Gfav
JF-Expert Member
- Oct 7, 2022
- 378
- 669
Habari zenu wana JF, samahani sana kwa usumbufu kama vile tujuavyo misemo ya wahenga kuwa mficha uchi hazai.
Since mwezi wa nne nasumbuliwa na hili tatizo nimetumia dawa nyingi sana ant fungus kama zote za tube mpaka za kopo ila bado tatizo linanisumbua.
Ninawashwa sana mwilini na vijipele vimetokea mkononi na sehemu za siri, nimepima hospital kama BURHAN, Regency wanasema siumwi kitu ila hali yangu mimi naona inazidi kua mbaya.
Majuzi nimepima hospitali ya mtaani wakasema na syphilis nimeanza matibabu ya sindano zile nne za mwezi mpaka sasa nishachoma sindano 2 ila bado hali iko vile vile tena ndio inazidi kabisa.
Mwenye msaada naomba anisaidie nawashwa sana mwili.
View attachment 1183912View attachment 1183913View attachment 1183915
UFAFANUZI WA JUMLA TATIZO HILI KUTOKA KWA MTAALAMU
MASUNDOSUNDO, MALENGELENGE, VINGWARU NA VIPELE LAINI NA VIDOGO SEHEMU ZA SIRI
Ukiwa mzima mshukuru Mungu mara mia mia, sisemi ukiwa sio mzima usimshukuru Mungu la hasha ila ninataka kuonyesha msisitizo ya kwamba kuna watu wanateseka na mardhi ya kila aina ile hali wewe mzima kabisa wala huoni sababu ya kumshukutu Mola wako.
Leo ningependa kuongelea habari ya #masundosundo, #vipele laini na #malengelenge sehemu za siri, ni vitu vidogo lakini mara nyingi vinaleta usumbufu hadi wengine kuanza kudhania wameathirika, kumbe sio. Kumbuka ili kujua umeathirika na #VVU lazima uwe umepima. Tabia ya kujipima wenyewe haifai na ni hatari sana. Kuna watu wanaota vinyama laini vidogovidogo kwenye sehemu za siri yaani nfano kichwa cha uume, mashavu ya uke, ndani kwenye mirija ya mkojo, maeneo yanayozunguka haja kubwa, kwenye makoo na mdomoni. Aidha wengine wanaota vipele vidogo vidogo sehemu mbalimbali za siri vinavyopasuka na kuacha maji mnato ivi na kisha kuunda kidonda cha wastani. Usikae na ugonjwa onana na madaktari au washauri wa afya ili uweze kuanza safari ya matibabu.
MAAMBUKIZI NA CHANZO CHA MAGONJWA HAYA ni ukosefu wa kinga imara ya mwili, kujamiiana hovyo kwa njia ambazo sio za asili na kuvaa nguo za ndani chafu. Magonjwa haya ni ya kuambukiza na pia ya kujitakia. Wadudu jamii ya virusi,bacteria na fangasi hupata nafasi kutokana na tabia hizoo na kuanza kushambulia maeneo haya niliyoyataja kirahisi sana.
DALILI ZAKE
- Kuna vinavyoonekana kwa macho lakini vingine huwa havionekani kabisa utasikia muwasho mkali kama wa kuunguza na moto kwa mbali, iwapo utakuna unaweza tokea michubuko inayochelewa kupona. Iwapo vinaonekana basi ni kama unavyoona katika picha hapo chini.
- Maeneo yaliyozungukwa na masundosundo saa ingine yanapata ganzi
- Kutokwa na uchafu mzito sehemu za siri kama ugonjwa upo kwa ndani.
- Kutokwa na damu ukeni hasa baada ya kufanya tendo la ndoa, ile hali hauko bleed.
UBAYA WA MAGONJWA HAYA
- Usumbufu wa kujikuna kuna sehemu za siri kila wakati wakati mwingine utajisahau hata mbele ya wakwe
- Maumivu
- Ukosefu wa uhuru
- Kuchochea magonjwa mengine
- Kukosa uhuru wa tendo la ndoa
NAMNA GANI UTAJIKINGA
Kama tayari umeshapata na unamagonjwa haya kwa muda mrefu au huwa yanakuja na kutoweka basi wasiliana nasi kwa ushauri zaidi. Ili uweze kupata ushauri kwa ajili ya kuongeza kinga yako ya mwili, kupata food suppliment ili kuweza kudhibiti wadudu hawa waharibifu na wasumbufu.
- CHAKULA NI KINGA YA KWANZA, kama hujapata bado basi hakikisha unakula chakula bora chenye uwingi wa vyakula vyenye kukukinga dhidi ya mardhi na vyenye kujenga nguvu ya mwili na kuzalisha seli kwa wingi. Vyakula hivyo ni pamoja na vyakula vyenye protein kwa wingi, mbogamboga na matunda
- EPUKA NGONO ZEMBE NA NGONO KIYUME NA MAUMBILE
- Wanawake wasagaji achana na mchezo huo
- Kuwa msafi kila wakati (hasa mliopo sehemu za joto kama DSM). Badili nguo za ndani mara kwa mara, wanaume mara nyingi utakuta mtu anavaa jeansi moja wiki nzima, hii siyo sawa.
- Vaa chupi zilizotengenezwa kwa pamba na usivae nguo nyingi za ndani.
- Siku za bleed tumia pedi za pamba, zenye uwezo wa kuingiza hewa safi na kutoa hewa chafu na kisha kuuwa wadudu wa aina yeyeto walio na uharibifu kwa mwili wako. Sisi tunapendekeza pedi za #Neplily kama hujawahi zitumia jaribu inaweza kuwa ndio mkombozi wako.
USHAURI KWA WADADA – Mapenzi ya kusagana, kunyonyana sehemu za siri na mapenzi kinyume na maumbile hayafai. Tafuta namna ingine ya kumridhisha mwenza wako. Najua wadada wengi ni wasafi lakini wachache ni wachafu kabisa, pia wengi hamtumii pedi salama.
USHAURI KWA WAKAKA – Mara nyingi wakaka hukutwa na malengelenge kwenye uume na vile vipele laini vyenye kutoa maji, masundodundo wengi yanawatokea kwenye haja kubwa. Wengi hubakia kuwa cariers kwa kuendelea kuambukiza wanawake wengine ile hali wao hawana dalili, kama mpenzi wako ana dalili mojawapo kati ya hizo hapo juu basi na wewe lazima upate tiba ili kumaliza tatizo hili kikamilifu.
Achana na tabia mbaya za ngono kinyume na maumbile, kupiga punyeto, kula vyakula visivyokuwa na matunda na mboga, kuvaa nguo chafu muda mrefu bila kufua, kutumia madawa ya kulevya na pombe kali kupindukia. Kama tayari una tatizo hili tafadhali kwa sasa lina ufumbuzi na utatuzi ambapo utatumia
BAADHI YA MAONI NA USHAURI KUTOKA KWA WADAU WA JF
---
---
---
---
Ni either wewe sio straight or hao madaktari are no straight, hili andiko uliloandika sijui lishe, uchafu bla bla ni la hovyo.