CHADEMA kina mbinu nyingi sana zinazobadilika kila wakati kuendana na wakati, mazingira na mahitaji ya nyakati.. CHADEMA digital ni mojawapo ya mbinu iliyowachapa vilivyo wapinzani wao in this case CCM
Pia nipende tu kukuhakikishia kwamba kuna think tank nyingine nje ya CHADEMA na ndani ya mamlaka inatoa support kubwa sana kwakuwa nayo imechoshwa mno na hiki kikongwe CCM
Hizi think tanks zote ni tool mojawapo yenye nguvu sana kuelekea kuikomboa nchi ndio maana nimeziweka zote kwenye kundi moja ndani ya CDM japo kiutendaji kila moja ina jukumu lake
Sawasawa mkuu, ni kweli Chadema Digital na Think tank zipo na kwa kweli zimejitahidi sana kufanya kazi zake katika mazingira magumu sana ya kuzuiwa.
Lakini kuna baadhi ya tools au nyenzo za ziada ambazo zipo na ambazo husaidia hizi Chadema dijitali na think tank na ntazizungumzia chache.
Kuna "events" yaani shughuli maalum ya kukutana katika eneo la mgombea mtarajiwa. Hapa si lazima kuwe na mkutano mkubwa sana bali shughuli ndogo tu ambayo yahusisha mgombea na wanachama wachache na kisha ujumbe kusambazwa mitandaoni kuhusu yalojiri katika tukio lile.
Pia kuna "organise" yaani uratibu na mawasiliano ambapo watu wa nje ya Chadema huweza kusaidia kutengeneza kampeni kiasi cha kuweza kushindana na hii hufanywa katika eneo husika la mgombea mtarajiwa. Kwa mfano hivi juzi CCM imefanya ziara zake magharibi mwa Tanzania kujaribu kuwazuabaisha wananchi kuwa wapo makini na usimamizi wa ilani ya uchaguzi na utekelezaji wake.
Lakini matatizo ya msingi ambayo Chadema bado ingepaswa kufuatilia na kukazia ni si tozo peke yake bali hali halisi ya uchumi wa nchi na wapi serikali imefeli na wao Chadema wana agenda zipi tofauti na zile za CCM na kisha kuzitoa kwa wanachama wake kupitia mitandaoni.
Mwisho, kuna kufikia lengo au "achieve" hii ni kwa ajili ya kueleimisha wapiga kura kuhusu mijadala inoendelea kwa kutumia "platform" ya mtandaoni au "jargon buster" ambapo maneno magumu kueleweka hufanyiwa upembuzi. Pia hapo wananchi wataelimishwa kwa mfano ni kwanini serikali yakopa fedha nje, fedha hizo zitalipwa vipi na kwa njia zipi na ufafanuzi wa jargon buster nini maana ya dhamana za serikali, mfumuko wa bei, nakisi ya bajeti, deni la taifa na serikali kujaa fedha za kutosha yaani surplus kwatokana na nini.
Kisha hapo Chedema huja na mbadala na ufafanuzi wao watafanya nini kuweka sawa uchumi, kudhibiti mfumuko wa bei na itasimamia vipi ukusanyaji kodi na kwa njia zipi mpya. Hivyo hii "learning platform" ni eneo zuri sana kuwafikia wale vijana wa "grassroots" ambao ndo Tanzania ya kesho.