Mjadala: Upinzani utaanzaje kujipanga kwa uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2024 na hatimae uchaguzi mkuu wa uraisi wa 2025 ndani ya mazingira magumu?

“Maridhiano” ni moja ya neno la kishenzi na la kipumbavu kupata kuli sikia katika taifa hili toka tumepata uhuru wa bendera 9/12/1961.
 
Sawasawa mkuu, ni kweli Chadema Digital na Think tank zipo na kwa kweli zimejitahidi sana kufanya kazi zake katika mazingira magumu sana ya kuzuiwa.

Lakini kuna baadhi ya tools au nyenzo za ziada ambazo zipo na ambazo husaidia hizi Chadema dijitali na think tank na ntazizungumzia chache.

Kuna "events" yaani shughuli maalum ya kukutana katika eneo la mgombea mtarajiwa. Hapa si lazima kuwe na mkutano mkubwa sana bali shughuli ndogo tu ambayo yahusisha mgombea na wanachama wachache na kisha ujumbe kusambazwa mitandaoni kuhusu yalojiri katika tukio lile.

Pia kuna "organise" yaani uratibu na mawasiliano ambapo watu wa nje ya Chadema huweza kusaidia kutengeneza kampeni kiasi cha kuweza kushindana na hii hufanywa katika eneo husika la mgombea mtarajiwa. Kwa mfano hivi juzi CCM imefanya ziara zake magharibi mwa Tanzania kujaribu kuwazuabaisha wananchi kuwa wapo makini na usimamizi wa ilani ya uchaguzi na utekelezaji wake.

Lakini matatizo ya msingi ambayo Chadema bado ingepaswa kufuatilia na kukazia ni si tozo peke yake bali hali halisi ya uchumi wa nchi na wapi serikali imefeli na wao Chadema wana agenda zipi tofauti na zile za CCM na kisha kuzitoa kwa wanachama wake kupitia mitandaoni.

Mwisho, kuna kufikia lengo au "achieve" hii ni kwa ajili ya kueleimisha wapiga kura kuhusu mijadala inoendelea kwa kutumia "platform" ya mtandaoni au "jargon buster" ambapo maneno magumu kueleweka hufanyiwa upembuzi. Pia hapo wananchi wataelimishwa kwa mfano ni kwanini serikali yakopa fedha nje, fedha hizo zitalipwa vipi na kwa njia zipi na ufafanuzi wa jargon buster nini maana ya dhamana za serikali, mfumuko wa bei, nakisi ya bajeti, deni la taifa na serikali kujaa fedha za kutosha yaani surplus kwatokana na nini.

Kisha hapo Chedema huja na mbadala na ufafanuzi wao watafanya nini kuweka sawa uchumi, kudhibiti mfumuko wa bei na itasimamia vipi ukusanyaji kodi na kwa njia zipi mpya. Hivyo hii "learning platform" ni eneo zuri sana kuwafikia wale vijana wa "grassroots" ambao ndo Tanzania ya kesho.
 
Ndomana nikasema maridhiano yanatakiwa yawe na timeframe.

Unadhani CDM watasusia uchaguzi Ili CCM wapete kama kipindi Cha nyuma????

Ndugu, nina uwezo mkubwa sana kuona MBALI na MBELE sana. Muda wa mabadiliko umefika, bila kujali mamlaka zinataka au hazitaki.

Hatupasi kusubiri wananchi waamue wenyewe kukataa Hali iliyopo, maana Mimi nimekuwa nikiona kundi kubwa sana la wananchi wasio na Idadi wakiwakimbiza watu walovaa suti na tai nyekundu kuwafukuza Kutoka viti walivyokalia.

Si mbali, niyaandikayo yatatokea.

Ameeeen
 
“Maridhiano” ni moja ya neno la kishenzi na la kipumbavu kupata kuli sikia katika taifa hili toka tumepata uhuru wa bendera 9/12/1961.

Nimesema mara kadhaa humu jukwaani kuwa katika mambo Mbowe na CDM wamechemsha ni kukubali huo utapeli uitwao maridhiano. Unakubali maridhiano ili aliyeko madarakani atawale bila pressure, matokeo yake amejua unatii atakacho, anafanya yale yale anayokuzuia ww kufanya.
 
