Mjadala: Nini chanzo na tiba ya tatizo la upele kuota kwenye uume?

Mkuu rikiboy shukrani sana kwa mchango wako na mimi nilipata tatizo hili kama miezi miwili iliyopita nimekuwa nikiskilizia kuona kwamba vitaisha vyenyewe lakini wapi.

Baada ya kukutana na hii thread na kuchanganua michango iliyotolewa nikaamua kufuata recommendation yako kwa kununua acyclovir capsules na ile acyclocir cream, Mungu ni mwema one hour later muwasho ukapungua kwa asilimia kubwa. Be blessed wakuu kwa wote mlioshiriki kwenye mjadala huu.
 
Pole sana na hongera kwa kuwa sawa.
 
Kweli una shida mpaka umeamua kuonyesha dushe humu jamvini, basi sawa nenda hospitali tu hakuna namna maana ni dalili za staphylococus areas plus syphilis zamani walikua wanawadunga sindano moja tu nwalikua wanaita ya punda usiombe mazee huamki siku mbili ila ndio tatizo kwaheriiii yaani inakua historia hiyo
 
Habarini za muda huu wakuu

Aisee hili tatizo na mimi limenikuta ni mda umepita nilipitia huu uzi....sasa nimejikuta na mimi limenikuta hili tatizo nilianza kuwashwa mwili yani kuwashwa ile serious hadi nikawa naogopa haikuchukua muda vikaanza kuchipua kijiupele hapa kwenye eneo ya kibovu na baadae uume nao anatokea kama ngozi flani ngumu na ukawa unawasha nikawa napaka mafuta ya nazi pia nikarudi kwenye huu uzi kusoma vizuri na kufuata baadhi ya ushauri uliokua ukitolewa hapa kwenye huu uzi pia nikamuona doctor Mmoja kwenye pharmacy yake hapa kijijini nikamuelezea tatizo langu nakuonyesha hivi kijiupele kwenye eneo la kibovu akaniambia ni tatizo la virus wa HPV akaniambia watibabu yake ni Sindano pamoja na dawa atanipa akaniambia nikatafute elf20 afu niende nayo anichome hiyo Sindano na kunipa hizo dawa nilipoenda kesho yake asubuhi akanichoma Sindano ambayo kama sijakosea ilikua imeandikwa zitheza yani hiyo dawa ipo kwenye kijichupa kidogo ya unga anaichanganya na vimaji flani vipo kwenye kichupa kingine afu anaitingisha kama kwa mda wa dakika 15 20 hivi afu ni dawa nyingi unachomwa Sindano mbili yaani tako la kulia moja na jingine moja inauma kiasi mtu muoga uchomi na dawa akanipa acyclovir yakumeza wiki moja pamoja na B.B.E yakupaka pamoja na azuma kidonge kimoja nikawa nameza 2x3 kwa Siku na kidonge za azuma nilimeza ile Siku tu na kidonge kingine alinipa pia

Sasa ni wiki ya pili sasa tangu nianze kutumia dawa kuwashwa kumeisha kwa asilimia kubwa sana ila sasa vile vijiupele kwenye uume bado vinaendelea na kingine kilitokea kwenye shingo ya kichwa cha umeme hadi kikawa kinatoa maji maji saivi kimekauka ila bado kuna vingine kama naota vidogo vidogo vinaendelea kuoteana na kile kinyama kwenye kibovu kipo vile vile sasa nikaona nitafute dawa nyingine nikarudi pale kwa doctor akaniambia hiyo ndio full doze ila inafanya kazi taratibu niendelee kusubiria sasa mimi naona navyoendelea kusubiria ndio tatizo litaendelea kuwa kubwa nikasema nitafute dawa nyingine ambayo Jina nililitoa hapa kwenye huu uzi inaitwa imiquimod na nyingine podofilox sasa kimbembe ni kwenye kuipata hiyo dawa nikaitafuta hapa kwetu hamna maana me nipo mkoani sasa kuna jamaa yangu yupo dar nimemuomba anitafutie kwenye pharmacy kubwa kubwa kule kariakoo ameniambia ameikosa..sasa nimebaki na wasiwasi sijui pakuipata nawaza vikiendelea itakuaje sitopiga tena shoo kweli daah hizi ngono naacha kama sio kupunguza hadi nitakapo oa mke wangu.. nimeweka kapicha hapo lengo ni kurahisisha kupata msaada

NB: Nimepima damu afya yangu ipo vizuri maana ndio cha kwanza nilifanya.. nilichoshindwa nikwenda kufanya vipimo zaidi vya huu ugonjwa maana sina bima.

Naomba kuwasilisha kwa msaada waungwana View attachment 1734415
View attachment 1734421
View attachment 1734426
 
Duh...
Aisee pole. Kuna vitu nikionaga huwa nasema sit***bi tena. Ni wazi una std na umeipata mahali. Natumaini umeenda hospitali mkuu.
 
Naugonjwa kama wa ndugu yetu hapo na mm unanisumbua nimetumua tube nyingi na caps (vidonge) vya aina tofauti tofauti ila bado tatizo lipo naomba msaada wenu.
Maana nimeenda hosptal nimeandikiwa sindano nimechoma ila vilipungua ila bado kuna sehemu vipo
 
Tumia dawa vidonge aclovir kwa siku 14 na scaboma ni ya kupaka hyo, vidonge unameza 2x4(kila baada ya masaa sita unameza)
 
Msaada wadau hivi vipele vinawasha Na ukivikuna ndo kama unavizidisha kuwasha yani hadi mwili unawaka moto usiku kucha silali vipo mapajani,miguuni kidogo,vidole vya mikono,mabegani,tumboni karibu na kitovu,kiunoni na kwenye uume
Msaada wenu pliz natanguliza shukrani Zangu zote kwenu
 
Nenda hospital haraka inawezekana kabisa si tatizo kubwa labda umekula kitu ambacho una allergy nacho hivyo kikiisha mwilini mwako baada ya siku chache muwasho na vipele vitapotea.
 
Nenda hospital haraka inawezekana kabisa si tatizo kubwa labda umekula kitu ambacho una allergy nacho hivyo kikiisha mwilini mwako baada ya siku chache muwasho na vipele vitapotea.
Sawa mkuu ila hii hali nakumbuka kwa mara ya kwanza niliiona kwa jamaa angu nayeishi nae gheto alikua nayo sasa naona na mim nimeipata
 
Wahi hospitali Mkuu kisha lete mrejesho.
 
Ila hiyo picha uliyoiweka mbona umeiondoa?
Hahahahaha lol!

Sawa mkuu ila hii hali nakumbuka kwa mara ya kwanza niliiona kwa jamaa angu nayeishi nae gheto alikua nayo sasa naona na mim nimeipata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…