Kama una mbinu iweke hapa au wapelekee CDM huko ofisini kwao. Lakini ninavyoona sioni kama utakuwa na mbinu yoyote yenye nguvu, na ifanye kazi zaidi ya machafuko. Njia za kistaarabu zimeproove failure katika kupambana na CCM. Ifahamike CCM haitumii njia za kistaarabu kubaki madarakani, itakuwa ni kosa la wazi kutegemea njia za kistaarabu wakati wenzako wanatumia uhuni kubaki madarakani.
Ukisema kama nina mbinu niwapelekee huko ofisini kwao unakuwa hutumii njia sahihi ya kufikiri kwa undani kwani waonyesha kukata tamaa lakini amini nakuambia hiki tukiongeacho hapa kina maana kubwa sana.
Bado naamini machafuko si njia sahihi bali njia za kawaida tu zatosha. Lakini kwanza tuna budi kuangalia hali ya kiuchumi ya upinzani je, wana hali gani kifedha? Shughuli za uendeshaji wa chama wahitaji fedha na mipango, je Chadema ina vyanzo imara vya fedha ambavyo huko mbele vitaweza kuwa mbadala wa ruzuku kutoka serikalini?
Fedha nyingi huelekezwa katika maeneo kama ya kidijitali na huko ndiko kwenye kukiimarisha chama lakini je ni kwa mtindo upi?
Ok, tuseme Chadema yaanza na uchaguzi wa serikali za mitaa hii ndo njia sahihi ya kujenga "base" ya viongozi wengi ambayo itasaidia kupatikana wabunge wengi kwa mtindo mmoja tu.
Sasa basi, wewe wataka kuwa diwani wa kata fulani lakini si mhuni, umesoma uzuri hadi chuo kikuu na ni lazima ushinde katika kata yako. Hivyo Chadema digital itaandaa "profile" ya mgombea, vipeperushi vinavyomuongelea mgombea na mwisho sera zake zote anoziuza kwa wapiga kura. Hali ni hiyohiyo kwa wagombea ubunge na hiyo si tu bila mkutano wa halaiki bali vipeperushi vyenye ujumbe tosha kwa mpiga kura.
Hizi ni hatua ambazo zapaswa kutekelezwa mwanzoni katika ya upigaji kura ya maoni na namna ya kuufikisha ujumbe kwa wananchi kulinganisha sera au ilani ya CCM na ile ya kwenu, wapi CCM wameshindwa na ninyi au mgombea wenu atafanya nini tofauti.
Hii hatua ya Chadema UNGANISHA au "connect" ni hatua ambayo ikifika kwa walengwa mgombea anakuwa hana shida ya kujitambulisha maana tayari ajulikana kabla hata ya siku ya mkutano wa kampeni.
Mambo yaliyomo katika hii "Connect" au UNGANISHA ni pamoja na uchapaji, utumaji na uwasilishaji wa ujumbe ama kumtambulisha mgombea au kuweka msisitizo wa siku ya kupiga kura.
Hivyo katika eneo husika la kugombea udiwani au ubunge kipeperushi maalum kinachomhusu mgombea kwamba yeye ninani, na ana sera zipi na taarifa zingine atapewa mpiga kura ili achambue.
Asikwambie mtu, hakuna siri kubwa ya kupiga kura kama utumiaji wa sanduku la kura hivyo kwenye hili mbinu kadha wa kadha huitajika ili kuhakikisha wingi wa kura unaleta hofu kuu kwa watawala na DS yao.
Mbinu ingine ni ile ya mvuto na kusajili wanachama katika kila kata kwa kutumia mfumo wa kidijitali na sio kukusanya panyaroad mitaani na wahuni wengi ambao wataviuruga mrindimo wa kisiasa. Hivyo Chadema Digital yapaswa kuweka platform ndani ya tovuti yake ambayo itasajili wanachama wapya kwa kutumia Chadema Digital App ili kusajili vijana au kuwatambua na kuwafanyia uhakiki wale "grassroots" wote ambao ndo nguzo muhimu ya uimarishaji na uhamasishaji.
Eneo hili la Chadema Digital CDM hawajalitendea haki kwani bado tovuti yao imejazwa mipicha tuu kila kona badala ya mambo mengine muhimu sana katika ulimwengu wa mitandao.
Sasa nimalize kwa kusema zipo njia nyingi zaidi ambazo hata wewe bado huzifahamu na labda mwenyekiti Mbowe atanielewa, kuna "Doorstep App", kuna "contact creator" nyakati za kampeni na pia kuna "Word Press Network". Hizi ni zile za kuingia ndani zaidi kumpata na kumshinda mtesi wako.
Tuendelee ntazungumzia kiaina maana hizi ni mbinu na huwezi kuweka mbinu hadharani.