Mjadala wa katiba mpya ITV; Mnyika, Tambwe Hizza na Dr. Mvungi

Mjadala wa katiba mpya ITV; Mnyika, Tambwe Hizza na Dr. Mvungi

Mzee Mwanakijiji ni heri yako uliyeumis maana Tambwe kachafua masikio ya watu, yaani paka masako amekasirika na kumwambia mtu mwenye elimu ya kawaida tu anaweza kuelewa kinachosemwa na watu lakini Tambwe haelewi kitu. Toka mwanzo wa mjadala Watu wanaeleza mapungufu ya katiba lakini tambwe anasema hajasikia mapungufu yakitajwa na anasema ameangalia mdahalo wa UDASA nao pia hakuna mtu aliyetoa mapungufu ya katiba.

Kweli Tambwe Anahitaji darubini kuutazama mlima kilimanjaro!
 
Tambwe amewekwa pale kuvuruga,kwani anapingana hata na m/kiti wake jk.suala la katiba mpya si la ccm wala chadema bali ni la watanzania wote,asidhani kuwa wana-ccm hawataki kuwepo kwa katiba mpya.
 
Nilishasema Tambwe ni mwehu kuliko Makamba, na ninaendelea na nitaendelea kuamini hivyo hadi CCM itakapotoka madarakani.
 
Mropokaji kwelikweli... Sijui hata anazungumzia nini hapa. Naona anajaribu kudefend badala ya kujenga hoja za msingi. Kanenepeana mpaka akili nayo imejaa mafuta

amenichosha ngoja nikalale.

Usiku mwema.
 
Tambwe amemwambia Mvungi,dr. kwamba katiba na sheria ni vitu viwili tofouti. Mpaka hapa nimeelewa kuwa Tambwe ni propaganda kama cheo chake cha ccm wala hana weledi wowote. Kama iyo ndo ccm basi ccm ni adui wa watanzania na ni funza kwa wananchi.
 
CCM hawajajiandaa na mabadiliko ya katiba na wala haiopo kwenye ilani yao ya uchaguzi. Iliyopo inakidhi mahitaji yao. Kwa hiyo msiwalazimishe.

Wanachofanya sasa hivi ni danadana kutoa mpira nje ya uwanja ili dakika 90 ziishe.
 
Nyerere aliwahi kusema hivi : tutaongea nao wakishindwa kutuelewa na kutimiza matakwa wetu basi tutawashitaki kwa Mungu, naye asipowashughulikia hatutawaacha, tutawashitaki kwa shetani.
 
Mbona Tambwe kasema kweli; kwani tume iliyoundwa imeundwa kwa ajili ya kufanya nini? Haijaundwa ili kusimamia mchakato wa kuandika Katiba Mpya! Labda msome tena hotuba ya mwaka mpya ya Rais Kikwete. Tambwe yuko sahihi, ndio maana wengine tumeshangaa kwanini tume ya kukusanya maoni inashangiliwa!
 
Tambwe amemwambia Mvungi,dr. kwamba katiba na sheria ni vitu viwili tofouti. Mpaka hapa nimeelewa kuwa Tambwe ni propaganda kama cheo chake cha ccm wala hana weledi wowote. Kama iyo ndo ccm basi ccm ni adui wa watanzania na ni funza kwa wananchi.

sasa ndg yangu ulitegemea kusikia nini toka kwa huyu kimeo? hana analojua zaidi ya propoganda kama kilivyo cheo chake kwenye kile cha cha kuhifadhi ufisadi na ubahirifu wa mali za uma
 
tambwe namfananisha na wale "Dinosaurs" kama nimepatia spelling! mwili mkubwa akili ndogoo
 
Jaman ccm wameisha . Pamoja na kukaa kupiga kura kumpitisha mwenye hoja nzuri awe mwakilishi ktk kipimajoto,aliyebora ni huyo Tumbo. Je waliobaki wanafananeje? Kumbe ccm kukimbia midahalo ya uchaguzi ilikuwa busara,wangehaibika!
 
nimeumiss.. ushaisha?

