Mjadala: Ni jambo gani kwenye Maisha yako lilichelewa sana? Ila sasa unaona kawaida sana

Mjadala: Ni jambo gani kwenye Maisha yako lilichelewa sana? Ila sasa unaona kawaida sana

Binafsi, nilichelewa sana kusafiri kwa kutumia ndege!!

Mimi nilichelewa sana kufika Mjini kutoka kijijini katika mkoa niliozaliwa.

Watoto wengi ambao nilikuwa nawazidi umri waliweza kufika mjini kutembea, mimi nikiachwa kupigika kijijini.

Ila Shule ishukuriwe, nilipofaulu kwenda form one nikalamba Jack port ya kupangwa Boarding school iliyopo mkoa mwingine tena jiji kabisa. Hapo ndoto za kukanyaga mjini ambazo zilikuwa zinaniumiza kichwa kila mara zikaenda kutimia. Si hivyo nikaweza kuvuka mipaka ya mkoa wangu kuwashinda wale waliokuwa wananiringishia wao kufika mjini kabla yangu.

Kwa sasa imekuwa kawaida.

Ndoto zilizopo kwa sasa ni nyingi sana ikiwemo hiyo ya kukwea Mwewe hata kwa Local route tu.
 
Ukianza kufikiria at the end wote tunakufa,utakuta cha muhimu ni kusomeka kwenye vitabu vya historia na hiyo ni bahati ya watu wachache katika wengi.
Mfano kuwa maarufu katika kama husika mfano siasa,michezo,sayansi, au tajiri mkubwa.
Sasa ukisomeka kwenye vitabu wewe marehemu itakusaidia nini?
 
Back
Top Bottom