MJADALA: Mafanikio kibiashara bila uchawi haiwezekani?

MJADALA: Mafanikio kibiashara bila uchawi haiwezekani?

Helixir

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2022
Posts
461
Reaction score
1,214
"Oy babu Hauwezi shika milioni kumi au kutengeneza himaya Kubwa kibiashara bila kwenda KWA mganga kuchukua ndagu"

Unamwona Fulani ako na kidonda kisichopona ...

Mangi anae msukule ndani unaodondosha udenda ambao ni hela...

Mpemba anayo majini ...

Hizi ni baadhi ya kauli tinazokumbana nazo kila siku kwenye mazingira ya utafutaji ,

Je ni kweli bila ndumba Mtu hawezi kufanikiwa kifedha?
 
Hiko hivi, duniani kuna nguvu mbili zina operate, nuru na Giza na zote zinafanya kazi.
Usiporoga basi inabidi usali Sana, changamoto watu haturogi wala hatusali tupotupo tu.
Ukifungua biashara karibu na mtu anaeroga basi na wew rogaa au sali.
 
Hiko hivi, duniani kuna nguvu mbili zina operate, nuru na Giza na zote zinafanya kazi.
Usiporoga basi inabidi usali Sana, changamoto watu haturogi wala hatusali tupotupo tu.
Ukifungua biashara karibu na mtu anaeroga basi na wew rogaa au sali.

Unaweza kufafanua kidogo mkuu ,haswa hapo kwenye kuroga?
 
Hakuna biashara ya halali kwa asilimia mia nyingi ya biashara ni za dhuluma mbalimbali, kukwepa kodi, wizi na ushirikina
Dah nitafika nikiwa nimechoka Sana , KWA kuchelewa au nisifike kabisa 😢
 
Nimesoma mabandiko ya watu wengi nafurahia michango yao.Lakini jambo la kweli ni hili, mafanikio ni jambo la rohoni na sio mwilini.

Ukimuona mtu tajiri leo ujue ni tajiri toka rohoni na sio mwilini, mwilini ni udhihirisho tu wa kile cha rohoni. Bahati mbaya watu wengi huficha siri za mali zao na ukijaribu kudodosa mtu watakwambia ni juhudi tu, usidanganyike sio kweli kunawatu wanfanya juhudi sana lakini hawana kitu.

Na kama ingekuwa juhudi basi wazee wetu vijijini wangekuwa matajiri sama maana wanajuhudi sanaa. Utajiri unapatikana kwa kuishi vizuri na Mungu au Nashetani njee ya hapo utakuwa na cheji za kawaida tu sana lakini huwezi vuka hatua za kutisha. Hata leo angalia wengi wa matajiri ni watu walioa ina either kwenye makampuni yao au serikalini nk. Je hizo ni juhudi nazo?

Si vizuri kutaja watu, ipo mifano ya watu waliokwenda kwa shetani na ni matajiri sana tu (wauza mioyo kwa shetani). Vikwazo vyakuwa tajiri ni vingi mnooooo kiasi kwamba bila nguvu za Mungu au shetani huwezi kitoboa.

Hapa natamani kusema ni wewe na akili zako kuamua utafute mali kwa kupitia upande upi bila kuathiri marshati na vigezo vya upande huo uutakao na mali utapata tuu tena sanaaaa

Kwa shetani ukipata mali ukahonga sawa tu, ukitoa sadaka kwa Mungu sawa tu maana unachuma laana na anapenda ulaaniwe maana Mungu hataki sadaka chafu, ukisambaza ukimwi sawa tu maana unajenga ufalme wake,ukinunulia watu pombe sawa tu, ukiwa na wanawake au wanaume hata 100 sawa tu, ukiuwa sawa tu ndo kwanza zinaongezeka. Kwa sababu unaujenga ufalme wake. Ila ukifaa motoni

Kwa Mungu, lazima Mungu akujaribu moyoni na ahalikishike kuwa hutatumia pesa kuharibu watu wake, umililiki wake na utakuwa msaada kwao. Hutakuwa na kiburi wala hutazitegemea pesa zako kwani Mungu peke yàke ndiye wa kutegemewa na yeye ndiye akupaye nguvu za kupata huo utajiri tena huo udumuo

Tena hutajenga kiburi na kujiona Mungu mtu maana Mungu anawapenda wanyenyekevu wa moyo na wapole wa nafsi.

Jambo hili la kupata pesa kwa Mungu ni mtihani mkubwa sana maana watu wengi tunapenda vitu rahisi na tukipata lazima ijulikane kuwa tunazo.

Tafakari na jifunze utajiri ni swala la rohoni na anae wahi rohoni ndiye anayekula nyama, ukibaki unaongelea mwilini utazeeka na story zako tu za vijiweni.
 
Back
Top Bottom