Sababu kubwa ni kuwa kwa jinsi walivyoumbwa wanawake wanapenda kwa nguvu, yaani wana hulka ya kupenda au kuamini kitu/ mtu kwa haraka, mara moja, jumlajumla n.k bila kufanya tafakari ya kina tofauti na wanaume.
Kiuumbaji wanawake wana huruma sana kulinganisha na wanaume. Sasa basi hulka yao hiyo (ya kuamini/kupenda) kama nilivyoeleza awali, inawafanya wanapokumbwa na changamoto za kisaikolijia mfano kufiwa na wapendwa wao, kuachwa/ kudanganywa katika ndoa/ uhusiano, magonjwa (hasa ya muda mrefu/ yasiyo na tiba) na wakati huohuo akatokea mtu andayedai kuwa anayo majibu ya changamoto hizo wanawake huamini harakaharaka, jumlajumla.
Ndiyo maana utawakuta wanawake wengi katika makongamano ya kidini, waganga wa kienyeji, sehemu za maombi n.k na hao watu (wanaodai kutatua changamoto hizo) hutumia udhaifu huo (wa wanawake) ambao wanaujua tayari kwa kuwaambia kuwa wana mapepo/ majini na vifananavyo.Ndiyo maana utawakuta wanawake ni wengi katika maeneo hayo.