MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

MJADALA: Kwanini Padri Luther aliondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia, na kwanini alijiondoa kanisa Katoliki?

Hahaha ....unapopinga angalia usitende dhambi ....neno la Mungu ni nini? Kuna andiko kwenye Biblia ambalo si neno la Mungu? Unajua neno la Mungu ni Mungu mwenyewe? Ukisema alisema Maria si Mungu ina maana mafundisho ya mitume ni ya mitume si Mungu? Tatizo lenu mnapopinga Ukatoliki mnajisahau hadi mnavuka mstari.
Unaendekeza hofu. Barua za Paulo kwa makanisa yalikuwa maneno yake. Nitakuwa na dhambi gani hapo?
 
Ndg yangu cjui umenipata concept yangu....?biblia imeandikwa na Mungu kupitia watu wake hata hiyo barua ya pili ya kichungaji kutoka kwa Paul kwenda kwa Timotheo mstari 3:16-17 ujaweza kuutumia vzuri,mm namaanisha biblia ya Kikatoliki yenye vitabu 73 imejaribu kumrahisishia msomaji aweze kupata mahudhui kirahisi zaidi kwani wanaanza na mhutasari kwenye kila kitabu kisha unaanza kusoma kitabu husika,NB:Unajua historia ya kuandikwa biblia...?Je unajua biblia ya kwanza iliandikwa kwa lugha gani...?Kwann Leo waprotestant biblia yao INA vitabu 66....?Kwann Leo wayahudi biblia yao INA vitabu 39....? na kwann Leo Wakatoliki biblia yao INA vitabu 73....?ndg hv ni vtu muhimu sana kabla ujaanza kunukulu barua za Paul kwa Timotheo.
Paulo hakuandika barua zake ziwe sehemu ya Biblia. Ni juhudi za watu zilizofanya hivyo. Na juhudi za zinaweza kuzifuta .
 
Hapana bana. Kulikuwa na makanisa mengi toka mwanzo. Na juhudi za watu kuwa na makanisa yao zilikuwepo. Lakini ukatoliki ilikuwa ni dini ya dola. Hivyo kanisa lilizima juhudi hizo.

Sehemu ambazo zilikuwa nje utawala wa kirumi kama vile Ethiopia, India na Uarabuni zilifuata ukristo uliokuwa tofauti na Ulaya.

Na pale jamii za Ulaya zilipoanza kutengenisha kanisa na serikali, makanisa tofauti yalianza kutokea.
acha kupotosha umma, huyo jamaa yuko sahihi

unasema kulikuwa na makanisa mengi tangu mwanzo,

unaweza kututajia makanisa walau matano yaliyokuwapo wakati huo wa Roman Catholic walipochukua dola na kuwa ya kikristo?
 
acha kupotosha umma, huyo jamaa yuko sahihi

unasema kulikuwa na makanisa mengi tangu mwanzo,

unaweza kututajia makanisa walau matano yaliyokuwapo wakati huo wa Roman Catholic walipochukua dola na kuwa ya kikristo?
Sasa unataka nikusaidia kwenye ufinyu wako wa elimu? Wewe unafikiri ukristu ilianza na kanisa moja tu la kikatoliki? Yesu aliishi Israel na wanafunzi wake walienda pembe zote zilizofahamika. Je wanafunzi wake waliokwenda India walibeba Biblia unayotumia sasa? Biblia unayotumia sasa ilikubaliwa miaka 300 baada ya Kristo. Je waumini katika kona za mbali walitumia vitabu gani?
 
uongo wa mchana hebu lete andiko.
maana maria ndiye aliyesema hivyo.
LUKA 1:46-48.
anasema watamwita mmbarikiwa lakini sio Mungu kusema tutamwita hivyo
Kweli wewe hajui kusoma. Ebu uwe Unaweka maandishi ya mstari uutoao
 
uongo wa mchana hebu lete andiko.
maana maria ndiye aliyesema hivyo.
LUKA 1:46-48.
anasema watamwita mmbarikiwa lakini sio Mungu kusema tutamwita hivyo
Afu uwe unajua Msingi WA hayo maneno yameanzia wapi. Anza mstari wa 41
 
Rejea Kitabu cha Mhubiri 7:12

Nayo mwili hurudi mavumbini ulikotoka nayo Roho kumrudia Mungu aliyeitoa .....

Roho haifi kamwe...

