mungu "makufuru". Yesu aliita chukizo la uharibifu,.Paulo alimwita mwana wa kuasi.Yohana namwita Kahaba Mkuu.[/QUOTE]
Upotoshaji ule ule wa babu yako William Miller juu ya mwisho wa dunia akitumia vifungu vya biblia 1844.....sasa na wewe unajaribu kulitukana Kanisa Katoliki ukitumia vifungu vya biblia.....!ebu tuambie Miller alitumia vifungu gani kutabiri mwisho wa dunia......?
 
Maria mama wa Mungu. UMEBARIKIWA kuliko wanawake Wote. Na Yesu Mzawa wa Tumbo lako AMEBARIKIWA.

Swali : nani Amewabariki hawa?
 
Kwa wale mnaosema Mungu siyo Mungu wa wafu JE wanaposema Mungu wetu ni wa ibrahim, isaka na yakobo je hawa sio wafu???? Kwa hiyo tunamwabudu Mungu wa wafu???
Tatizo sio wafu. Tatizo ni kuabudu mtu tena sanamu badala Ya Kumuabudu Mungu pekee.
 
Tatizo sio wafu. Tatizo ni kuabudu mtu tena sanamu badala Ya Kumuabudu Mungu pekee.
Kuabudu maana yake ni kufanya ibada kwa kitu ambacho unaamini kuwa ni muweza wa yote/ muumbaji, swali je wakatoliki katika ibada wanazitukuza zile sanamu na kuziabudu au huwa ni ibada kwa Mungu?? Kama wanaabudu sanamu mbona wakianza ibada kuna sala wanasali WANASADIKI KWA MUNGU MMOJA.....WANASADIKI KWA YESU KRISTO...... Na PIA WANASADIKI KWA ROHO MTKTIF.... Mbona hawasemi wanasadiki kwa sanamu...
Iweje muwalazimishe kuwa wanaabudu sanamu???

Shukrani
 
Question religion question it all,And Questions exists until them questions are solved.
 
Pole sana inanyesha huamini Biblia.Mafungu niliyoweka hapo yote yanatoka katika Biblia.
Yanotaka katika biblia siyo sababu...Je! Mantiki na maudhui ya hayo mafungu umeyaelewa...???

Maria ni mfu, mkipigia magoti sanamu yake, jueni mnaabudu mfu. "Kufuru ikioje" Ndiyo maana Bibli
Aliyesema anaabudu ni nani...? Hii umetolea wapi...??

Ile ilikuwa ni ahadi, "nakuambia leo hivi, utakuwa nami peponi".
Kwahiyo kama ni ahadi...??

Ahadi hii ni kwa yeyote amwamimiye Yesu awe hai ama amekufa ahadi itatimia mara tu Yesu ajapo.
Kwani watu wakifa huenda wapi...? Naona huamini maisha baada ya kifo...Hili ni tatizo..

Kabla ya wewe kukurupukia mistari usio na weledi nayo...ni hora ungepitia mstari huu...Mhubiri 7:12


Soma kwa makini mafungu hayo ya Biblia. Inasema tutakuwa na Bwana milele, kama Yesu alivyomwahidi yule mwizi kuwa atakuwa naye peponi, hii ahadi hukamilika Yesu ajapo.
Huu upuuzi umetolea wapi...?? Aliyekuambia maisha baada ya kifo hamna ni nani..? Ni Ellena..?

Msijidanganye kwa hadithi za kiroma ili kuhalalisha ibada ya wafu.someni Biblia wenyewe msingoje kuhadithiwa Padri.
Tusome Biblia gani...?
 
Kitaja,
9 Na alipoifungua muhuri ya tano, nikaona chini ya madhabahu roho zao waliochinjwa kwa ajili ya neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda waliokuwa nao.

Ufunuo wa Yohana 6 :9

10 Wakalia kwa sauti kuu, wakisema, Ee Mola, Mtakatifu, Mwenye kweli, hata lini kutokuhukumu, wala kuipatia haki damu yetu kwa hao wakaao juu ya nchi?

Ufunuo wa Yohana 6 :10

11 Nao wakapewa kila mmoja nguo ndefu, nyeupe, wakaambiwa wastarehe bado muda mchache, hata itakapotimia hesabu ya wajoli wao na ndugu zao, watakaouawa vile vile kama wao.

Ufunuo wa Yohana 6 :11

Soma kwa utulivu bila mihemko. Kwavile mnapenda sana nukuu labla ubishane na maandiko sasa. Ndugu kama wewe ni Mkristo na huamini ukifa katika hali ya neema huendi direct mbinguni basi wewe tumaini lako ni bure ....nenda kajifunze upya maana ya ufufuo wa wafu ....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…