Get prepared, bt usisahau KANU kiliangushwa na majabali yaliyotoka ndani ya chama kuungana na wapinzani .

CDM ikinyamaza, tegemea uasi Kutoka ndani ya chama tawala, lazima watagombana kugombea madaraka.
 
Upinzani wa hapa nchini hawana mpango wowote mpaka sasa wa kushinda chaguzi za 2024 na 2025.
Mkuu, umesema maneno machache lakini ni maneno mazito sana.

Ni kwanini wadhani Upinzani nchini hawana mpango wowote wa kushinda chaguzi za 2024 na 2025?

Karibu sana mkuu, fafanua.
 
Kufanikisha haya CDM itafute watu makini Hasa ktk platform ya JAMII forum siasa wenye uwezo wa kuleta taarifa na mijadala ya kimkakati.

Waliopo wengi jukwaani wanaendesha siasa za matusi na kejeli, hawaangalii hoja, humshambulia mtoa hoja ikiwa tu wanajua ni mwana CCM!!!!
 
Maridhiano mara nyingi ni huitwa "whitewash" yaani wapiga rangi nyeupe pale penye madoa yanochafua.

Afrika Kusini walikuwa na maridhiano lakini leo hii Mandela na Desmond Tutu hawapo na bado Afrika Kusini kuna shida waafrika kusini weusi wana shida huku idadi ya wasoajiriwa kuongezeka kiasi cha kuanza kushambulia wageni na pia bado njia za kawaida za kumiliki uchumi zikiwa zimebinywa au kupewa watu wachache wenye kamba zilifungwa vifundo vya chama tawala.

Hivyo basi, maridhiano kwa Tanzania yangekolezwa na kuwepo kwa uhuru wa wananchi kuulizwa masuali katika kura ya maoni kama wataridhia mabadiliko ya katiba au watataka ilioyopo iendelee. Hapo suala zima la kuwepo kwa demokrasia nchini linakuwa limetimilizwa na si kubatilishwa.
 
Ni kweli kabisa mkuu na hizi platforms si tu kwa JF bali sehemu zingine tofauti.

Na kuhusu mtoa mada hii naomba nifafanue kidogo na nadhani nimesahau kuweka tahadhari mwanzoni kwa mada.

Mie si mwanachama wala mfuasi wa CCM naomba nieleweke hivyo.

Isipokuwa kuanzia mwishoni mwa 2015 nilianza kumfuatilia raisi aliepita baada ya kuona maono yake kuwa huenda yangetufikisha mahala, na kweli ikawa angalau tukafikia uchumi wa kati ambao tuliambiwa na vyombo vya fedha vya kimataifa vya IMF na WB na sidhani kama hayati JPM aliwahonga watu hawa ili watoe hizio taarifa.

Hivyo nadhani ntakuwa nimetoa mwanga kwa wale wenye shaka juu ya msimamo wangu.
 
Vyombo vya dola hufanya vitendo vya kikatili kutokana na hali yao kiuchumi kuwa mbaya kwao , au tu ni roho mbaya na ukatili, je, ni elimu duni juu ya sheria au tu ni kufuata amri kutoka juu?
 
Nashauri Mr Mbowe aongeze umakini Kwa suala la maridhiano.

Timeframe ni muhimu, ninanusa harufu ya HADAA mahali!!!!
 
Nashauri Mr Mbowe aongeze umakini Kwa suala la maridhiano.

Timeframe ni muhimu, ninanusa harufu ya HADAA mahali!!!!
Ni kweli, lakini pia wapiga kura huwa wanyiwa nafasi ya kuuliza zile "terms" za maridhiano maana ni mwisho tu sie huambiwa kulikuwa na mazungumzo kati ya kiongozi wa nchi na kiongozi wa upinzani.

Kisha tusisahau kuwa Mbowe si mbunge na ili aweze kupata nguvu zaidi nadhani yupo makini na hili kuhakikisha anarudi bungeni ili kwanza awe mbunge na kisha aendelee kuwa kiongozi wa upinzani palepale eneo la tukio Bungeni.

Kuhusu Timeframe hii ni uzuri ukafafanua mkuu wataka timeframe ya namna gani?
 
