Mtukutu wa Nyaigela
JF-Expert Member
- Sep 4, 2018
- 8,013
- 14,263
Bikra Maria amebarikiwa , ni kweli ,hakupewa kazi ya kuombea watuMimi ni mkatoliki, nilibatizwa mwaka wa 1970, nilizaliwa mwaka 1968 NA sasa Nimefikisha miaka 50 na miezi kadhaa. Kwa kweli niseme tu, hizo kashifa dhidi ya kanisa letu hazikuanza Leo, zipo tangu zamani miaka ya nyuma sana na ziliasisiwa miaka 1880 NA waprostetant wa karne hizo NA baadaye walikuja wasabato akina Helen white na baadaye kabisa walikuja mathehebu ya kilokole ambapo mpaka wanaendeleza chuki zao NA kashifa zao dhidi ya kanisa NA Pope Francis.
Mimi nilibahatika kusoma baadhi ya nyaraka au vitabu mbalimbali vinavyoelezea historia ya mapapa NA ukatoliki, pope wa Kwanza kabisa ambaye kaburi lipo Vatican City pale Saint Peters Busilica, alikuwa mtume PETRO NA baadaye wengi wamekuja NA kuondoka duniani maana duniani tunapita tu, makao yetu ni mbinguni kwa Baba. Kuna suala LA kuwaombea materemu, waprotestanti wanalipinga hilo, lakini wanasahau kusoma MT 12:32, kumbe upo msamaha baada ya kifo. Kwahiyo, sisi hutuabudu sanamu na wala hatumtegemei mwanadamu kuishi bali tunayo SALA YA BABA YETU rejea misale ya waamini ambayo hiyo sala imerejea andiko LA biblia Mt 6:9-13.
Kuhusu sala ya bikira Maria, sisi hatumwabudi bali tunamwamba kupitia tu kwake kwa kuwa MUBGU mwenyewe kupitia malaika akimtamkia kuwa amebalikiwa NA kupewa NEEMA na Bwana NA Bwana yu pamoja naye na atamzaa MTOTO mwanaume NA jina lake ni YESU, mwana wa aliyejuu, Mungu mkuu rejea Lk 1:26-31, Isa 7:14, 9:6, MT 1:21-23, Lk 1:30-35.
Pia, Mama bikira watu walikuwa wakimfuata kumwomba amwambie mwanaye awatekelezee mahitaji yao, rejea wakati wa harusi ya Kana, hata DIVAI ilipokuwa ilipokuwa imewatindikia kwa biblia ya kiingereza by Gideon anasema when the wine ran out, the mother of Jesus said to the Jesus, they have no wine and Jesus said to his mother, my hour has not yet come and mother told the servants do whatever he tells you, Ina maana hawa watumishi wa waliomba kupitia kwa mama Maria na Yesu alifanya muujiza kwa kubadili maji kuwa divai, Yn 2:1-11.
Kwa Leo naishia hapa, nitaendelea tena kujibu hoja kwa kadiri MUNGU atakavyoniongoza.
Ila muombezi wetu ni Yesu tu
1Timotheo 2:5Maana yuko Mungu mmoja, na pia yuko mmoja anayewapatanisha watu na Mungu, binadamu Kristo Yesu,