MJADALA: Ni changamoto gani unakumbana nayo kwa kuchelewa kuoa/kuolewa?

MJADALA: Ni changamoto gani unakumbana nayo kwa kuchelewa kuoa/kuolewa?

Habari za jumatatu,

Ni changamoto gani unazipata katika harakati za kutafuta mke kama wewe ni wale waliochelewa kuoa. Kwa mtazamo wa jamii zetu za kiTz mwanaume au mwanamke aliezidi miaka 35 hajaoa au kuolewa ni kuwa amechelewa. Hii sio sheria mwingine anaweza kuwa na mtazamo tofauti.

Mimi binafsi changamoto ninazopata ni hizi;

1.Umri-wanawake wengi kwenye jamii zetu ambao hawajaolewa umri wao ni 22-26. Kwangu mimi bado wadogo yaani tofauti ya umri naiona kubwa.

2.Siko tayari kuoa mwanamke mwenye mtoto-naomba nisieleweke vibaya, huu ni msimamo tu nimeamua hivyo. Changamoto kubwa sasa ni kuwa wale ambao naona ndio umri sahihi wa kuolewa na mimi wengi wao wana mtoto/watoto.

3.Nachagua sana (Naambiwa hivyo inabidi nikubali)-kuoa bila kuchagua inawezekana kweli? Huyu ni mtu nitakaekuwa nae kwa maisha yangu yote sasa inabidi nipate mtu nilieridhika nae.


Tuchangie thread hii kwa lengo la kusaidiana, kurekebisha na kushauri.
Bila shaka hii project ilishakamilika.

Miaka 7 sasa imekatika
 
Back
Top Bottom