Mjadala wa katiba mpya ITV; Mnyika, Tambwe Hizza na Dr. Mvungi

Ki mtazamo nilivyomsoma huyu jamaa wa ccm

malipo ya dowans ndio ajenda kubwa kwao ambayo taka tusitake lazima yatafanyika :frusty:

suala la katiba mpya ni ndoto labda kutumia nguvu ya uma kwa mfumo wa sasa ni sawa na danganya toto why jamaaa anadhubutu kusema mimi na wewe hatutaki katiba mpya whu is he to speak on behalf of me

napata pia shaka na uwepo wa noti mpya nchi imeshakua ya kibiashara no one care is like the end justify the means tayari tushapigwa changa la macho. tafakari
 
Wakuu,
Kupitia kipindi cha kipima joto cha ITV kilichorushwa moja kwa moja jana, sasa imekuwa dhahiri kuwa msimamo wa kikwete kuhusu katiba ni tofauti na wengi wetu tunavyofikiria. Bw. Tambwe hiza alifafanua kuwa alichosema kikwete hakimaanishi kwamba katiba mpya ni lazima ipatikane. Kumbe kamati atakayounda kikwete itakuwa na kazi ya kukusanya maoni ya wananchi na kuangalia kama kutakuwa na haja ya kuunda katiba mpya. Kwa maneno mengine nikuwa upo uwezekano kamati isione haja ya kuwa na katiba mpya.

Jamani alichosema tambwe hiza ndiyo msimamo halisi wa kikwete. Kwa wale walioshuhudia majadiliano kwenye ITV watakuwa mashahidi kwamba kuna wakati tambwe hiza alikuwa busy na simu zake mbili akiandika na kusoma sms. Inawezekana wakubwa wa ccm walikuwa wanamtumia maneno ya kufafanua msimamo huo. Watanzania tukae chonjo tusikubali nchi iendeshwe na kikundi cha wachache tu.
 
Cjapata ona kiongoz mpuuz kama tambwe, cjui ana2mia akil gan, ktk mambo muhmu ya kitaifa analeta ubish wa kitoto? Cna haja ya kumjadil zaid, ana upeo mdogo wa kufikir, shame upon ccm.
 


Tumsifu sana Tambwe maana ametoa live kilicho moyoni kwa Makamba na wengine wenye upeo kama wake ambao ndio wengi sana....nawafananisha na wanachana wa klabu moja ambao nao wana mawazo mgando kwa ajili ya maslahi ya wachache kuwa watakula wapi mfumo wa uendeshaji ukibadilishwa na kuwa kampuni....ndio ccm hao wale inner circle ambao wanafaidika kwa fitna na majungu pale ndio wanaojipa moyo na kuendesha usanii na propaganda ila muda utawapita hawa na ukweli chama kitawapasukia...

Tambwe ametoa ambao kipo ndani ya chama chao...hiyo tume ni kupoteza muda na kusogeza time hadi uchaguzi ujao upite wanajua demand itakuwa imepungua sana hawajui joto hili halitashuka kabisa....tumeapata picha kamili ya jk anaogopa bomu kumpasukia...la nchi na chama anapoteza muda amalize muda akae pembeni...
 

huyu jamaa anakunywa zed ..... haa haaaa
 
Cjapata ona kiongoz mpuuz kama tambwe, cjui ana2mia akil gan, ktk mambo muhmu ya kitaifa analeta ubish wa kitoto? Cna haja ya kumjadil zaid, ana upeo mdogo wa kufikir, shame upon ccm.

Tambwe hiza anawakilisha sura halisi ya chama kilichovimbiwa madaraka na chenye mawazo mgando. Pamoja na wewe kumdharau hivyo, chama chake kimemwamini na kuruhusu atamke yale aliyotamka jana. Ni aibu na fedhaha kubwa chama kikongwe kama ccm kuwakilishwa na mchovu wa akili kama tambwe hiza.
 

Chama kikongwe makada wake nao lazima wawe wakongwe, lakini tambwe ameota kutu, nadhani. Kama watoto wake walotazama kile kipindi na watembelea Hapa jamvini wamshauri asikubali tena mialiko ya tv.
 
Asante mwanakijiji kwa ufafanuzi huo. Hata mimi nilishawambia watu na kushangaa watu wanashangilia uundwaji wa tume ya kutafuta maoni?
 
