MJADALA: Ni changamoto gani unakumbana nayo kwa kuchelewa kuoa/kuolewa?

MJADALA: Ni changamoto gani unakumbana nayo kwa kuchelewa kuoa/kuolewa?

hahahahahahahaha lol! ungekumbuka utotoni tu kulamba kamasi mbele kwa mbele 🙂🙂 nimecheka sana kwi kwi kwi kwi hukupiga mswaki kapeace?

Hapo kunyonya kamasi nimekupa salute aisee shikamooooo
Mi mwanangu tu nilishindwa na yalikuwa yamemkaba balaa, nikafumba macho nikayavuta Halafu mbio kwenda kutema na kusukutua
 
Thank you for appreciation BINTIYAZA

unajua aina ya watu kama huyo jamaa ndio wanaotuharibia wanawake, sasa hapo kupata uto tu binti tuwili out of desperation basi ndio ameona wanawake wote mchawi wao pesa tu.

Ulemavu huo!
Hahahaaa! Eti ulemavu!!
 
Habari za jumatatu,

Ni changamoto gani unazipata katika harakati za kutafuta mke kama wewe ni wale waliochelewa kuoa. Kwa mtazamo wa jamii zetu za kiTz mwanaume au mwanamke aliezidi miaka 35 hajaoa au kuolewa ni kuwa amechelewa. Hii sio sheria mwingine anaweza kuwa na mtazamo tofauti.

Mimi binafsi changamoto ninazopata ni hizi;

1.Umri-wanawake wengi kwenye jamii zetu ambao hawajaolewa umri wao ni 22-26. Kwangu mimi bado wadogo yaani tofauti ya umri naiona kubwa.

2.Siko tayari kuoa mwanamke mwenye mtoto-naomba nisieleweke vibaya, huu ni msimamo tu nimeamua hivyo. Changamoto kubwa sasa ni kuwa wale ambao naona ndio umri sahihi wa kuolewa na mimi wengi wao wana mtoto/watoto.

3.Nachagua sana (Naambiwa hivyo inabidi nikubali)-kuoa bila kuchagua inawezekana kweli? Huyu ni mtu nitakaekuwa nae kwa maisha yangu yote sasa inabidi nipate mtu nilieridhika nae.

Tuchangie thread hii kwa lengo la kusaidiana, kurekebisha na kushauri.
Mkuu kati ya maeneo maishani yasiyo taka masihara,ni hili!
Ni vizuri sana kuweka sifa na vigezo vyako unavyo fikiri ndio zitakusogeza ktk kufurahia ndoa,lkn Mungu ndio namba moja!Sisi wakristo tunaamini kuwa mtu hupewa nyumba na urithi na babaye lakini mke mwema hupewa na Mungu.
Kumbuka hakuna hata binadamu aliyekamilika ispokuwa Mungu pekee!
 
Amen..!
 
Back
Top Bottom