jino kwa jino
JF-Expert Member
- Nov 3, 2010
- 794
- 191
Huyo ndio chongo wa ccm
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimefuatilia kwa kina kipindi cha KIPIMAJOTO cha ITV kilichokuwa na mjadala kuhusu Katiba mpya.
Pamoja na mambo mengine nimegundua kuwa Tambwe Hizza (mkuu wa kitengo cha propaganda CCM) ni mtu muhimu sana katika kukiua chama chake.
Tumsifu sana Tambwe maana ametoa live kilicho moyoni kwa Makamba na wengine wenye upeo kama wake ambao ndio wengi sana....nawafananisha na wanachana wa klabu moja ambao nao wana mawazo mgando kwa ajili ya maslahi ya wachache kuwa watakula wapi mfumo wa uendeshaji ukibadilishwa na kuwa kampuni....ndio ccm hao wale inner circle ambao wanafaidika kwa fitna na majungu pale ndio wanaojipa moyo na kuendesha usanii na propaganda ila muda utawapita hawa na ukweli chama kitawapasukia...
Tambwe ametoa ambao kipo ndani ya chama chao...hiyo tume ni kupoteza muda na kusogeza time hadi uchaguzi ujao upite wanajua demand itakuwa imepungua sana hawajui joto hili halitashuka kabisa....tumeapata picha kamili ya jk anaogopa bomu kumpasukia...la nchi na chama anapoteza muda amalize muda akae pembeni...
Tambwe ameonesha kile hasa watanzania walikuwa wakihisi (doubt) kuhusu ccm. Awali Watanzania wengi walihisi ccm ni chama cha watu waliokosa hekima, wasio na uvumilivu (people with no political tolerance), wavivu wa kufikiri, wenye ghilba, wenye kupenda nafsi zao kuliko wananchi, wenye upeo mdogo wa kufikiri, waanafiki, na wazandiki.
Kabla ya leo saa 9pm hoja hizo hapo juu zilikuwa dhahania tu kwa wananchi (doubts) lakini, baada ya KIPIMA JOTO doubts zote zimenndoka baada ya Tambwe kudhibitisha kuwa ccm ndivyo walivyo kiuhalisia.
Ameonekana kukosa hekima, kujikanganya na alipoona amezidiwa hoja akawa anaingilia hoja za kina Dr.Mvungi bila utaratibu wala aibu.
Akamtukana Bi.Ussu Mallya eti anadai katiba ya wanawake. Aibu gani hii kwa ccm? Hivi huu si unyanyasaji wa kijinsia kweli? Wanaharakati wanasemaje ktk hili?
Akambishia Dr.Mvungi kuhusu ufafanuzi wa kisheria aliokuwa anautoa, akasahau kwamba ufahamu wa sheria alionao Dr.Mvungi ni zaidi ya mara 100 ya Hizza.
Lakini cha ajabu zaidi akamkosoa rais Kikwete ambaye ndiye mwenyekiti wa chama chake eti kuwa hakuna haja ya katiba mpya kwa sasa. Hakika Hizza ameonesha kile ambacho kipo kwenye mioyo ya wanaCCM wengi kiitwacho unafiki.
Ameivua nguo ccm hadharani na kuanika uozo uliomo ndani ya ccm na namna chama hicho kisivyo na miiko ya uongozi, kwa maana kwamba rais anaweza kuongea hili leo kisha akaja kukosolewa kwa kudhalilishwa na mkuu wa propaganda.
Hizza ameonesha mgando wa mawazo walio nao viongozi wengi wa ccm. He has removed all doubts kuwa ccm ni chama kisichojali wananchi zaidi ya kuchumia tumbo. Kwa kufanya hivyo Hizza amefanya kazi kubwa sana inayostahili kupongezwa na kila mwanamageuzi kwa kuipeleka ccm kaburini. Hongera Tambwe Hizza kwa kuitoa ccm ICU na kuipeleka MOCHWARI. Congratulation brother!!
