Ndugu yangu baki kwenye siasa huku unapwaya sana. Waandishi wa vitabu vinavyounda Biblia ni wengi lakini unajua akina nani walichambua vitabu vyote wakaona hivyo unavyojua leo ndio vinastahili kuwekwa pamoja? Unajua injili zilikuwepo nyingi na sio nne tu unazoona leo?
Nani aliamua mpangilio wa hivyo vitabu? Kianze kipi, kifate kipi hadi ufunuo? Walitumia utaratibu upi kupata mpangilio? Unajua biblia unayotumia leo mpangilio wa chapters umewekwa mapema karne ya 13 na Askofu Steven Langton na chapters za bible zimewekwa kwa verses baadae kabisa! Zote hizi ni kazi za Kanisa Katoliki ambalo ndio lilisimamia michakato yote na kupitisha matumizi yake kwa waamini.
Usisahau kazi hii yote inafanyika hakuna makanisa ya kilokole zaidi ya Kanisa Katoliki ambalo baadae liligawanyika na kuzaliwa Orthodox church ambalo pia ni apostolic church.
Kanisa ni moja tu, ndio maana hutokaa usikie makanisa ya Katoliki maana Kristo hakusema atajenga makanisa yake bali atajenga Kanisa lake! Kanisa Katoliki! Ndio alama pekee ya kanisa la Kristo ulimwenguni tukiamini imani moja, ubatizo mmoja na mchungaji mmoja.
Sent using
Jamii Forums mobile app