Mjadala: Upinzani utaanzaje kujipanga kwa uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2024 na hatimae uchaguzi mkuu wa uraisi wa 2025 ndani ya mazingira magumu?

Get prepared, bt usisahau KANU kiliangushwa na majabali yaliyotoka ndani ya chama kuungana na wapinzani .

CDM ikinyamaza, tegemea uasi Kutoka ndani ya chama tawala, lazima watagombana kugombea madaraka.

Bora kusubiri huo uasi ndani ya ccm, lakini kwa mwenendo huu wa chaguzi ambazo rais na genge lake wanaamua nani atangazwe mshindi, kisha watu kuachwa na vilema vya maisha, halafu viongozi wanaenda kwenye maridhiano sijui muafaka ni upuuzi tu.
 
Vyombo vya dola hufanya vitendo vya kikatili kutokana na hali yao kiuchumi kuwa mbaya kwao , au tu ni roho mbaya na ukatili, je, ni elimu duni juu ya sheria au tu ni kufuata amri kutoka juu?

Kwa katiba hii ambayo viongozi wa vyombo vya dola wanapewa vyeo kama hisani na rais, usitegemee vyombo vya dola kufanya kazi kwa mujibu wa sheria, zaidi ya utashi wa rais na genge lake. Tuliona jinsi Magufuli alitumia waziwazi vyombo vya dola kufanya mambo yaliyo nje ya sheria.
 
Ahsante sana nimekuelewa.

Hata hivyo maana sahihi ya maridhiano ni kuweka mawazo au imani ya pande mbili yawe sawa yaani kuwiana.

Lakini Chadema lazima itambue kuwa CCM inanunua muda hadi 2024 na 2025 hiyo ipo wazi.

Hapo ndipo unapokuja na mikakati ya namna ya kujiandaa maana umeshatambua azma ya mtesi wako.

Pili, hiyo ya kupanga RASIMU ya Warioba irudishwe mezani nalo pia CCM yanunua muda.

Sasa ni mwisho wa September na mwakani ni 2023 na chaguzi ni 2024 kisha 2025.

Upo sawa.

Hapo ndipo nnapokuja na nyenzo namba 4 iitwayo kuunganisha yaani "Connect" ambayo itafanywa na Chadema digital katika mtandao wake.

Hii nyenzo au "tool" itasaidia sana kati ya sasa na ifikapo wakati wa uchaguzi wa 2024 na ule wa 2025.

Lakini "CHADEMA UNGANISHA" yafanyaje kazi?

Kwa kuwa njia hii yaingia zaidi kimkakati sitaweza kuijadili sana hadi hapo ntaporidhika na maoni ya wapinzani wenyewe kwani kweli Chadema ikitumia njia hii basi CCM itapata taabu sana.
 

Kwa taarifa yako vyama aina ya CCM huwa havijali majadiliano, bali huogopa tu nguvu ya umma. Hayo majadiliano yanaendelea sasa ni furahisha genge. Kama watu wataendelea kukaa kwenye meza ya maridhiano, tegemea viongozi kupewa ulaji huku madai yako yakipuuzwa. Nikusaidie kitu, wananchi hawajaamua kukaa kimya, bali uoga ndio umewaingia.

Hilo la kususia uchaguzi ni jambo sahihi, maana kwenda kila siku kwenye box la kura, kisha mabox ya kura kuletwa kwa uratibu wa vyombo vya dola, mbele ya wasimamizi wa uchaguzi, utakuwa una matatizo ya kiakili kama utaendelea kushiriki uchaguzi wa aina hiyo. Inshort hakuna uchaguzi wa CDM na wafuasi wake wa kwenda zaidi ya kupotezeana muda. Bado nasisitiza, machafuko au nchi kupinduliwa ndio yatarejesha heshima ya box la kura.
 

