Binafsi ninamuunga mkono mtoa mada japo kidogo. Hili swali nimekua nikijiuliza sana tena kwa muda mrefu sana. Sijawahi kuona mkutano wa dini umefanyika au maombi yamefanyika alafu mwanaume mtu mzima au mvulana akapandisha mashetani. Siku zote nimekua nikiona wanawake tu wasichana kwa wamama watu wazima.
Wanawake tumeumbwa viumbe dhaifu
Yale si majini au mapepo ni maruwenge yao...maruwenge hayo yanachangiwa zaidi na shuda mbalimbali za maisha, kukosa watoto, waume zao kutojali familia, kukosa mume, kazi nk nk....
Jamani ni nabii au mtume gani hapa bongo ambae yupo vizuri kwenye haya mambo?
Ila mimi bado nna swali, kama kweli ni maruwenge inakuaje yanaamka tu pale unapoombewa tena na nabii,mtume au mchungaji? mbona kanisani hayo maruwenge hayapandi?
Hilo nalo neno!!Si kweli, ila mabint na hao kina mama wanatumia vitu vingi vinavyowavutia mapepo kuwa marafiki zao: Mapepo wanapenda sana mahali pachafu kama, Kuvaaa mawigi, nguo za kikahaba kama vipedo na matiti wazi vyote hivyo ni vivutio kwa mapepo.