Mjadala wa katiba mpya ITV; Mnyika, Tambwe Hizza na Dr. Mvungi

Mjadala wa katiba mpya ITV; Mnyika, Tambwe Hizza na Dr. Mvungi

Kwa wasiomjua Tambwe sasa wanaweza kujua ni mtu wa aina gani
 
huyu tambwe ametolewa lini hospitali? nimeona magazeti ya leo kuwa amelazwa,alipotoka tu akaelekea itv!!!?
duh anaongea upupu hadi tumekosa mambo ya maana kutoka kwa watalaam wetu.....
hivi lazima kuikubali mijitu kama hii kuingia kwenye mjadala???
 
Sasa nimegundua kwanini ccm wamemtuma tambwe kwenye huu mjadala. Ameletwa kuja kuvuruga mjadala, amewatoa kwenye mjadala na sasa wanabishana. Mjadala umeharibika kabisa

kaharibu mjadala wote
 
Mheshimiwa JK pole sana unawakati mgumu... hata kukiokoa chama kwa hali hii sijui nani angekiweza... watu wameoza halafu wanahaha kulindana... pole kaka wengi hawaelewi lakini uko kwenye wakati mgumu sana... sidhani kama watu wanaelewa... na mbaya zaidi wengine wamekupania kukumaliza na mengi yanajidhihirisha unakumbuka walipopinga sana swala la katiba kupitiwa? Watu wakajua ni msimamo wako kumbe masikini vijana hawanan nidhamu hata hawasubiri kukuuliza mwenyekiti mtoe msimamo wenu kwa taratibuzenu rasmi wanaanza kuropoka ona sasa umeafiki kupitiwa katiba wanavyohanaika pole saana
 
@#$%#$ tambwe hiza-yaani kaja kuvuruga huu mjadala wote leo-kwanza anamuintercept kila mtu aliekuwa anaongea-akipewa nafasi anazungumza pumba-next time si mtu wa kumwalika huyu-ana umbo kubwa but empty minded.cccm cjui wamempa nini?kaniuzi sana leo
 
Mubarikiwe sana kwa kutuletea kinacho endelea uko... Tambwe amejibu vipi swali la Masako, alilo muuliza kuhuse yeye kupingana na m/kiti wake?
 
Da mdahalo umeisha! Angekuwa si huyu upupu hapa mdahalo ungenoga zaidi... propaganda tupu za huyu jamaa.
 
nimepata shida kipindi kilikuwa cha mabishano zaidi.tambwe anakera jamani.natamani asiwe anasikika katika vipindi muhimu kama hivi.ccm walete mtu makini
 
huyu Tambwe is so harsh na yupo arrogant, anaharibu mjadala.

yaani tambwe ameboa kweli amepotosha kabisa hadi ya mjadala umekuwa kama kijiwe cha kahawa stupid boy itv wasi waruhusu watu kama hawa.stupid boy
 
Mubarikiwe sana kwa kutuletea kinacho endelea uko... Tambwe amejibu vipi swali la Masako, alilo muuliza kuhuse yeye kupingana na m/kiti wake?

Amejibu eti jk kakubali wananchi waseme kama kunahaja ya katiba mpya kwa kuunda tume itakayo ratibu kuona kama mapungufu ni mengi basi iundwe mpya na kama ni kidogo ifanyiwe mabadiliko
 
CCM ina wenyewe na wenye ndio kina Tambwe Hiza. Hivi kama Tambwe Hiza ndio ameonekana ana uwezo wa kupewa madaraka ya umbea katika chama ana uwezo mdogo hivyo hao wengine wana hali gani?
 
Mubarikiwe sana kwa kutuletea kinacho endelea uko... Tambwe amejibu vipi swali la Masako, alilo muuliza kuhuse yeye kupingana na m/kiti wake?

kajibu pumba kasema hajampinga rais bal ni propaganda za vyama'halafu anasema katiba mpya mpaka ya sasa ikionekana haifai kabsa
 
pumba alizo mwaga tambwe hizza sijawai ziona ukimpa nguruwe anazimia kabisa
 
Inawezekana kulikuwa na habari za kiintelligencia kuwa mjadala ungewatoa sana wapinzani kwa hiyo ikabidi atumwe mlopolaji aka mpropaganda
 
Sijui ni kina nani walimuintaview huyu jamaa ukiacha makamba
 
Back
Top Bottom