MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

9 Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi;
10 kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja.
11 Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu.
12 Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja.
fst,
 
MESHACK WARIOBA,
Kuna jambo huwa hatuelewi. Nalo ni elimu, uelewa na mazingira. Kuhusu dini wazungu wana elimu na uelewa mkubwa akilinganisha na wafrika.

Aidha, mazingira ya wazungu na wafrika yanatofautiana.

Kati ya mambo ambayo hupaswi kuyaelewa kama ni BINAFSI ni dini. Dini au imani sio jambo binafsi. Kuelewa hivi ni kazi bure.

Kwa sababu hiyo, dini na kile inachokibeba ndio maisha yenyewe ya mwanadamu. Jambo la kujiuliza, hatahivyo, ni je, kwanini kuna dini au makanisa tofautitofuauti? Ni kweli Mungu alikusudia dini au makanisa tofautitofauti?

Aidha, dini inakuwaje jambo binafsi ikiwa watu ni uzao?
 
Martin alikuwa padre wa shirika la Mt. Agustino wakati wa kipindi cha Papa Leo.Anyways does God love Rebellion?

Ukihama kanisa sababu padre/mchungaji amekosea kosa ni la nani kama sio lako?

Kanisa ni la Padre/ mchungaji au ni la Mwenyezi Mungu? Mwanzo wa kosa moja ni Mwanzo wa makosa mengine kama unavyoona leo kila mtu anajifungulia kanisa lake na watu kupotea................
 
Kwanini Papa wa Kikatoloki alitoa amri Martine Luther auwawe na ahesabiwe kama mnyama?
Katoliki ni dhehebu la kishetani wanamwabudu mungu wa kipagani.

Ndio maana ukiwa Mkatoliki hurusiwi kuhoji wala nini unatakiwa kukubaliana na maelekezo ya miungu (Mapadri) Deogratius Kisandu,
 
Aidha, dini inakuwaje jambo binafsi ikiwa watu ni uzao?
Ndugu yangu, Je unaelewa maana ya neno BINAFSI? Kuamini unachoamini ni hiari yako mkuu..! Ndio maana unaweza kuamini unachochagua wewe? Ndio maana nikasema ni suala Binafsi, yaan linategemea na Uamuzi wako.

Ile kwamba Umezaliwa kwenye budhist, Muslim, Christianity haimaanishi kwamba huwezi hama kama utakuwa radhi na imani nyingine, ishu ipo kwa mtu binafsi, na ndio nikasema watu wanaogopwa kutengwa na jamii; of which kama uko commited naamini hakuna kutengwa na jamii isipokuwa unabadilisha jamaa kutoka uliokuwa nao Muslim, kwenda Budhist kama utakuwa umehamia huko.

Hivyo ni suala BINAFSI, uzao unatoa msingi tu;
 
Ndugu yangu unaongea kwa kashfa sana na si Ustaarabu;
Lakini pia nadhani Hufahamu Historia Vizuri, Katika masuala ya Denomination za Christianity, Wakatoliki ndio watu wametoa mwanga kwenye Denomination unazozijuwa zote, wao walifanya toka Karne ya kwanza wakiwa wanaitwa Warumi.

Kama umesoma History ya Church utaona kwamba Walikuwa wakibadilika Karne hata Karne; hayo mambo unayosema inawezekana hawakupatika watu wa kuyaweka sawa Mapema.

Watu wengi tunaishia kusoma Bible pekee, bila kufahamu Historia ya Kanisa Duniani; Ukisoma Historia ya Kanisa utagundua Dini kuu mbuli Christian na Muslim zilifanya mauaji sana Kulazimisha watu wa enzi hizo Kufuata Imani yao; Hivyo hakuna Dini ambayo haikupitia Mfumo Fulani;

Mimi si mkatoliki lakini kutumia Maneno ya kashfa kwenye imani za watu si sawa. Kama Mungu alivyochagua Israel, lakini wengi wao wamekataa kuchaguliwa, Ndivyo ilivyo Katoliki, Denomination zote zimetokea hapo.
 
Mtabishana sana, bado itabaki historia iliyosimuliwa na waliosimulia ni vizuri kusoma kwani inawakilisha walichokiamini lakini pia ni wajibu wetu kutafuta ukweli katika walichokiamini. Tu kamili kama wao, waliwezaje sisi tushindwe kwani tumaumbo kamili yalioumbwa na Mungu,

hivyo basi tuko na Mungu ndani yetu na hatuhitaji simulizi wala maandishi kuthibitisha hilo. KABLA YA KUTAFUTA NA KUJUA MUNGU NI NANI? HEBU TUANZE KUTAFUTA SISI WA UKWELI TUKOJE? ( The true self) Kwani TUMEUMBWA KWA MFANO WA MUNGU. TUKIIJUA NAFSI YETU YA KWELI TUTAJUA NJIA YA UKWELI YA UHAI NA MAISHA YETU tutaacha kubishania masimulizi ya vitabuni. YOH: 4: 23 -24