Kama una mbinu iweke hapa au wapelekee CDM huko ofisini kwao. Lakini ninavyoona sioni kama utakuwa na mbinu yoyote yenye nguvu, na ifanye kazi zaidi ya machafuko. Njia za kistaarabu zimeproove failure katika kupambana na CCM. Ifahamike CCM haitumii njia za kistaarabu kubaki madarakani, itakuwa ni kosa la wazi kutegemea njia za kistaarabu wakati wenzako wanatumia uhuni kubaki madarakani.
 
Huu ujinga unao itwa maridhiano baina ya mwenye madaraka na wasio nayo, una zalisha aina ya utawala kama uliopo Zanzibar Rais [ CCM ] , makamu wa Rais wa kwanza & wa pili [ ACT + CCM ] hapa pote bado mamlaka yapo kwa CCM . Labda kama Chadema wanataka kuwa tawi la CCM-B

Njia ya maridhiano haiwezi kuleta matokeo chanya kama bado CCM ana madaraka zaidi tu yataifanya Chadema kuwa tawi la CCM.
 
Katiba ya warioba ilisema mawaziri hawatokani na wabunge, ma DC sijui RC kufutwa meaning huhitaji wanasiasa wengi kuongoza nchi Una source tu professionals unaoona Wana uwezo wa kuongoza kama tu alivyofanya JPM kwa kina Mpango, Kabudi n.k ndio haswa katiba mpya ilitaka.

Kingine CHADEMA Ina watu wengi sana na Sio wote mpaka wawe wabunge ndio uwajue, binafsi nafahamu Wana CHADEMA wapo serikalini, mashirika ya kimataifa kama World Bank wengine ma doctor UD pale so usidhani kina Lema ndio cream utakua unaona kichuguu tu wakati kuna mlima wa Viongozi kibao wametapakaa ila sheria tu zinawabana kuwa active majukwaani ila siku CCM ikidondoka utawaona wazi wazi.

Mfano hii kata nayoishi anayedhamini vikao vya CHADEMA na mambo ya CHADEMA digital ni kigogo mmoja mstaafu wa JWTZ, so unaweza ona network za chama zilivyopenya hadi jeshini.
 
Mkuu nadhani Iko wazi Mbowe alitaka siasa za amsha amsha ila umeona kesi ya ugaidi na Ile ilikua message kwamba tukichagua njia hiyo basi tutegemee watu wafungwe, kunyongwa, mitutu ya risasi n.k so Mbowe hakua na choice kwakweli ni sawa tu na Mandela alipokua gerezani.

2. Maridhiano nadhani ni nia ya kuingia Dili kwamba tutakuacha ufanye mipango Yako bila bughudha sisi utupe katiba mpya na time huru Ili 2025 wananchi waamue!!! Mama akakubali hayo madai ya katiba sasa time frame ni mpaka 2023 wakiona hakuna progress obvious watajitoa kwenye hiyo arrangement.

Nadhani sio jambo baya kama mtu kakubali "myamalize" mezani why mparuane barabarani, Mnyika aliomba tuwe watulivu mpaka mwisho wa vikao then ndio tuone mulekeo na mafanikio
 
Yes, afafanue.

Tangu UHURU hajatokea Bado mtu starategic, forward looking LEADERS aina ya Mbowe Kwa vyama vya upinzani.

Sijawahi mpuuza MWAMBA.
Mbowe wa maridhiano?😆.Mara 100% Tundu Antipas Lissu kuliko mbowe wa maridhiano upinzani/chadema kuchukua nchi kutoka kwa CCM ina wahitaji wanasiasa wenye kaliba za Lissu kuwatoa CCM madarakani na sio viongozi aina ya mbowe ana fanya siasa alizo fanya Mwalimu 1950s wakati ana dai Uhuru toka kwa Muingereza ana sahau kuwa mkoloni wa sasa karne hii ya 21 ni mweusi [ CCM ] asiye amini katika njia anayo amini mbowe.

