HOJA MJADALA: Nini kifanyike kuwadhibiti madalali wa nyumba, vyumba, mashamba, gari n.k?

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

Stanboy

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2013
Posts
1,115
Reaction score
1,328
Habari wakuu,

Kama kichwa cha mada kinavyojieleza hapo juu, kumekuwa na changamoto kubwa katika suala zima la kupanga na kununua nyumba, mashamba, magari na kadhalika.

Hawa watu wanaojulikana kama madalali au 'mtu wa kati' wamekuwa wakifanya maisha kuwa magumu kila siku yaani ni kero kwa kifupi. Hawana huruma hata kidogo, imagine nyumba inauzwa milioni 20 yeye atataka akuuzie milioni 50.

Kwenye vyumba ndo usiseme kuonyeshwa tu 10,000/= haijalishi utaipenda ama vipi. Ukishaipenda inakubidi umlipe malipo ya mwezi mmoja tena hawapunguzi hata 100/=.

Mbaya zaidi hawalipi kodi wala mapato yao hayana msaada wowote kwa nchi na jamii kwa ujumla zaidi ya kuwaumiza wananchi.

Je, unafikiri nini kifanyike kuwadhibiti?
 
Sijaelewa unaposema mapato yao hayana faida yeyote kwa nchi, jamii Zaidi ya kuwaumiza tu wananchi.

Kwa nini nimesema hivyo: Hawa madalali wanasomesha, wana familia zinazowategemea n.k. Nadhani hao wote wanafaidika na vipato vya hawa madalali. Nchi inaweza kufaidika na vijana wanaosomeshwa na hawa madalali kwa namna moja au nyingine, kwani wanaweza kuja kulitumikia taifa au kuja kulipa kodi kutokana na shughuli zao watakazokuja kuzifnya.

Hawa wasingejiajiri kwa kuwa madalali pengine wangekuwa omba omba barabarani ambao tunawapiga vita kila siku; pengine pia wangeweza kuwa majambazi (Hasara kwa taifa); Au wangekuwa wanaendelea kuilaumu Serikali kwa kutotoa ajira.

Nafikiri suala la muhimu ni kuboresha/kurasilimisha shughuli zao tu
 
Umeeleza vizuri kwa mtazamo wako,
lakini kiwango wanachotoza ni kikubwa mno na kuna harufu ya utapeli pia
 
Ukienda pale kariakoo gerezani kutafuta spare za gari ndo utajuta. Yani bei ya spare una patana na mtu wa 3.huo mlolongo wa watu halo kati wote wanataka hela.
Nawasihi wenzangu ukienda gerezani kununua spare siku ya kwanza ukiona spare unayotaka usinunue. Subiri kama week uende wew mwenyew utanunua kwa bei ya chini mpaka utashangaa
 
Umeeleza vizuri kwa mtazamo wako,
lakini kiwango wanachotoza ni kikubwa mno na kuna harufu ya utapeli pia
Ni kweli mkuu, inawezekana kiwangi ni kikubwa. Na hapo ndipo napoona kuna haja ya kurasimisha shughuli zao ili kuweka mambo yote hayo ikiwemo ya bei n.k
 
Sijaelewa unaposema mapato yao hayana faida yeyote kwa nchi, jamii Zaidi ya kuwaumiza tu wananchi.

Kwa nini nimesema hivyo: Hawa madalali wanasomesha, wana familia zinazowategemea n.k. Nadhani hao wote wanafaidika na vipato vya hawa madalali. Nchi inaweza kufaidika na vijana wanaosomeshwa na hawa madalali kwa namna moja au nyingine, kwani wanaweza kuja kulitumikia taifa au kuja kulipa kodi kutokana na shughuli zao watakazokuja kuzifnya.

Hawa wasingejiajiri kwa kuwa madalali pengine wangekuwa omba omba barabarani ambao tunawapiga vita kila siku; pengine pia wangeweza kuwa majambazi (Hasara kwa taifa); Au wangekuwa wanaendelea kuilaumu Serikali kwa kutotoa ajira.

Nafikiri suala la muhimu ni kuboresha/kurasilimisha shughuli zao tu
we lazma utakua dalali

Sent from my HUAWEI LUA-U22 using JamiiForums mobile app
 
Madalali wapumbavu sana,chumba cha elfu kumi anaweza akakwambia elfu 50 ili yeye apate cha juu.

