Mjadala wa katiba mpya ITV; Mnyika, Tambwe Hizza na Dr. Mvungi

Mjadala wa katiba mpya ITV; Mnyika, Tambwe Hizza na Dr. Mvungi

Katiba mpya inapaswa kuweka kifungu cha haki ya kuwachapa viboko waropokaji kama Makamba na Tambwe Hiza:frusty:
 

WATANZANIA sasa ni dhahiri kipaumbele cha CCM ni MALIPO YA DOWANA jinsi CC ya CCM ilivyokwishatoa baraka ya malipo tangu jana.

Katika tamko lao pia walidhihirishia taifa UDINI NI SERA YAO RASMI kutugawa Watanzania ili tunapogombana wao wawe wanalipana kodi zetu. Hakuna mahala CCM ilikemea UDINI kwenye tamko lake iliyoshamiri nchini kwa ufadhili wao hivi sasa, ajabu ya mwaka hiyo!!!

Jana hoiyo hiyo, kiongozi mwandamizi wa CCM Bwn Tambwe Hiza, katamkia taifa bila aibu kwamba Mhe Kikwete ALICHOTUAHIDI MWAKA HUU NI MAONI TU na wala HAKUAHIDI SISI WANANCHI KUANDIKA KATIBA MPYA. Huu ni ghiliba na utani mkubwa usiokubalika hata kidogo.

Cha ajabu zaidi Tambwe Hiza alijiaibisha ajabu kwenye ITV pale alipotafuta 'kufundisha samaki namna ya kuogelea kwenye maji'.

Kwa kudhania ya kwamba anaongea na akina sisi huku uswahilini; Hiza alidiriki kutaka kuingiza Mtaalam wa Sheria anaeheshimika sana nchini, Dr Mvungi, kwa kudai kwamba KATIBA na Sheria ni vitu viwili tofauti visivyotegemeana hata kidogo na kwamba Watanzania CCM inafikiria tunachohitaji ni utunzi wa Sheria tu - jamani hadi lini BUSH-LAWYERS kama huyu mwenzetu watakoma kujitwisha utaalam ambao hawana????

Nielewavyo mimi Katiba ni SHERIA MAMA ambapo sheria zote za nchi hupatikana na kufanyiwa kazi.

Wakati sheria za kawaida hutungwa na wawakilishi wa wananchi kwa maana ya Wabunge kule bungeni Dodoma, Katiba ni sheria mama yenye UPEKEE KATIKA JAMII HUSIKA ambapo utungaji wake ni JUKUMU LA RAIA WOTE katika nchi.

Sasa Ugomvi mkubwa kati ya vyama vya upinzani na Wanaharakati, kwa upande mmoja, dhidi ya CCM ni katika kusema kwamba NI HAKI YA KILA MTANZANIA KUSHIRIKI MOJA KWA MOJA katika kutekeleza wajibu wao kutunga Katiba Mpya.

Lakini wao CCM wakiongozwa na Mafisadi wao wanasema Rais ANATOSHA KUTUTUNGIA TU KATIBA KWA KUSHIRIKIANA NA LOWASA, CHENGE na akina ROSTAM AZIZI kututungia tu katiba hiyo kupitia KIKUNDI CHA MADALALI WAO KWA JINA LA WATAALAM WALIOBOBEA KWENYE SHERIA.

Sasa swali hapa ni kwamba; tangu lini Watanzania tukasikia KIKUNDI CHA Mi-FISI wakatunga sheria murua ya kulinda maslahi ya SWALA jangwani???

UWEZO TUNAO, haki hapewi mtu bali ni kwamba haki hufuatwa na kuchukuliwa. Kazi inaendelea kila kona ya nchi kwa watu tunaojali maslahi ya taifa letu. Hakuna kulala!!!
 
Je, kwa jinsi CCM inavyotofautiana vipaumbele na jamii ya Tanzania kuhusu hoja ya msingi ya raia kutaka kujiandikia Katiba Mpya kwa kupitisha mchakato Bungeni na wala si kwa wale watu wanaoithamini na kuruhusu malipo kwa Dowans, wananchi tutegemee nini kwa hizi kauli za serikali ya Mhe Kikwete zinazobadilika kila dakika?????
 
