Nimefuatilia kwa kina kipindi cha KIPIMAJOTO cha ITV kilichokuwa na mjadala kuhusu Katiba mpya.
Pamoja na mambo mengine nimegundua kuwa Tambwe Hizza (mkuu wa kitengo cha propaganda CCM) ni mtu muhimu sana katika kukiua chama chake.
Tambwe ameonesha kile hasa watanzania walikuwa wakihisi (doubt) kuhusu ccm. Awali Watanzania wengi walihisi ccm ni chama cha watu waliokosa hekima, wasio na uvumilivu (people with no political tolerance), wavivu wa kufikiri, wenye ghilba, wenye kupenda nafsi zao kuliko wananchi, wenye upeo mdogo wa kufikiri, waanafiki, na wazandiki.
Kabla ya leo saa 9pm hoja hizo hapo juu zilikuwa dhahania tu kwa wananchi (doubts) lakini, baada ya KIPIMA JOTO doubts zote zimenndoka baada ya Tambwe kudhibitisha kuwa ccm ndivyo walivyo kiuhalisia.
Ameonekana kukosa hekima, kujikanganya na alipoona amezidiwa hoja akawa anaingilia hoja za kina Dr.Mvungi bila utaratibu wala aibu.
Akamtukana Bi.Ussu Mallya eti anadai katiba ya wanawake. Aibu gani hii kwa ccm? Hivi huu si unyanyasaji wa kijinsia kweli? Wanaharakati wanasemaje ktk hili?
Akambishia Dr.Mvungi kuhusu ufafanuzi wa kisheria aliokuwa anautoa, akasahau kwamba ufahamu wa sheria alionao Dr.Mvungi ni zaidi ya mara 100 ya Hizza.
Lakini cha ajabu zaidi akamkosoa rais Kikwete ambaye ndiye mwenyekiti wa chama chake eti kuwa hakuna haja ya katiba mpya kwa sasa. Hakika Hizza ameonesha kile ambacho kipo kwenye mioyo ya wanaCCM wengi kiitwacho unafiki.
Ameivua nguo ccm hadharani na kuanika uozo uliomo ndani ya ccm na namna chama hicho kisivyo na miiko ya uongozi, kwa maana kwamba rais anaweza kuongea hili leo kisha akaja kukosolewa kwa kudhalilishwa na mkuu wa propaganda.
Hizza ameonesha mgando wa mawazo walio nao viongozi wengi wa ccm. He has removed all doubts kuwa ccm ni chama kisichojali wananchi zaidi ya kuchumia tumbo. Kwa kufanya hivyo Hizza amefanya kazi kubwa sana inayostahili kupongezwa na kila mwanamageuzi kwa kuipeleka ccm kaburini. Hongera Tambwe Hizza kwa kuitoa ccm ICU na kuipeleka MOCHWARI. Congratulation brother!!