Mjadala: Upinzani utaanzaje kujipanga kwa uchaguzi wa serikali za mitaa wa 2024 na hatimae uchaguzi mkuu wa uraisi wa 2025 ndani ya mazingira magumu?

Nashauri Mr Mbowe aongeze umakini Kwa suala la maridhiano.

Timeframe ni muhimu, ninanusa harufu ya HADAA mahali!!!!
Huyu jamaa yuko makini kwani anasubiria kikosi kazi kimalize kazi na hayo maridhiano wasipopata mwafaka watalianzisha ndani na yule Lisu atalianzishia Airport kwani uwanja utakuwa wao.
Ndo maana watu wanalazimisha arudi sasa ili joto lisiwe Kali wakati Mwamba anajua anachokifanya ili mwisho uwe mzuri kwao ila sisi tutabaki tunasema tungejua na hiyo tungejua mandamano yatakuwa yameshaenea nchi nzima.
Mwanaccm mm nakuwaga muwazi kuendana na mazingira yalivyo
 
Wewe wachangamsha baraza sio?
 

Richard naona umetawaliwa na nadharia, uhalisia ni huu, kwanza CDM kwa sasa haina fedha nyingi ya kuendesha shughuli zake, labda za watu wakujitolea, ambao nao wameingia woga kwani wanaweza kukomolewa na dola, na haya tumeona kwa wengi waliosupport upinzani.

Fahamu kuwa kwa sasa wafuasi wengi wa upinzani na wananchi wengi wamelipuuza box la kura. Hivyo usitegemee wapiga kura hasa wa upinzani kujitokeza tena kwa wingi, labda Lisu arudi apandishe hamasa. Kile kitendo cha wafuasi wa upinzani kuwapigia kura, na kulinda kura za wagombea wao, kisha wakaondoka kwenda kuunga juhudi, na hawa akina Mbowe kwenda kwenye maridhiano sasa, wafuasi wengi wa upinzani wamekosa imani sana na mwenendo huo. Huu ushauri wako unaosema sioni kama utakuwa na maana au nguvu yoyote kwa watu waliopuuza box la kura, machafuko tu ndio njia ya ukweli kwenye hali hii.
 
Nadharia ni hatua mojawapo ya kufikia lengo lako, hata ukiataka kuendesha gari si utapitia kwanza nadharia au ukisoma kemia si kuna nadharia kwanza na kisha vitendo?

Hivyo weye chukulia hii ni nadharia na ikipenya na kungia kwenye fikra utafahamu nini namaanisha.

Nadharia zipo nyingi tu hii tunoiongelea hapa ni nadharia ya mabadiliko au "theory of change" kwamba yaelezea kuhusu njia fulani ya kipekee ambayo ikitumika italeta matokeo chanya na yenye ufanisi.

Angalia mfano wa dhana ya mabadiliko alotengeneza jamaa aitwa Align yaitwa Align Theory of Change.



Hapo kwa harakaharaka ni kwamba hali ya sasa yaani "current condition" ni kwamba si nzuri kiuchumi na pia kuna mambo mengi yasofaa kabisa kinyume na matarajio ya wapiga kura.

Pili, stratejia ni kwamba tupo kwenye hatua ya kutengeneza mijadala na hii mada ni mojawapo na stratejia hizo.

Tukimaliza hii twaingia kwenye kuchukua hatua yaani "Action" na kufuatia kuangalia matokeo yaani Impact ya hatua zilochukuliwa.

Tukipita hapo yaani 2024 na 2025 tunakuwa na Vision yaani maono sahihi na twaendelea na kazi.
 
Katiba yetu ya mwaka 1977 inaweka wazi utaratibu wa mikutano ya hadhra kwa sasa mazingira yaliyopo hayana tofauti na ya yale ya mwaka 2010 na mwaka 2015 , Upinzani uache uwoga ujenge hoja na agenda inayokidhi matarajio ya wananchi waendeshe mikutano ya Hadhra katika mazingira hayahaya ya sasa , haki haiombwi haki inatafutwa kwa nguvu , tunahitaji viongozi wa upinzani wenye kukaa frontline kama ilivypkuwa miaka ya nyuma ya 2005- 2015,mobilization ya wananchi kuhusu elimu ya demokrasia , na mamlaka waliyonayo kikatiba nk.
 