Kama Tambwe ndio huyo! Jamani nipeni ruhusa nimpongeze Makamba! Yeye ni chongo (bora) kati ya vipofu CCM! Kama wamemkubalia Tambwe Hiza awawakilishe na mwenyewe ndio anasoma katiba wakati mdahalo unaendelea kazi kweli kweli CCM wanayo! Imagine Tambwe anam-face sharp mind kama Mnyika na Dr. Mvungi na Mama Usu Mallya! Hata Masako, the moderator anamshangaa Tambwe na wapiga simu hawamwelewi! Jamani CUF walitua mzigo ambao CCM waliona mali! Ama kweli wahenga walisema.. Ganda la mua la jana...Chungu kajionea kivuno! Chairman Mao Tse Tung alisema, mafisadi waache wanenepiane (kama Tambwe) ili siku ya mapinduzi watashindwa kukimbia na itakuwa rahisi kwetu kuwa....
Cjapata ona kiongoz mpuuz kama tambwe, cjui ana2mia akil gan, ktk mambo muhmu ya kitaifa analeta ubish wa kitoto? Cna haja ya kumjadil zaid, ana upeo mdogo wa kufikir, shame upon ccm.
Tambwe hiza anawakilisha sura halisi ya chama kilichovimbiwa madaraka na chenye mawazo mgando. Pamoja na wewe kumdharau hivyo, chama chake kimemwamini na kuruhusu atamke yale aliyotamka jana. Ni aibu na fedhaha kubwa chama kikongwe kama ccm kuwakilishwa na mchovu wa akili kama tambwe hiza.
Asante mwanakijiji kwa ufafanuzi huo. Hata mimi nilishawambia watu na kushangaa watu wanashangilia uundwaji wa tume ya kutafuta maoni?Mbona Tambwe kasema kweli; kwani tume iliyoundwa imeundwa kwa ajili ya kufanya nini? Haijaundwa ili kusimamia mchakato wa kuandika Katiba Mpya! Labda msome tena hotuba ya mwaka mpya ya Rais Kikwete. Tambwe yuko sahihi, ndio maana wengine tumeshangaa kwanini tume ya kukusanya maoni inashangiliwa!
Cjapata ona kiongoz mpuuz kama tambwe, cjui ana2mia akil gan, ktk mambo muhmu ya kitaifa analeta ubish wa kitoto? Cna haja ya kumjadil zaid, ana upeo mdogo wa kufikir, shame upon ccm.
sidhani kama ni sahihi kumwita huyo kilaza kiongozi hiyo level hana, nilishangaa alivyokuwa mweupe upstairs, yaani watu wanashuka vitu vilivyoenda shule halafu yeye anatuletea ze comed,yeye alifikiri wapo pale kushindanisha vyama kumbe wenzie walikuwa ki-nchi zaidi
Mhe, JK ameamua kutoongea sana safari awamu hii, yeye anaamini sana vikao vikubaliane then anachagua Vuvuzela mojawapo kufikisha ujumbe kwa wananchi (kuwafafanulia wananchi kikao kimeamua nini ) kwa hilo la katiba katumia VUVUZELA Tambwe Hiza , La Dowans jana alitumia VUVUZELA Chiligati , bado tutayaona mengine mengi yakipulizia wananchi maazimia ya vikao vya ccm.Wakuu,
Kupitia kipindi cha kipima joto cha ITV kilichorushwa moja kwa moja jana, sasa imekuwa dhahiri kuwa msimamo wa kikwete kuhusu katiba ni tofauti na wengi wetu tunavyofikiria. Bw. Tambwe hiza alifafanua kuwa alichosema kikwete hakimaanishi kwamba katiba mpya ni lazima ipatikane. Kumbe kamati atakayounda kikwete itakuwa na kazi ya kukusanya maoni ya wananchi na kuangalia kama kutakuwa na haja ya kuunda katiba mpya. Kwa maneno mengine nikuwa upo uwezekano kamati isione haja ya kuwa na katiba mpya.
Jamani alichosema tambwe hiza ndiyo msimamo halisi wa kikwete. Kwa wale walioshuhudia majadiliano kwenye ITV watakuwa mashahidi kwamba kuna wakati tambwe hiza alikuwa busy na simu zake mbili akiandika na kusoma sms. Inawezekana wakubwa wa ccm walikuwa wanamtumia maneno ya kufafanua msimamo huo. Watanzania tukae chonjo tusikubali nchi iendeshwe na kikundi cha wachache tu.