Afadhali umeukosa kwa sababu Tambwe alisambaza pumba na upupu ikabidi wengine tuondoke kwenye TV zetu na kuwahi bafuni kuoga haraka haraka tusijepata upele wa kuambukizwa na upupu aliotoa pale.

Halafu eti mtu huyo ni mkuu wa kitengo fulani (PROPAGANDA) cha chama tawala na alikuwa akiwania kuingia bungeni awakilishe jimbo la Temeke!!!!
 
Hivi mlitegemea cha maana kutoka kwa huyu kilaza? Lazima ziwe pumba tu !!!
 
Mbona Tambwe kasema kweli; kwani tume iliyoundwa imeundwa kwa ajili ya kufanya nini? Haijaundwa ili kusimamia mchakato wa kuandika Katiba Mpya! Labda msome tena hotuba ya mwaka mpya ya Rais Kikwete. Tambwe yuko sahihi, ndio maana wengine tumeshangaa kwanini tume ya kukusanya maoni inashangiliwa!
Aliwachezea kwa maneno wakaami mchakato umeanza..kumbe mchakato wenye ni wakukusanya maoni!Kwahiyo yasipojitosheleza katiba mpya hakuna!
 
Tambwe amemwambia Mvungi,dr. kwamba katiba na sheria ni vitu viwili tofouti. Mpaka hapa nimeelewa kuwa Tambwe ni propaganda kama cheo chake cha ccm wala hana weledi wowote. Kama iyo ndo ccm basi ccm ni adui wa watanzania na ni funza kwa wananchi.

Katiba ni SHERIA MAMA ambapo sheria zote za nchi hupatikana na kufanyiwa kazi.

Wakati sheria za kawaida hutungwa na wawakilishi wa wananchi kwa maana ya Wabunge kule bungeni Dodoma, Katiba ni sheria mama yenye UPEKEE KATIKA JAMII HUSIKA ambapo utungaji wake ni JUKUMU LA RAIA WOTE katika nchi.

Sasa Ugomvi mkubwa kati ya vyama vya upinzani na Wanaharakati, kwa upande mmoja, dhidi ya CCM ni katika kusema kwamba NI HAKI YA KILA MTANZANIA KUSHIRIKI MOJA KWA MOJA katika kutekeleza wajibu wao kutunga Katiba Mpya.

Lakini wao CCM wakiongozwa na Mafisadi wao wanasema Rais ANATOSHA KUTUTUNGIA TU KATIBA KWA KUSHIRIKIANA NA LOWASA, CHENGE na akina ROSTAM AZIZI kututungia tu katiba hiyo kupitia KIKUNDI CHA MADALALI WAO KWA JINA LA WATAALAM WALIOBOBEA KWENYE SHERIA.

Sasa swali hapa ni kwamba; tangu lini Watanzania tukasikia KIKUNDI CHA Mi-FISI wakatunga sheria murua ya kulinda maslahi ya SWALA jangwani???

UWEZO TUNAO, haki hapewi mtu bali ni kwamba haki hufuatwa na kuchukuliwa. Kazi inaendelea kila kona ya nchi kwa watu tunaojali maslahi ya taifa letu. Hakuna kulala!!!
 
Tambwe Hiza!!Hao itv wametumia kigezo gani kumualika Mtu wa aina hii au swala la KATIBA wanataka kuligeuza kuwa Propoganda?Ndo kazi ya huyu Bwana cjawahi kumsikia akiongea point hata 1tu katika maisha yangu.

Ndugu yangu hawa ndio aina ya watu waliojikoni kwa ccm, sasa unategemea wangemwita nani makamba? Na yeye sana sana angetoa nukuu za misahafu hana jipya, mbona kazi tunayo.
 
Back
Top Bottom