Njia pekee itayo waondoa CCM madarakani ni revolution [ millitary revolution/ mass revolution ] na wala sio upumbavu unao itwa sanduku la kura wala ushenzi wa maridhiano.
 

Sipingi usemacho, lakini sikioni kwenye utekelezaji. Ngoja nitulie, lakini najua ni kupotezeana muda.
 
Mkuu, umesema maneno machache lakini ni maneno mazito sana.

Ni kwanini wadhani Upinzani nchini hawana mpango wowote wa kushinda chaguzi za 2024 na 2025?

Karibu sana mkuu, fafanua.
Kwa sababu moja kuu , ni kwamba vyama vyote vya upinzani vinahitaji kufanyiwa “polical reform” mpya kifalsafa na kimuundo wa vyama . ili kuweza kupambana na CCM na kumyang'anya madaraka njia wanazo tumia sasa hivi kupambana na CCM ni za kijinga sana zina wafanya wacheze vizuri ngoma zinazo pigwa na CCM huku wenyewe wakiwa hawajui ni kwa namna gani njia zao zina wanufahisha CCM mfano wa ujinga mmoja ni hii taka taka inayo itwa maridhiano.
 
Ndugu ingekuwa Rahisi mama kutimiza Masharti ya CDM ikiwa tu Hana Nia ya kugombea 2025.

Ingekuwa mapema tu baada ya kuanza vikao angefuta Lili zuio Batili.

Bado Pana utata sana ktk jambo Hilo.
 
Ndugu ingekuwa Rahisi mama kutimiza Masharti ya CDM ikiwa tu Hana Nia ya kugombea 2025.

Ingekuwa mapema tu baada ya kuanza vikao angefuta Lili zuio Batili.

Bado Pana utata sana ktk jambo Hilo.
Mkuu hii mbinu alitumia Tshisekedi na alipopata upenyo tu wote mnajua alivyokigeuka chama tawala kilichopita, so ikifanikiwa huwa ni mbinu nzuri ya kumaliza adui Yako kimya kimya.

2. Kuhusu incumbency ya Samia, kwa maoni yangu dili lilivyokaa ni kwamba Samia ataendelea 2025 ila obviously kwingine kote wananchi waamue, which is a win kwa upinzani maana wameingia kwenye meza ya mazungumzo wakiwa hawana hata madiwani 10 nchi nzima so kupata wabunge hata 120+ na halmashauri za kumwaga kama 2015 hivi ni mafanikio makubwa kuelekea kuifuta CCM 2030.

Kitila Mkumbo amesema chance ni hii tu, akiingia Rais mwingine tusahau katiba mpya Wala tume huru na CCM itatawala milele. So ni bora ujifanye mjinga katiba ipatikane afu mnyooshane baadae maana hatokua na la kufanya tena.
 
Hizo hesabu ni ngumu kuliko Function, matrix, log,nk.

CCM Kwa HILA, akitoka shetani, wanafuatia.!!!!
 
Mimi nashauri hivi lile jopo zima la tume ya uchaguzi Nchini Kenya [emoji1139] likiongozwa na Chebukati na mahakama ya Kenya lije Lisimamie uchaguzi wa Tanzania 2024-2025....la sivyo Hii nchi yetu[emoji1241] ina waoga,wajinga,wahujumu uchumi,walamba Asali wengi mnooo....watakao fanya juu chini hata kushirikiana na mabeberu kuendelea kusalia Uongozini....ikishindikana hivi itabidi mtutu wa bunduki utumike[emoji3] kusambaratisha genge la wanyonyaji...
 
Ukisema kama nina mbinu niwapelekee huko ofisini kwao unakuwa hutumii njia sahihi ya kufikiri kwa undani kwani waonyesha kukata tamaa lakini amini nakuambia hiki tukiongeacho hapa kina maana kubwa sana.