Soma ufunuo 5:8 uone Watakatifu wanafanya kazi gani mbinguni..
Usiongee usichokijua na pia unapo-quote mstari hebu uandike ili tunapopitia tuusome na tuelewe ulichokuwa unataka tujue..mfano Ufunuo 5:8 inasema: Hata alipokitwaa kile kitabu, hao wenye uhai wanne na wale wazee ishirini na wanne wakaanguka mbele za Mwana - Kondoo, kila mmoja wao ana kinubi, na vitasa vya dhahabu vilivyojaa manukato ambayo ni maombi ya watakatifu.''
ehe..Ulitaka kusema nini juu ya Mstari huo kwa kufuatana na maelezo ya Mwanadamu kuchukua nafasi ya Yesu Kristo kupitisha maombi yetu..
 
Soma Ufunuo uone jinsi Yohane anapata ufunuo..

"Tazama ishara ikaonekana mbinguni, mwanamke aliyevikwa jua na mwezi chini ya miguu yake na taji ya nyota 12 juu ya kichwa chake"
Eee! Unaelewa maana ya huo Mstari..unajua alikuwa anamaanisha nini? Mwanamke ni nani huyo?...Jua na mwezi zinawakilisha nini? Taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake ni nini hicho?
Usimeze mistari tu bila kujua maana yake..!
 
Mkuu we ninani hadi umpinge mtu ambaye aliweka agano na Mungu?unadhani uwepo wa bikra Mariam ni wakibahati mbaya?soma Bible vizuri,halafu tuliza akili yako vzr,achana na mapokeo ya mafundisho ya wachungaji wako,fikiri vizuri,Wakati Mungu akimtumia ujumbe Mariam hapakuwepo na wanawake wengine,kwanini bikra Mariam?,Yaani Mungu Baba aweke agano la milele na Na Mama yule wewe useme she is noboby,ama kweli,watu wake wanaangamia kwa kukosa maarifa!!!!
Usikasirike, Elezea kinagaubaga watu wakuelewe kwanini Bikra Maria ameperwa nafasi ya Yesu Kristo kinyume na Maandiko...Nadhani ukielezea watu watakuelewa tu..usipende kukaririshwa mafundisho na wewe unataka kuwakaririsha wengine kama hayana msingi kimaandiko huwezi kujitetea, Wewe sema Biblia inasema hivi na bikra Maria alishaambiwa hivi na ndiye aliyeandikwa katika Kitabu fulani...usizungukezunguke na kuanza kukasirikia pasipo sababu..Karibu udadavue sasa!
 
KWANINI PADRE Luther ALIFUKUZWA KANISA KATOLIKI? NA KWANINI ALIONDOA BAADHI YA VITABU KWENYE BIBLIA AGANO LA KALE?

Padre Luther alikuwa miongoni mwa Mapdre wenye karama nyingi ndani ya Kanisa katoliki wakati wake, Yeye alikuwa na Madai mengi sana juu ya mapungufu kwa kanisa. Hata hivyo madai yake mengi hayakuwa na msingi wowote.

Moja ya madai yake ilikuwa ni kuondoa kibali cha kwamba baada ya kuungama muumini asipewe stakabadhi ya kuonesha ameungama kwa kuwa kitubio ni siri ya MTU. Hili lilifanyiwa kazi. Mengine ikiwemo kurekebisha mfumo WA sala ya Kanuni ya Imani. Na mambo mengine mengi ambayo alipojibiwa, yeye hakuridhika pamoja na kueleweshwa vya kutosha. Alikuwa ni Great Thinker sana.


Mbaya zaidi alipokuja kusababisha mpaka akajitenga na kanisa ni kitendo cha kuondoa baadhi ya vitabu kwenye Biblia ikiwemo pia kupunguza baadhi ya mistari kwenye vitabu kama cha Esta na Cha Danieli.
Aliondoa vitabu vya Deutrokanoni na vingine baadhi na kuwa jumla ya vitabu 7 vilivyotolewa kwenye Biblia. Na kila kitabu alikuwa na sababu yake aliyoibainisha. Kimsingi alipata wafuasi wengi WA kumuunga mkono hoja yake hasa wale ambao walikuwa wanatafta njia ya kuchuma pesa kiulaini. Na hapo Biblia mpya ilianza yenye Vitabu pungufu.

Na ndio maana Leo watu hawaujui Ukristo vizuri na wanakinzana bila kujua historia ya kanisa. Watumishi wengi WA Mungu hasa HAWA WA kileo wasiojua nhistoria vizuri wao kila kitu wanapinga. Sio kosa lao Bali ni kosa la kutokujua historia ya kanisa.
Matumizi ya Ubani yalipingwa sana, na hapa ilikuwa ni kuondoa idadi ya waelewa. Kutokana na watu wengi walikuwa wamegeuka kama waganga kila mapepo ya kiwakabili walitumia ubani kuyafukuza na yalikimbia, lakini watu walijisahau kusali na kuomba na hata kufika ibadani ikawa nadra maana wanajua kujiponya kuondokana na majini na wachawi. Hapa Padre Luther na wenzake wakapiga marufuku matumizi ya ubani na kuwa sihi wakazanie Neno zaidi.