Nimefuatilia kwa kina kipindi cha KIPIMAJOTO cha ITV kilichokuwa na mjadala kuhusu Katiba mpya.
Pamoja na mambo mengine nimegundua kuwa Tambwe Hizza (mkuu wa kitengo cha propaganda CCM) ni mtu muhimu sana katika kukiua chama chake.

Tambwe ameonesha kile hasa watanzania walikuwa wakihisi (doubt) kuhusu ccm. Awali Watanzania wengi walihisi ccm ni chama cha watu waliokosa hekima, wasio na uvumilivu (people with no political tolerance), wavivu wa kufikiri, wenye ghilba, wenye kupenda nafsi zao kuliko wananchi, wenye upeo mdogo wa kufikiri, waanafiki, na wazandiki.

Kabla ya leo saa 9pm hoja hizo hapo juu zilikuwa dhahania tu kwa wananchi (doubts) lakini, baada ya KIPIMA JOTO doubts zote zimenndoka baada ya Tambwe kudhibitisha kuwa ccm ndivyo walivyo kiuhalisia.

Ameonekana kukosa hekima, kujikanganya na alipoona amezidiwa hoja akawa anaingilia hoja za kina Dr.Mvungi bila utaratibu wala aibu.

Akamtukana Bi.Ussu Mallya eti anadai katiba ya wanawake. Aibu gani hii kwa ccm? Hivi huu si unyanyasaji wa kijinsia kweli? Wanaharakati wanasemaje ktk hili?

Akambishia Dr.Mvungi kuhusu ufafanuzi wa kisheria aliokuwa anautoa, akasahau kwamba ufahamu wa sheria alionao Dr.Mvungi ni zaidi ya mara 100 ya Hizza.

Lakini cha ajabu zaidi akamkosoa rais Kikwete ambaye ndiye mwenyekiti wa chama chake eti kuwa hakuna haja ya katiba mpya kwa sasa. Hakika Hizza ameonesha kile ambacho kipo kwenye mioyo ya wanaCCM wengi kiitwacho unafiki.

Ameivua nguo ccm hadharani na kuanika uozo uliomo ndani ya ccm na namna chama hicho kisivyo na miiko ya uongozi, kwa maana kwamba rais anaweza kuongea hili leo kisha akaja kukosolewa kwa kudhalilishwa na mkuu wa propaganda.

Hizza ameonesha mgando wa mawazo walio nao viongozi wengi wa ccm. He has removed all doubts kuwa ccm ni chama kisichojali wananchi zaidi ya kuchumia tumbo. Kwa kufanya hivyo Hizza amefanya kazi kubwa sana inayostahili kupongezwa na kila mwanamageuzi kwa kuipeleka ccm kaburini. Hongera Tambwe Hizza kwa kuitoa ccm ICU na kuipeleka MOCHWARI. Congratulation brother!!
 
Huyu jamaa anaakili kweli? Wenzake wanatoa hoja zenye maana yeye analeta Ubishi kama yupo kijiweni au mlevi kwenye Bar.. Ndio kusema sisiem hawana makini wakuwaweka kwenye hard talks kama zile??
Anaongea ongea tu, contradictions tuuu.. Jaman CCM kuweni makini kwenye masuala muhimu kama haya, toeni viongoz washabiku hawa!! Mwisho tutasema shame on u CCM.

Src: ITV Kipima Joto
.:frusty::frusty::frusty::frusty::frusty::frusty::frusty:
 
Ndio kichwa cha CCM hicho na hapo unaweza kuona walivyo wa hovyo! CCM hawahitaji watu makini kama mtendaji wao mkuu (katibu mkuu ) ni makamba unategemea nini mkuu?
 