Sent from my ALE-L21 using JamiiForums mobile app
 
Sijaelewa unaposema mapato yao hayana faida yeyote kwa nchi, jamii Zaidi ya kuwaumiza tu wananchi.

Kwa nini nimesema hivyo: Hawa madalali wanasomesha, wana familia zinazowategemea n.k. Nadhani hao wote wanafaidika na vipato vya hawa madalali. Nchi inaweza kufaidika na vijana wanaosomeshwa na hawa madalali kwa namna moja au nyingine, kwani wanaweza kuja kulitumikia taifa au kuja kulipa kodi kutokana na shughuli zao watakazokuja kuzifnya.

Hawa wasingejiajiri kwa kuwa madalali pengine wangekuwa omba omba barabarani ambao tunawapiga vita kila siku; pengine pia wangeweza kuwa majambazi (Hasara kwa taifa); Au wangekuwa wanaendelea kuilaumu Serikali kwa kutotoa ajira.

Nafikiri suala la muhimu ni kuboresha/kurasilimisha shughuli zao tu
Kwa kumsaidia zaidi ni kuwa katika dunia hii huwezi kuukwepa udalali. Hata huko nchi zilizoendelea ni udalali ndio unafanyika kama kuuza wachezaji Akina Lukaku, Pogba, Ronaldo......hata makocha kuna madalali wanawauza. so inachotakiwa tu hawa wa kwetu watambulike kisheria na wawe na ofisi. Fikiria wewe ni mgeni dar umetoka mkoa. Ni nani atakusaidia kupata au kutafuta nyumba au kujua nyumba iliyo empty. Au kufahamu nani anauza gari, shamba au kiwanja.
 
Aisee umeongea point.. Wachukue tuu 10% inawatosha.. Yani wao wanataka kodi ya mwezi mzima.. Imagine unataka apartment ya mil 2 kwa mwezi.....
 
wanakusaidia na kukurahisishia huku wanakuumiza

Sent from my GT-I9300 using JamiiForums mobile app
 
Ukienda kwa mwenye nyumba direct hakubali...anakuambia madalali watamletea shida
Shida gani, kwani nyumba si yake!
Hao madalali wa namna hiyo ni majambazi..., pengine waje wafanye fitina ili mpangaji ahame tu au wamwibie n.k
 
Kwa kumsaidia zaidi ni kuwa katika dunia hii huwezi kuukwepa udalali. Hata huko nchi zilizoendelea ni udalali ndio unafanyika kama kuuza wachezaji Akina Lukaku, Pogba, Ronaldo......hata makocha kuna madalali wanawauza. so inachotakiwa tu hawa wa kwetu watambulike kisheria na wawe na ofisi. Fikiria wewe ni mgeni dar umetoka mkoa. Ni nani atakusaidia kupata au kutafuta nyumba au kujua nyumba iliyo empty. Au kufahamu nani anauza gari, shamba au kiwanja.
Ulaya hamna madalali wale ni mawakala wanaotambulika kisheria kama ni hivyo basi watu wangekuwa wanakuja tu kariakoo kutafuta mchezaji. Mfano kina Mino Raiola, Jorge Mendes

Sent from my TECNO_W4 using JamiiForums mobile app
 
Dalali, wakala......wote ni kitu kimoja. tofauti tu wale wanafanya kisheria na wamesajiliwa. Na hawa wetu wanafanya kienyeji........baadala ya kwenda Tigo ofisini kwao kutuma pesa unamtafuta wakala yaani mtu wa kati unatuma hela naye anapata cha juu chake kutoka tigo. Kifupi huyo ni Dalali. .....au baada ya kumfuata Ronaldo direct kumshawishi ahame unamfuata Dalali wake aliyeruhusiwa au mwenye leseni ya kumuuza. wakala ni Dalali. Na kazi yao na lengo Lao wote ni moja kupata cha juu. Yaani watu wa kati. Aka middle man.
 
Na awakwepeki ktk dunia ya sasa,,, ,,kuna vitu ukitaka kuuza ndio utajua muhimu wa dalali, ,,iyo serikali yenyewe inadalaliwa
 
Back
Top Bottom