Mjadala wa elimu: Watoto wa viongozi wanasoma shule hizi za umma?

Mjadala wa elimu: Watoto wa viongozi wanasoma shule hizi za umma?

Joined
Oct 13, 2018
Posts
35
Reaction score
260
Na Thadei Ole Mushi.

Wiki Moja iliyopita kupitia Ukurasa mtandao wa kijamii Facebook ITV iliripoti kuwa huko Geita kwenye shule ya Sekondari Magema ina walimu wawili tu. Habari hii haikupewa kipaumbele Sana kwa kuwa Tanzania tupo selective kwenye habari. Tunapenda Sana Scandal kuliko mambo yanayotuhusu na maendeleo yetu.

Shule hii ilinifanya kutafakari Sana je kwenye shule kama hii Diwani anaweza kupeleka hapo mtoto wake kusoma? Je Mbunge atampeleka? Je waziri atathubutu kufanya risk ya namna hiyo katika maisha ya mtoto wake?.

Kiuhalisia sio shule Moja tu yenye tatizo hilo LA walimu kama Sekondari ya Magema. Zipo shule nyingi mno na tatizo la walimu nchini ni kubwa na kinachofanyika huko Shuleni ni Bora liende.

Viongozi na wenye Fedha watoto wao wapo Kaizaregi, Feza, St Marium nk.

Mwaka 2017/2018 iliyokuwa kamati ya Bunge ilibainisha kuwa kwa mwaka mmoja tu walimu 7,000 hustaafu na kwa mujibu wa data ilikuwa inaonyesha kwa kipindi Cha Miaka 30 wangelistaafu walimu 30,000.

Mwaka 2014/2015 alipokuwa anasoma budget ya Wizara yake Dr Shukuru Kawambwa aliliambia Bunge kuwa Taifa lilikuwa likikabiliwa na upungufu wa walimu 30,945 wa shule za msingi pekee. Upungufu huu ulikuwa kabla ya kutumbuliwa wa vyeti fake na kabla ya utekelezaji wa Elimu bure ambapo sera hii imeongeza maradufu wanafunzi kwenye shule zetu hivyo na upungufu wa walimu kuongezeka.

Mwaka 2017 Ripoti ya Haki Elimu ulitoa utafiti ukiozungumzia changamoto za Elimu Tanzania. Wakati utafiti ule unatoka 2017 ulionyesha kuwa mwalimu mmoja alikuwa akihudumia wanafunzi 164 badala ya 45 kitaalamu (1:164 badala ya 1:45) yaani Mara tatu zaidi ya uhalisia.

Kwa Kutumia tu utafiti huo 2017 utaona kuwa mwaka 2017 tulihitaji tuongeze walimu kwenye shule zetu mara Mbili ya idadi iliyokuwepo ili kukidhi matakwa ya kitaalamu katika utoaji wa Elimu kimataifa.

Kwa kutumia Data za mwaka 2018 toka katika jarida la Trading economics world Bank ilisema Tanzania ina idadi ya waalimu wa shule za msingi 199,705 huku wa Sekondari wakiwa 102,982 Jumla ya waalimu wote Sekondari na Msingi watakuwa 302,687.

Tanzania Kuna wanafunzi wa shule za msingi 11,051,537 milioni Kumi na Moja hamsini na Moja elfu Mia tano na thelathini na Saba.

Wanafunzi wa Sekondari kwa kutumia Data za 2018 toka kwenye jarida Hilo Hilo la Trading economics World bank iliripoti kuwa Tanzania Kuna wanafunzi 2,140,442 milioni mbili laki moja na arobaini elfu Mia nne na arobaini na mbili.

Ukijumlisha wanafunzi wote msingi na Sekondari nchini unapata jumla ya wanafunzi 13,191,979. Wanafunzi hawa kwa ratio ya 1:45 wanahitaji jumla ya walimu 293,155. Huu ni mchanganuo wa 2018.

MATOKEO.

Hakuna Shortcut kwenye Elimu. Unachokipanda ndicho utakachovuna. Tafiti na takwimu zinatuambia kuwa:-

Mwaka 2012 wanafunzi 5,200 walioingia kidato cha kwanza walipimwa wakashindwa kusoma kabisa. Kwa agizo la aliyekuwa naibu waziri wa elimu Philipo Mulugho alisema warudishwe nyumbani.

Ripoti ya utafiti ya Uwezo 2010 ilikuja na matokeo kuwa kati ya wahitimu 5 wa darasa la saba Mmoja wao alikuwa hajui kusoma kabisa sentensi Rahisi ya darasa la kwanza. Katika ripoti hiyo ilionyesha asilimia 42 tu ya wahitimu hao ndio waliokuwa wanaweza kusoma kwa ufasaha.

Mwaka 2014 taasisi ya uwezo ilikuja na ripoti nyinginine na kuonyesha kuwa Watoto wanaotokea familia Maskini kati ya asilimia 100 ya waliokuwepo kwenye utafiti ni asilimia 40 tu walioweza kumidu Stadi za KKK. Kwenye ripoti hiyo Uwezo wanaonyesha kuwa watoto wanaotokea familia tajiri wanauwezo mkubwa zaidi wa kumudu stadi za KKK kwani katika asilimia 100 wao asilimia 60 wanamudu stadi hizo.

Mama SAMIA kaagiza kifanyike Replacement ya walimu 6,000 kwanza lakini huko Mashuleni hali ni mbaya Sana Ratio ndio hiyo kwa mujibu wa tafiti 1:164. Mhadhiri mmoja wa Chuo kikuu kule Africa Kusini aliwahi kusema ukitaka kuliharibu Taifa usiwalipue kwa mabomu wewe haribu tu Elimu yao.

Ole Mushi
0712702602

FB_IMG_1618422989479.jpg
 
Back
Top Bottom