Utakatishaji pesa ni nini? Kitendo cha kufua pesa ni pale ambapo mtu mwenye pesa chafu Za ufisadi (toka kwenye upigaji wa miradi mbali mbali ya seriakali), au pesa chafu za uuzaji wa madawa ya kulevya, au pesa chafu zilizolowa damu toka kwenye ‘conflict zones’ huko DRC, anapotumia mianya mbali mbali kuzisafisha na kuziingiza katika mfumo rasmi wa kibenki kana kwamba zilikuwa ni pesa safi na halali kabisa.
Hadi sasa, kulingana na mwanya uliopo kisheria, njia safi na rahisi kabisa ya kutakatisha pesa chafu / haramu ni kwa kupitisa taasisi za kidini, hivyo basi maharamia wengi huanzisha taasisi za kidini na majumba ya ibada, ambapo kama kuna bilioni kadhaa zimepatikana toka kwenye shughuli zao za kiharamia, huzipeleka kwenye taasisi zao za kidini na zinapokelewa kama sadaka swafi na halali kabisa.
Kumbuka, Sadaka haipigwi kodi ya aina yeyote, haina mkataba wa aina yeyote, haitolewi risiti ya EFD kwa namna yeyote, jina la aliyetoa sadaka ni siri (hata vitabu vya sini vinasema iwe siri), kiwango cha sadaka anachotoa mtu ni siri. Kwahiyo hata Andrew Chengge angesema apige vijisenti vyake huko halafu avipeleke kwa Mwamposa kama Sadaka, na kisha Mwamposa akaenda kununua Kiwanja cha Chennge chenye thamani ya milioni 100 kwa bei ya shs.Billioni. 3 ambapo zitaingizwa kwenye akaunti ya benki ya Chennge kama pesa safi na halali ya mauzo ya kiwanja chake, hapo ianakuwa amezisafisha na zinatakata kabisa!
Hapo andrew Ataenda kudraw hizo pesa benki kadri atakavyohitaji na kula maisha, na hapo pesa inakuwa imatakatishwa. Bila kusahau, commission atakayopewa Mwampusa itamwezesha na yeye kuendesha kanisa lake na familia yake kwa anasa za aina yake, maana hapo biashara inakuwa imetiki.
Mfano mwingine ni tusema Makonda anabilioni zake 100 za madawa ya kulevya, anampelekea Gwajima kama sadaka, kumbuka sadaka ni siri, haipigwi kodi, haina mkataba wala risiti ya EFD. Kisha anaenda kununua shamba la Makonda lenye thamnai ya milioni 100 kwa bilioni 100, zinaingizwa kwenye akaunti ya benki kama pesa safi, na zingine anabaki nazo Gwajima kama commision yake anayoweza kwenda kununua hata private jet safi kabisa.
Hapo Makonda ataenda kudraw oesa benki kama pesa safi na halali kabisa iliyotakatishwa.
Wenye ujuzi zaidi tunaomba mjazie nyama..
Baada ya hapo , mtueleze ni vipi huyo Kimaro imekuwa inavyokuwa..., msipende kugusa maslahi ya watu halafu mkategemee kubaki salama...