Cjapata ona kiongoz mpuuz kama tambwe, cjui ana2mia akil gan, ktk mambo muhmu ya kitaifa analeta ubish wa kitoto? Cna haja ya kumjadil zaid, ana upeo mdogo wa kufikir, shame upon ccm.

sidhani kama ni sahihi kumwita huyo kilaza kiongozi hiyo level hana, nilishangaa alivyokuwa mweupe upstairs, yaani watu wanashuka vitu vilivyoenda shule halafu yeye anatuletea ze comed,yeye alifikiri wapo pale kushindanisha vyama kumbe wenzie walikuwa ki-nchi zaidi
 
Jamani bado tu mnasubiri TUME iundwe? hivi hamtambui kuwa katiba ya sasa inasema kuwa raisi anao uwezo wa kukubali ama kukataaa maoni ya kamati ambayo yeye raisi ameiunda?
ni maoni mangapi yaliyotolewa na tume mbalimbali zilizoundwa na raisi na hyakukubaliwa na ilifikia wakati wajumbe wa tume walituhumiwa kuwa maoni walio towa ni yao binafsi
Jamani huu sio wakati wa kuisubiri CCM iseme juu ya katiba
Tuwaelimishe wananchi wajue umuhimu wa katiba then
iwe kama kenya tu kwani hiyo ni haki yetu na sio ya kikundi cha watu wachache
VIJANA TUAMUE SASA MAISHA YETU YASIWE CHINI YA WACHACHE HUU NI WAKATI WETU TUAMKE,TUDAI KATIBA KWA NGUVU ZOTE

MAPINDUZIIIII DAIMAAAAAA:kev::A S-fire1:
 

Hao hao wanaosema fidia ya DOWANS ilipwe. Wananchi wanatakiwa wasikubaliwa kuburuzwa na vilaza ama hawa viongozi wa vyama vyenye ubinafsi wa kupindukia.
 
Hakuna anaeweza kuzuia jua kuwaka!!! Watake.... wasitake.... Katiba mpya lazima!!
 
Je Tambwe Hiza ana elimu ya kiwango gani, kweli jana nilishangaa sana, badala ya kusikiliza na kujibu hoja kwa hoja analeta maneno ya kwenye kahawa, ccm vipi jamani, hao ndiyo kati ya washauri wenu?
 
Mbona jamani tunataka kuwa semea wengi? tuache watu wajisemee wenyewe jamani, tusiendeshwe kwa mhemko mtu anasema nchi isiendeshwe na kundi flani la watu wakati huohuo anatuasa vijana tupambane ipatikane katiba mpya we umejuaje mimi naihitaji katiba mpya ama la wakati hata hiyo iliyopo siijui na sijui mapungufu yake? Ndugu zangu labda tujaribu kukumbuka waliyotueleza wanazuoni wetu pale Nkrumah Hall Chuo Kikuu cha Nchi Prof. Issa Shivji, Jenerali Ulimwengu na Azavel Feza Lwaitama kuwa tusiwasemee watu tuwaache waseme wenyewe na ndiyo maana katika kongamano lile walikua wanaangalia mambo makuu matatu 1. Je ipo haja au kuna uhitaji wa katiba mpya? 2. Kama ipo haja au hii iliyopo ibadilishwe, je iwe na maudhui gani? 3. Je mchakato upi utumike kupata katiba hiyo? walisisitiza kuwa haya majibu yote yanapaswa kujibiwa na wananchi na siyo mtu au chama fulani. Tunacho paswa kuangalia je kamati hiyo itatoa majibu kwa nani? itatumia adidu rejea zipi au za mfumo upi? wananchi watapewa uwanja uhuru wa kuelimishwa kabla ya kutoa maoni? Tukisema hoja ipelekwe bungeni tumeshatahadharishwa kuwa idadi ya wabunge wa CCM ni kubwakuliko upinzani hivyo tusishangae ikarudi katiba ya CCM kama Shivji aliyotuelimisha. Sidhani kama tukiandamana nchi nzima ndiyo itakua katiba mpya kama alivyosema mwanasias flani siku ya kongamano kuwa damu ya Arusha ndiyo dibaji Lazima kuwa na organ au chombo kitakacho ratibu swala zima kinaweza kuwa cha rais au bunge na si vinginevyo. Ujue katiba inabadilishwa na katiba na siyo vinginevyo.
 
Aisee wakuu wahenga husemaga ukistaajabu ya Musa utaona ya Firauni na kweli jana nimeona live.Kumbe basi Makamba ana afadhali kuliko Tambwe Hiza yaani yule ni kilaza plus plus na lazima atakuwa na mtindio wa akili.Duh ccm kweli sijaipatia jibu niiweke pande gani na watu wake.
 
Mhe, JK ameamua kutoongea sana safari awamu hii, yeye anaamini sana vikao vikubaliane then anachagua Vuvuzela mojawapo kufikisha ujumbe kwa wananchi (kuwafafanulia wananchi kikao kimeamua nini ) kwa hilo la katiba katumia VUVUZELA Tambwe Hiza , La Dowans jana alitumia VUVUZELA Chiligati , bado tutayaona mengine mengi yakipulizia wananchi maazimia ya vikao vya ccm.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…