Nasisi tumezidi kunamuda tuisaidie chadema Mana Kama chama kimetusemea vyakutosha

tuendelee kuwaombea kwenye kipindi hiki champito na mipango yao inayoiua ccm taratibu kwa uhakika
 
Mkuu, nashukuru sana kwa kunielewa.

Katiba ni kweli huenda yaweka wazi utaratibu wa mikutano ya hadhara.

Lakini usisahau sheria ya vyama vingi je nayo yaweka wazi suala la mikutano ya hadhara?

Kwa mfano mikutano mikuu ya kila mwaka huweza kufanywa mara moja au mbili kulingana na katiba za vyama, jer sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 yasemaje juu ya hilo?

Lakini juzi CC ya CCM imekutana na je imetumia sheria ipi ya mikutano ya ndani au wiki mbili zilopita makamu mwenyekiti wake Kinana amezunguka kanda ya ziwa na pia waziri wa fedha kaonekana Singida akihutubia umati.

Hapo ndipo haya yanpoitwa maridhinao yanapotakiwa kuainisha masuala haya.

Sasa je, ni kifungu gani ndani ya katiba ya JMT chatoa fursa kwa chama cha upinzani kufanya mikutano ya hadhara?
 

Muda wa nadharia umeisha, kwa sasa CCM inategemea kukaa madarakani kwa shuruti kupitia vyombo vya dola, hizo njia za kushindana kwa sera tuwaachie Wakenya ambao tayari walishapita hatua ya machafuko, na sasa wako hatua ya demokrasia ya kweli ambapo sera ndio zinapigiwa kura.

Hapa kwetu tuko kwenye hatua ya tume kuchaguliwa na kupokea maagizo kutoka kwa mwenyekiti wa CCM, wapinzani wanaenguliwa kihuni, usalama wa taifa ndio wanakuwa na fomu fake za matokeo, mawakala wa upinzani wanazuiwa kuingia kwenye vituo vya kupigia kura. Hizo njia unazopendekeza zimeshatumika sana imegeuka ni kupotezeana muda. Machafuko tu ndio iliyobaki. Kama bado watu wanaogopa kufanya machafuko ni bora kuachana na kwenda kusimama kwenye box la kura kupoteza muda.
 
Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 namba 05 inaweka wazi utaratibu wa kuendesha mikutano ya hadhra , upinzani uache uwoga ,haki haiombwi inatafutwa kwa nguvu .......
 
Sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992 namba 05 inaweka wazi utaratibu wa kuendesha mikutano ya hadhra , upinzani uache uwoga ,haki haiombwi inatafutwa kwa nguvu .......
Na sheria hiyo pia ilifanyiwa mabadiliko mwaka 2019.

Je, ni haya mabadiliko ya sheria hii ambayo ndiyo yanozuia vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa?
 

Hiyo ni Kweli, Kuna miaka zaidi ya Saba imepita bila ELIMU ya URAIA kutolewa Kwa wananchi.

Vijana kuanzia miaka ishirini kurudi chini hawajui chochote kuhusu HAKI ya Kuchagua na kuchaguliwa kama msingi mkuu mojawapo wa Maendeleo.

ELIMU ya URAIA ni HAKI, ipiganiwe. Ameeen
 
Huu ndio ukweli ambao watu wanaogopa kuuzungumza. Bila mapinduzi hakuna mabadiliko. Wananchi tutakapoona tumeshindwa kuhimili mikodi ndio mabadiliko yatakapotokea, kutegemea vyama vya siasa na chaguzi ni kujidanganya.
 
Lema ameshauri CDM ijiondoe kwenye maridhiano, Ili turudi KUHESABIWA.

Naunga mkono HOJA.

Maana wakati maridhiano yakiendelea, wanaendelea kuumiza raia. Wanazidi kuzuia mikutano Eti tusubiri upuzi wa mukdala!!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…