Kama Tambwe ndio huyo! Jamani nipeni ruhusa nimpongeze Makamba! Yeye ni chongo (bora) kati ya vipofu CCM! Kama wamemkubalia Tambwe Hiza awawakilishe na mwenyewe ndio anasoma katiba wakati mdahalo unaendelea kazi kweli kweli CCM wanayo! Imagine Tambwe anam-face sharp mind kama Mnyika na Dr. Mvungi na Mama Usu Mallya! Hata Masako, the moderator anamshangaa Tambwe na wapiga simu hawamwelewi! Jamani CUF walitua mzigo ambao CCM waliona mali! Ama kweli wahenga walisema.. Ganda la mua la jana...Chungu kajionea kivuno! Chairman Mao Tse Tung alisema, mafisadi waache wanenepiane (kama Tambwe) ili siku ya mapinduzi watashindwa kukimbia na itakuwa rahisi kwetu kuwa....
 
Huyu jamaa anaakili kweli? Wenzake wanatoa hoja zenye maana yeye analeta Ubishi kama yupo kijiweni au mlevi kwenye Bar.. Ndio kusema sisiem hawana makini wakuwaweka kwenye hard talks kama zile??
Anaongea ongea tu, contradictions tuuu.. Jaman CCM kuweni makini kwenye masuala muhimu kama haya, toeni viongoz washabiku hawa!! Mwisho tutasema shame on u CCM.

Src: ITV Kipima Joto
.:frusty::frusty::frusty::frusty::frusty::frusty::frusty:
Kama mtendaji mkuu ni Ma-rope usitegemee mtendaji wa chini yake akawa tofauti!!!
 
hilo Sakala...
fuatilia elimu yake ndio utagundua kuwa ni Sakala.

Alirudia mara mbili masomo ya chekechea.
Kafeli mpk Madrasa huyo hakumaliza
 
Mti ukipinda basi kivuli hakiwezi kunyooka.
Kama Mtendaji ni Luteni Yusuph sasa mlitegemea Hizza aweje?
 
Tunakuwa tunakosea kumlaumu Tambwe katika mjadala uliopita muhimu kuhusu Katiba,Lawama ziende kwa CCM,ambao wamekuwa na dharau kwa kila jambo linaowahusu Watanzania.Kwa viongozi wanaojali wasingethubutu kumruhusu Tambwe kwenda kukiwakilisha Chama ktk Mjadala Muhimu kwa mstakhabali wa Taifa.Ikiwa Viongozi wao wa kitaifa hawaoni umuhimu wa kuifahamu Katiba itakuwaje wafuasi wao?Waacheni wajianike,wananchi wanaona na ipo siku watasema basi! Shame on CCM!
 
big up mnyika tuelimishe wananchi huo ni mfano wa vijana wa chama namuona tambwe anadesa kwa mnyika kaegesha tumbo tu na anakaribia kupasuka
nilikuwa nafuatilia kupitia TV AFRICA,CCM kumruhusu mtu kama tambwe kwenye suala nyeti kama hili la katiba ni dalili tosha kuonyesha kwamba wamelidharau/hawana nia ya kweli ya kubadili katiba,lakini watawala lazma watambue TANZANIA ya leo sio ile ya zidumu fikra za mwenyekiti wanachi wakichoshwa na ubabaishaji unaoendelea TZ haitotawalika
 
Huyu jamaa anaakili kweli? Wenzake wanatoa hoja zenye maana yeye analeta Ubishi kama yupo kijiweni au mlevi kwenye Bar.. Ndio kusema sisiem hawana makini wakuwaweka kwenye hard talks kama zile??
Anaongea ongea tu, contradictions tuuu.. Jaman CCM kuweni makini kwenye masuala muhimu kama haya, toeni viongoz washabiku hawa!! Mwisho tutasema shame on u CCM.

Src: ITV Kipima Joto
.:frusty::frusty::frusty::frusty::frusty::frusty::frusty:
yanii sisim kama inawatu wa kiivyo basi kwisha habari yake. JAMAA HAMNAZO KABISAAA ETI PROPAGANDA!
 