Waziri Mkuu kwa mujibu wa Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 anatokana na chama chenye wabunge wengi Bungeni,hivyo hoja yako inategemea na chama chenye wabunge wengi,pia tambua kuwa CHADEMA ni Watanzania,CCM ni Watanzania na vyama vingine ni Watanzania vile vile,swala la uongozi ni nani anakubalika na wananchi na si team kama hoja yako inavyojikita.Na nchi yoyote duniani huwa haiongozwi na akili za Rais aliyepo madarakani bali sheria za nchi ndizo huongoza .
Tuache mawazo yasiyo na tija kuwa nani anafaa huo ni ubaguzi,Soma Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 ibara ya 12(i),(ii) na 13(i)(ii)(iv)&(v)
 
Well said mkuu.

Tunao watu ambao bado wahitaji elimu hivyo jitahidi kuelimisha.
 
Time frame ya Maridhiano ninayomaanisha ni:

1. Ikiwa, Maridhiano yataendelea Hadi 2024, halafu yakavunjika, CDM itakuwa imepata hasara Kwa kiasi Gani??? Lazima iwe calculated.

2. Ikiwa watakubalina RASIMU alosimamia Judge WARIOBA irudishwe mezani, na wakiruhusu uundwaji wa Tume na Katiba mpya ya Zima moto mwaka 2024 Kwa mfano, je muda wa kikatiba wa kiuchaguzi utawatosha kuwashirikisha wananchi?
 
Mkuu, umesema maneno machache lakini ni maneno mazito sana.

Ni kwanini wadhani Upinzani nchini hawana mpango wowote wa kushinda chaguzi za 2024 na 2025?

Karibu sana mkuu, fafanua.
Yes, afafanue.

Tangu UHURU hajatokea Bado mtu starategic, forward looking leader aina ya Mbowe Kwa vyama vya upinzani.

Sijawahi mpuuza MWAMBA.
 
Mara nyingi vurugu hutegemea na hali halisi ya jamii kiuchumi na kiakili huwezi fahamu kama wale wafanyao vurugu uwezo wao kiakili umekaaje ukaja kujutia uamuzi wa kuleta vurugu.

Nchi ilipo saa hii ina shida kubwa ila twasema kwa kiingereza ipo "contained within" yaani wananchi wameamua kunyamaza. Sasa ukija na kuhamasisha vurugu utaleta hali ya zaidi ya yale yalotokea Kimbari.

Sasa hivi tuna Panyaroad na vijana wengi wasajiriwa hili ni jeshi tayari sasa upo tayari kuona ndugu zako na familia yako zinapata taabu?

Sisi wenye kujadili kwa makini hatutaki hali hiyo itokee hata kidogo.

Majadiliano au "Dialogue" bado ndo njia sahihi ya jamii ilostaarabika hadi kitapoeleweka. Cha msingi ni masuala yepi Chadema wayaweka mezani kwenye majadiliano na huyafuatilia kwa kiasi gani.

Hata uamuzi wa kususia chaguzi si sahihi kwani pia huwanyima wapiga kura wa Chdema haki yao ya msingi ya kupiga kura.
 
Wananchi waliokaa kimya ni Hatari kuliko wanaoongea.

Kuna wimbi kubwa la wananchi wanaotoa uhai wao na familia zao Kwa kukata tamaa ya maisha.

Lipo pia kundi kubwa la vijana wanaoasi maadili na kurudi kuwaumiza raia kama panya road n.k

Jana mbunge mmoja ameripoti diwani wa CCM na Mbunge Dodoma kuporwa Mali zao na makundi haya.

Watawala wakiipuuza KATIBA mpya wakaruhusu madai Kwa njia ya maandamano, HOFU kubwa ni makundi ya vijana wahalifu wakiungana na vyama pinzani dhidi ya Serikali matokeo yake ni mabaya sana.

Watawala wajiulize, ikiwa mwananchi amediriki kujikata Koo mwenyewe, au kuua familia na baadae kujimaliza mwenyewe, ataogopa Virungu na mabomu au risasi za POLISI wachache?

Zama zimebadilika CCM Ione mbali na mbele sana kuliko wananchi na vyama vya siasa.

Ameeeeen.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…