MJADALA: Kwanini Wanawake wanaongoza kuwa na majini/mapepo kwa kasi kuliko Wanaume?

MJADALA: Kwanini Wanawake wanaongoza kuwa na majini/mapepo kwa kasi kuliko Wanaume?

Binafsi ninamuunga mkono mtoa mada japo kidogo. Hili swali nimekua nikijiuliza sana tena kwa muda mrefu sana. Sijawahi kuona mkutano wa dini umefanyika au maombi yamefanyika alafu mwanaume mtu mzima au mvulana akapandisha mashetani. Siku zote nimekua nikiona wanawake tu wasichana kwa wamama watu wazima.

Wanawake tumeumbwa viumbe dhaifu
 
Jamani ni nabii au mtume gani hapa bongo ambae yupo vizuri kwenye haya mambo?
 
Teamo,
Mkuu ungemaliza kwa kusema: huko waendako wanawake, Luna manabii, maaskofu, wainjilisti, watumishi, mashekhe, maulamaa, maustadhi na walimu wengi, wengi sana, walio wanaume.
 
Yale si majini au mapepo ni maruwenge yao...maruwenge hayo yanachangiwa zaidi na shuda mbalimbali za maisha, kukosa watoto, waume zao kutojali familia, kukosa mume, kazi nk nk....
 
Yale si majini au mapepo ni maruwenge yao...maruwenge hayo yanachangiwa zaidi na shuda mbalimbali za maisha, kukosa watoto, waume zao kutojali familia, kukosa mume, kazi nk nk....

Bora sie wanawake maruwenge nyie wanaume mkishindwa tu maisha mnakufa kwa presha au kujiua kama suluhisho
 
Ila mimi bado nna swali, kama kweli ni maruwenge inakuaje yanaamka tu pale unapoombewa tena na nabii,mtume au mchungaji? mbona kanisani hayo maruwenge hayapandi?
 
Yap ni kwamba wanawake hawjistiri na malaika hawezi kuwa karibu na mwnamke isiyejistiri kufunika nywele pamoja na viungo vyake vingine ndo mana majini yanawaingia. Kwa kuongezea kupenda kukaa kwenye kioo kujiangalia maumbile yake hao nao wapo hatarini kuingiwa na majini. ukweli ni huo watake wasitake yapo mengi sana ni hayo kwa ufupi..
 
Ila mimi bado nna swali, kama kweli ni maruwenge inakuaje yanaamka tu pale unapoombewa tena na nabii,mtume au mchungaji? mbona kanisani hayo maruwenge hayapandi?

Inategemea, na mtu anyekuombea. Au huyo kiumbe aliye mwilini ana nguvu kiasi gani.

Pia usafi/uchafu wa mtu husika anayesumbuliwa na tatizo hilo hutegemea pia kuwa na nguvu za ziada kiasi gani, hapa nazungumzia nguvu za kiroho. Na pia usafi/uchafu nazungumzia wa kiroho pia mamiii.
 
Si kweli, ila mabint na hao kina mama wanatumia vitu vingi vinavyowavutia mapepo kuwa marafiki zao: Mapepo wanapenda sana mahali pachafu kama, Kuvaaa mawigi, nguo za kikahaba kama vipedo na matiti wazi vyote hivyo ni vivutio kwa mapepo.
Hilo nalo neno!!
Ukiwaambia hiyo si sawa wataanzisha vita na wewe!!!
 
Ni kweli kwamba wanawake wanaodhuriwa na mapepo/majini ni wengi zaidi kuliko wanawake. Sababu ziko kadhaa:-

a) Kimaumbile, wanawake wanafanya mambo yao kwa hisia. Wanaweza kujiingiza kwenye jambo lolote bila kufikiri sana. Ndio maana wanashawishika kirahisi sana. Wakishashawishika ni rahisi kwao kuingia kwenye mazingira ambapo wataathiriwa na mapepo. Wanaume wao wanatafakari jambo kabla ya kuamua.

b) Wanawake wengi wana tabia ya kupenda kupewa tu, hata kama wana pesa nyingi. Mwanamke hata kama ana milioni kwenye begi lake bado anataka umnunulie muda wa maongezi wa elfu mbili. Kwa sababu hiyo wanajikuta wameshapokea vitu vinavyoambatana na mapepo.

c) Wanawake wengi wanataka wawe wanapendwa na waume au wachumba zao. Wapo wengi ambao wanashawishika kwenda kwa mganga. Mwanamke ataenda kwa mganga eti kutafuta dawa ili mume wake ampende zaidi kumbe hajui tabia zake ndizo zimesababisha upendo wa mumewe kupungua. Mganga anapomwambia amempa 'dawa' ya mvuto anakuwa amempa jini la kumfanya mwanaume wake avutiwe naye au kumfanya 'duwanzi' awe anakubali kila kitu mke anachomwambia.

d) Mwanamke anapokosa mtoto inamwia shida sana. Wengi wanaenda kwa waganga ili wapate watoto. Wapo waganga wengi tu wanaume ambao wanamwambia mwanamke aliyeenda kwake kutafuta 'dawa ya kupata mtoto' kwamba hiyo dawa haifanyi kazi mpaka mwanamke alale na huyo mganga. Hapo baadhi ya majini ya mganga yanahamia kwa huyo mwanamke. Hata kama mwanamke huyo hajalala na mganga, hiyo 'dawa ya kupata mtoto' ni jini analowekewa.
 
Wanawake hawana utukufu wa mungu ndani , hiyo ndio sababu .
 
Adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie majini yaliyo mengi yanayotuandama sisi wanawake ni ya kutupiwa na wachawi , na hiyo yote inasababishwa na chuki kati yetu kama , wivu , husda , vijicho, n.k. ndo maana unakuta wanawake tunaongoza kwa kuwa na ugonjwa wa majini na mapepo kwa sababu ya chuki, husda, wivu wa wenyewe kwa wenyewe ..
 
Mkuu kumbuka ibilisi huwafuatilia sana wanaomtafuta Mungu (mostly wanawake *your perspective*) na kutokuwa na shida na watu ambao anao tayari (wanaume * your perspective*).
 
Teamo,
Usijichoshe sana mdogo wangu
Shetani anapenda kukaa sehemu chafu Na ukizingatia wanawake wengi wanatokwa na hedhi so muda mwingi hawako tohara yani wasafi kwahiyo mashetani inakuwa rahisi sana kuwaingia.
 
mitindo huru,
Umejiaminisha na elimu ya kulishwa na wachumia tumbo kwa mgongo wadini, kuna vitu umeandika humu ukiulizwa utaishia kusema ktk ulimwengu wa roho.

Kifupi wala hakuna mapepo kwa kiasi inachoonekana,kinachowatatiza akina mama na kuonekana mapepo ni roho mbaya,wivu,na yanayofanana na hayo ambayo wameyajaza mioyoni mwao kiasi cha kuharibu utu wao wa ndani na akili zao.

Wakiacha roho mbaya,tamaa,majungu,wivu,vijicho,chuki,husuda,usengenyaji,uongo,na sasa tamaa ya kumiliki wanaume,hautaona tena hilo neno mapepo kwa wanawake
 
Back
Top Bottom