Hapa walichotakiwa kufanya ni kuliishi Neno la Mungu na wakati WA ibada basi ubani uchomwe kama Mungu alivyo agiza.
Luther na wenzake lengo lao lilikuwa ni biashara hapo baadae na kimsingi mpango huo ulifanikiwa. Na ndio maana mpaka Leo watu wametawaliwa na mfumo WA majini katika maisha yao kwa kuwa wamefungwa akili ya kujitambua na wanaamini maneno ya mdomoni na sio Maandiko ya Biblia kama yanavyosema.
Nimengi ya kujifunza sana Leo hii lakini kwa Leo naishia hapa.

deogratius Nalimi Kisandu.
1. 1. 2017.
Source Please..! No Research No Right to Speak..! Si wajua hii ni forum ya Public unaweza sema kuwa ulifanya uchunguzi wa kutosha na kujiaminisha kuwa ni KWELI na kuamini kuwa haktakuwa na impact hasi kwa wana forum.! Please
 
Maria ni Mtakatifu kama Watakatifu wengine...Na Watakatifu wana kazi ya kutuombea....Wao ni Kanisa Shindi huko mbinguni..

Soma Ufunuo 5:8 uone maombi ya Watakatifu na Wale wazee 24 mbele ya Kiti cha Mwana Kondoo..
Mmmm! wanakuombea lini? Hebu uandike huo mstari ili tuusome wote tuone hicho unachokisema kama ndicho kinachomaanishwa..Karibu
 
Source Please..! No Research No Right to Speak..! Si wajua hii ni forum ya Public unaweza sema kuwa ulifanya uchunguzi wa kutosha na kujiaminisha kuwa ni KWELI na kuamini kuwa haktakuwa na impact hasi kwa wana forum.! Please
Good reply...Amekurupuka tu!
 
Kwani kwenye harusi ya kana kinywaji kilipoisha, walimfuata nani ili awaombee kwa Yesu?, tatizo haya makanisa ya kilokole yanayoendeshwa na wachungaji ambao ni darasa la saba wanawapotosha, hawaijui biblia
Hili ndiyo tatizo. Kuna jamaa mmoja miaka ile tulipata komunyo ya kwanza pamoja, baada ya kama mwezi nakutana naye eti ameokoka na kunena kwa lugha,

Kichwani alikua mweupe, yaani akianza kukuhubiria anajua tu sikukuu ya pentekoste na vifungu vya sadaka, nilicheka saana maana alikuwa ananena kwa lugha kila anapojiskia, bahati mbaya hakujua kua anatamka maneno yanayojirudia, shakarobosho kashararaa, aliyokaryosambaa shokororoboto...

Tumuogope Mungu Jaman.
 
Tatizo ni wivu tu
Yn.14:6 inasema: 'Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi'....Yesu Kristo peke yake ndiye njia ya kumfikia Mungu Baba, hakuna mtu mbadala wala mwingine aliye kiunganishi kati ya mwanadamu na Mungu Baba. Huo mstari ndiyo tafsiri yake kwa ufupi...Haya..elezea Mstari gani unampa mwanya mtu mwingine zaidi ya Masihi...Yesu Kristo Kumfikia Mungu Baba ..!
 
Sasa unataka nikusaidia kwenye ufinyu wako wa elimu? Wewe unafikiri ukristu ilianza na kanisa moja tu la kikatoliki? Yesu aliishi Israel na wanafunzi wake walienda pembe zote zilizofahamika. Je wanafunzi wake waliokwenda India walibeba Biblia unayotumia sasa? Biblia unayotumia sasa ilikubaliwa miaka 300 baada ya Kristo. Je waumini katika kona za mbali walitumia vitabu gani?
hatuzungumzii ukristo, tunazungumzia makanisa

kuanzia huo mwaka 300 AD,

Wakati wa dola ya kirumi,

kulikuwa na makanisa mangapi?
 
Eee! Unaelewa maana ya huo Mstari..unajua alikuwa anamaanisha nini? Mwanamke ni nani huyo?...Jua na mwezi zinawakilisha nini? Taji ya nyota kumi na mbili juu ya kichwa chake ni nini hicho?
Usimeze mistari tu bila kujua maana yake..!
Kwa taarifa yako, sio kujua hayo mafumbo ya vitu na watu, ni kuwa kitabu chote cha Apokalpse ya Yohana nina weledi nacho ..

Vipi unataka tuelimishane...??
 
Back
Top Bottom