Jamani mbona tambwe anaendelea kufutuka tu?? Unene wa aina hiyo siyo kawaida kwa mwanaume mwenye majukumu. Anakula nini huyo mlopokaji??

asikuambie mtu anakula kiti moto na bia, kwa fedha za wizi wa piga debe, imagine CCM wamekaa chini
wakaona mtu ambaye at least ana kaakili ni Tambwe hiza, na umeeona alivyo hovyooooo, je angekuja wa
akina makamba, chili goat, si ndio ungeshangaaaa madudu, taraabu, yaani
 
kama tambwe ndio huyo! Jamani nipeni ruhusa nimpongeze makamba! Yeye ni chongo (bora) kati ya vipofu ccm! Kama wamemkubalia tambwe hiza awawakilishe na mwenyewe ndio anasoma katiba wakati mdahalo unaendelea kazi kweli kweli ccm wanayo! Imagine tambwe anam-face sharp mind kama mnyika na dr. Mvungi na mama usu mallya! Hata masako, the moderator anamshangaa tambwe na wapiga simu hawamwelewi! Jamani cuf walitua mzigo ambao ccm waliona mali! Ama kweli wahenga walisema.. Ganda la mua la jana...chungu kajionea kivuno! Chairman mao tse tung alisema, mafisadi waache wanenepiane (kama tambwe) ili siku ya mapinduzi watashindwa kukimbia na itakuwa rahisi kwetu kuwa....
jamani nilisema kuwa mwenye pumba kati ya makamba na tambwe tambwe ni kiboko! Mmeshuhudia wenyewe!
 
Mbona Tambwe kasema kweli; kwani tume iliyoundwa imeundwa kwa ajili ya kufanya nini? Haijaundwa ili kusimamia mchakato wa kuandika Katiba Mpya! Labda msome tena hotuba ya mwaka mpya ya Rais Kikwete. Tambwe yuko sahihi, ndio maana wengine tumeshangaa kwanini tume ya kukusanya maoni inashangiliwa!

mkuu nachoshangaa CCM ni wajingaaaaaaaaaaaaaa beyond my Imagination, hivi huyu Tambwe ndio wamemuona ana afadhali na ndio
kihiyo hivi, hata he doesn't know what constitution is, huu sasa ni upunguwani na utahira wa akili, huyu ni mwendawazimu au tahira kaaaaahhh
yaani anacheza tu as if yupo na vimada au na mkewe wanapiga zogo, yaani vituko, madudu, brain is different thing.
 
Mbona Tambwe kasema kweli; kwani tume iliyoundwa imeundwa kwa ajili ya kufanya nini? Haijaundwa ili kusimamia mchakato wa kuandika Katiba Mpya! Labda msome tena hotuba ya mwaka mpya ya Rais Kikwete. Tambwe yuko sahihi, ndio maana wengine tumeshangaa kwanini tume ya kukusanya maoni inashangiliwa!

Hotuba ya Rais, kwenye suala la katiba inasema:

Ndiyo maana tukaamua kuanzisha mchakato huu na kwa ajili hiyo,nimeamua kuunda Tume maalum ya Katiba, yaani Constitutional Review Commission. Tume hiyo itakayoongozwa na Mwanasheriaaliyebobea, itakuwa na wajumbe wanaowakilisha makundimbalimbali katika jamii yetu kutoka pande zetu mbili za Muungano.Jukumu la msingi la Tume hiyo litakuwa ni kuongoza na kuratibumchakato utakaowashirikisha wananchi wote bila kubagua, vyamavya siasa, wanasiasa, wafanyabiashara, asasi za kiraia, mashirika yadini, wanataaluma na makundi mbalimbali ya watu wa nchi yetukote nchini, katika kutoa maoni yao juu ya wayatakayo kuhusuKatiba ya nchi yao.Baada ya kukamilisha kukusanya maoni, Tume itatoa mapendekezo yake yatakayofikishwa kwenye vyombo stahiki vya Kikatiba kwakufanyiwa maamuzi.

Then inamalizia kwa kusema:

Baada ya makubaliano kufikiwa, taifa letu litapata Katiba mpya kwa siku itakayoamuliwa ianze kutumika.

Kwa hiyo kuwa na katiba mpya kutagemeana na makubaliano yaliyofikiwa which mean still kuna possibility ya kutokuwa na katiba mpya.
 
Back
Top Bottom