Bado naamini machafuko si njia sahihi bali njia za kawaida tu zatosha. Lakini kwanza tuna budi kuangalia hali ya kiuchumi ya upinzani je, wana hali gani kifedha? Shughuli za uendeshaji wa chama wahitaji fedha na mipango, je Chadema ina vyanzo imara vya fedha ambavyo huko mbele vitaweza kuwa mbadala wa ruzuku kutoka serikalini?

Fedha nyingi huelekezwa katika maeneo kama ya kidijitali na huko ndiko kwenye kukiimarisha chama lakini je ni kwa mtindo upi?

Ok, tuseme Chadema yaanza na uchaguzi wa serikali za mitaa hii ndo njia sahihi ya kujenga "base" ya viongozi wengi ambayo itasaidia kupatikana wabunge wengi kwa mtindo mmoja tu.

Sasa basi, wewe wataka kuwa diwani wa kata fulani lakini si mhuni, umesoma uzuri hadi chuo kikuu na ni lazima ushinde katika kata yako. Hivyo Chadema digital itaandaa "profile" ya mgombea, vipeperushi vinavyomuongelea mgombea na mwisho sera zake zote anoziuza kwa wapiga kura. Hali ni hiyohiyo kwa wagombea ubunge na hiyo si tu bila mkutano wa halaiki bali vipeperushi vyenye ujumbe tosha kwa mpiga kura.

Hizi ni hatua ambazo zapaswa kutekelezwa mwanzoni katika ya upigaji kura ya maoni na namna ya kuufikisha ujumbe kwa wananchi kulinganisha sera au ilani ya CCM na ile ya kwenu, wapi CCM wameshindwa na ninyi au mgombea wenu atafanya nini tofauti.

Hii hatua ya Chadema UNGANISHA au "connect" ni hatua ambayo ikifika kwa walengwa mgombea anakuwa hana shida ya kujitambulisha maana tayari ajulikana kabla hata ya siku ya mkutano wa kampeni.

Mambo yaliyomo katika hii "Connect" au UNGANISHA ni pamoja na uchapaji, utumaji na uwasilishaji wa ujumbe ama kumtambulisha mgombea au kuweka msisitizo wa siku ya kupiga kura.

Hivyo katika eneo husika la kugombea udiwani au ubunge kipeperushi maalum kinachomhusu mgombea kwamba yeye ninani, na ana sera zipi na taarifa zingine atapewa mpiga kura ili achambue.

Asikwambie mtu, hakuna siri kubwa ya kupiga kura kama utumiaji wa sanduku la kura hivyo kwenye hili mbinu kadha wa kadha huitajika ili kuhakikisha wingi wa kura unaleta hofu kuu kwa watawala na DS yao.

Mbinu ingine ni ile ya mvuto na kusajili wanachama katika kila kata kwa kutumia mfumo wa kidijitali na sio kukusanya panyaroad mitaani na wahuni wengi ambao wataviuruga mrindimo wa kisiasa. Hivyo Chadema Digital yapaswa kuweka platform ndani ya tovuti yake ambayo itasajili wanachama wapya kwa kutumia Chadema Digital App ili kusajili vijana au kuwatambua na kuwafanyia uhakiki wale "grassroots" wote ambao ndo nguzo muhimu ya uimarishaji na uhamasishaji.

Eneo hili la Chadema Digital CDM hawajalitendea haki kwani bado tovuti yao imejazwa mipicha tuu kila kona badala ya mambo mengine muhimu sana katika ulimwengu wa mitandao.

Sasa nimalize kwa kusema zipo njia nyingi zaidi ambazo hata wewe bado huzifahamu na labda mwenyekiti Mbowe atanielewa, kuna "Doorstep App", kuna "contact creator" nyakati za kampeni na pia kuna "Word Press Network". Hizi ni zile za kuingia ndani zaidi kumpata na kumshinda mtesi wako.

Tuendelee ntazungumzia kiaina maana hizi ni mbinu na huwezi kuweka mbinu hadharani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…