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwahiyo hivyo vitabu unavyotaka tukavisome vimeshushwa au vimeandikwa na wanadamu kama Mimi na wewe,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii makala au riwaya ina walakini mwingi na haina mantiki kabisa! Mwandishi anapaswa kujua kuwa Bibilia haikuandikwa na mtu mmoja,na ilikuwa kazi ya watu wengi mno kutafisiri lugha ya michoro ya zamani ili kupata maana
Luther hakuwa na hoja yoyote na Bibilia as alikuja kuisoma Biblia ukubwani sana,wakati huo Wakatoliki walikuwa na Mithali/Misali za waumini ambayo ni kama Biblilia iliyochujwa sana,ni Bibilia halisi ndio ikimfungua Luther hadi akaona mistari inayosema kuwa kwa kupigwa kwake Yesu sisi tumesamehewa bure,qakati huo msamaha ulikuwa unatolewa kwa fedha! Unalipa ndio upate msahama
 
Ndugu yangu baki kwenye siasa huku unapwaya sana. Waandishi wa vitabu vinavyounda Biblia ni wengi lakini unajua akina nani walichambua vitabu vyote wakaona hivyo unavyojua leo ndio vinastahili kuwekwa pamoja? Unajua injili zilikuwepo nyingi na sio nne tu unazoona leo?

Nani aliamua mpangilio wa hivyo vitabu? Kianze kipi, kifate kipi hadi ufunuo? Walitumia utaratibu upi kupata mpangilio? Unajua biblia unayotumia leo mpangilio wa chapters umewekwa mapema karne ya 13 na Askofu Steven Langton na chapters za bible zimewekwa kwa verses baadae kabisa! Zote hizi ni kazi za Kanisa Katoliki ambalo ndio lilisimamia michakato yote na kupitisha matumizi yake kwa waamini.

Usisahau kazi hii yote inafanyika hakuna makanisa ya kilokole zaidi ya Kanisa Katoliki ambalo baadae liligawanyika na kuzaliwa Orthodox church ambalo pia ni apostolic church.

Kanisa ni moja tu, ndio maana hutokaa usikie makanisa ya Katoliki maana Kristo hakusema atajenga makanisa yake bali atajenga Kanisa lake! Kanisa Katoliki! Ndio alama pekee ya kanisa la Kristo ulimwenguni tukiamini imani moja, ubatizo mmoja na mchungaji mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wakishashiba makande bwana, watataka kutunisha matumbo yao ili watu waone la nani ni kubwa kama wale jamaa zangu wa Ethiopia wanaotembea chululu zipo nje!😂😂

All in all dini zilikuja kwa mashua tu, kinachopaswa kufuatwa ni imani thabiti ya mtu.. ukimwamini Mungu, ukaacha uovu, inatosha hayo mengine tuwaachie Wajerumani na Waitaliano.
 
Umetoa wapi hili fundisho? Au ndio umeamua kuamini unachotaka?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usisahau siasa ndio inaratibu maisha yetu ya kila siku
Hitimisho lako kuwa Biblia imeandikwa na Wakatoliki ni upotoshaji mkubwa.
Mosi.Bibilia ya kwanza inasadikiwa iliandikwa kwa lugha ya Armaic hii ni lugha ya eneo la Mashariki ya Kati pamoja na pembe ya Afrika,ni miongoni mwa lugha za kwanza kuandikwa zaidi ya miaka 4500 iliyopita
Pili.Ukiristo kwa ujumla wake umeanza miaka 2000 baada ya ufufuo wa Yesu Kristo na ndio wakati Agano la jipya,tafsiri yake ni kuwa Ukatoliki umeanza karne ya kwanza yaani baada ya Yesu kufufuka

Tatu.Dini ya kwanza ya iliyotimia Bibilia ni Judaism ambayo ilianza miaka mingi kabla ya Yesu


 
Kuna watu wanadanganya pia kuwa madhehebu yote yametoka kwenye ukatolik. Nadhani ndo wanavyodanganywa huko.
Ukweli ni kuwa ukatolik ukishirikiana na serikali ulikandamiza madhehebu mengine na kuwaua waumini wake , hivyo kupelekea kutokuabudu waziwazi
Na baada ya upinzani kutoka ndani yao wenyewe kwa wenyewe, ikashindikana kuthibitiana ndio madhehebu mengine yakaanza harakati zake waziwazi
Wakatolik hawakuandika biblia yoyote. Kwanza hawapendi watu wasome biblia kwa kuwa mambo mengi wanayofanya hayaendani nayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…