.
*uandishi wako unaonyesha kua huijui historia ya kanisa,,,
kwa mfano huzungumzii sala kwa bikira maria na cheo chake cha umalkia, ubatizo,,, imani, na neno..
Kwani sala ya Bikira Maria (japo umeandika jina lake kwa herufi ndogo) ina tatizo gani. Ni maneno ya kutoka kwenye Biblia toka kwa Malaika Mkuu Gabriel kama amkio na maneno ya shangazi yake Maria akiitwa Elizabeth. Labda nikukumbushe amkio ili. Salamu Maria umejaa neema umebarikiwa kuliko wanawake wote (Malkia) na yule utakayemzaa (aliyeko tumboni mwako amebarikiwa) - (“salaam Maria ewe uliyebarikiwa na Mungu! Bwana yuko nawe” Lk 1:28.)
Ona
Elizabeti, mama wa Yohane, alijiona hastahili kutembelewa na Bikira Maria, Mama wa Yesu, akamuita, “Mama wa Bwana wangu” (Lk 1:43).
Habari nzima hii hapa: anzia haya ya 39 -45
39 Basi, Mariamu akaondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda,
40 akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia Elisabeti.
41 Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu;
42 akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa.
43 Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?
44 Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu.
45 Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.
Sasa wewe ni nani upinge kilichoandikwa. Wewe ni nani useme salamu ambayo Wakatoliki wanamuamkia Bikira Maria si halali wakati Malaika mkuu amemwamkia Maria na Mama yake Yohana Mbatozaji mama Elizabeth amefanya hivyo?