TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

Joined
Aug 9, 2016
Posts
13
Reaction score
67
Mradi wa Tushirikishane (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") umeanza rasmi jimbo la Bukoba mjini chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Mbunge Wilfred Lwakatare.

Tokana na misingi ya TUSHIRIKISHANE iliyoelemea katika kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi 4 kati ya jumla ya ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi kwa kushirikiana na wananchi; mada hii itatumika kuwasilisha, kujadili na kupeana taarifa ya kile kinachojiri Bukoba mjini.

Ahadi walizochagua kufuatilia wananchi wa Bukoba mjini kwenye mradi wa TUSHIRIKISHANE

a. Ujenzi wa soko kuu la Bukoba, soko la Kashai na Stendi kuu ya mabasi Bukoba

b. Mikopo ya vikundi vya kijasiriamali vya akina mama na vijana

c. Urasimishaji wa makazi

d. Bima za afya kwa wananchi angalau​

Makubaliano.jpg

Meya wa Manisapaa ya Bukoba, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane

Mada hii itatumika zaidi na Wana Bukoba kutupa taarifa.

Baadhi ya Washiriki watakuwa:-

1. Mh. Mbunge Wilfred Lwakatare
2. Katibu Alex Xavery (Katibu)
3. Happiness Essau (Afisa habari Bukoba)
4. Chief Karumuna (Mayor wa Bukoba)
5. Jimmy Kalugendo (Naibu Mayor)
6. Na washiriki wote wa Warsha hiyo na wale wote wenye mapenzi ya Maendeleo ya Bukoba mjini.

Karibuni...

[HASHTAG]#Tushirikishane[/HASHTAG] [HASHTAG]#Bukoba[/HASHTAG]

Kufahamu majimbo mengine yenye mradi huu tembelea - JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"

======
UPDATE: 1st December, 2016.

Waendeshajinwa mradi wa [HASHTAG]#TUSHIRIKISHANE[/HASHTAG]. Wanawaalika wana tushirikishane katika kikao chetu kwa pamoja kinachotarajiwa kufanyika mnamo tarehe 02/12/2016 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa Bukoba kuanzia saa nane za mchana.

Ufunguzi rasmi wa kikao utaanza saa tisa kamili bila kujali idadi ya wajumbe.

Kuwahi ni muhimu sana, kuhudhuria kwako ndiyo mafanikio ya taarifa nyeti za halmashauri kuwafikia wananchi moja kwa moja.

Mchango wako wa maoni, maswali, na hoja mbalimbali ndiyo chachu ya maendeleo ya jimbo letu.

Kumbuka wewe ni mwakilishi wa mamia, nao wanakutegemea bila kujua, tenda haki na Mungu atakulipa kwa namna yake.

Njooni tupate kujua miradi yetu imepiga hatua kwa kiwango gani mpaka sasa.

Waweza kukili kuhudhuria kwako kwa msg fupi kwenda namba 0765 82 92 56.

Taarifa hii mfikishie na mwenzio.

Asanteni sana na Mungu awabariki.⁠⁠⁠⁠

=====

Akaunti za mradi wa Tushirikishane katika mitandao ya Kijamii:

Tushirikishane (@tushirikishane) • Instagram photos and videos

Tushirikishane | Facebook

Tushirikishane (@tushirikishane) | Twitter
 
Ndugu Wananchi na wadau wa Bukoba Mjini na Kagera; leo nimepata fursa ya kuuliza swali ambalo limetuumiza vichwa wengi kuhusiana na mkoa wetu kuwa kati ya mikoa mitano maskini Tanzania kwa 39% ikizingatiwa kuwa mkoa wa Kagera una historia ya kuwa mkoa tajiri pamoja na Mbeya na Dar es Salaam miaka ya 1960 mpaka tulipokumbwa na vita ya Kagera-Uganda ambayo mpaka leo serikali haijawapa wananchi fidia iliyotolewa na Serikali ya Uganda.

Lakini pia mkoa wetu ulikuwa na shirika la BCU(Bukoba Cooperative Union) ambalo liliweza hata kuikopesha serikali. Leo hii hata Chama cha Ushirika KCU kimesambaratika kwa sababu za kisiasa.

Lakini pia, inatuwia vigumu kiziamini takwimu hizi. Je ni baadhi ya wilaya zenye umaskini au ni Kagera nzima?

Je, serikali imetuwekaje katika Mpango wa Matokeo Makubwa (BRN) ili kurudisha hadhi ya mkoa wa Kagera?

Yafuatayo ni Majibu ya Naibu waziri wa Fedha na Mipango Mh Kijachi.
-Vigezo vilivyotumika katika kubainisha umaskini ni uwezo wa kaya kukidhi mahitaji ya msingi; chakula, mavazi na malazi. Utafiti wa 2011/2012 mkoa wa kagera una kiwango cha 39% ya umaskini.

Ifuatayo ni mipango ya serikali katika kuinua uchumi wa Kagera:

1.Kuendeleza maeneo yenye fursa za uwekezaji na viwanda vidogo na vya kati.kwa kuboresha miundombinu.
3. Serikali inahamasisha wananchi kuzitumia fursa na rasilimali zilizopo ili za kuwapatia kipato.
4.Serikali inaboresha upatikanaji wa pembejeo na masoko ya mazao na uvuvi yanayozalishwa na wananchi.
5. serikali ina mpango wa kuendeleza viwanda vya nyama ili kuendeleza sekta ya ufugaji.
7. Serikali iko mbioni kufufua viwanda vya nguo. Haswa mkoa wa Kagera.
8. Serikali mwezi Disemba itaanza utekelezaji wa kujenga reli ya kati kwa kiwango cha geji kuelekea Mikoa ya Magharibi ikiwemo Kagera ili kufungua fursa za uchumi.

NITUMIE FURSA HII KUWAAMSHA WAZAWA WA KAGERA WALIOKO NDANI NA NJE YA NCHI, KURUDI NA TUIJENGE BUKOBA KWA PAMOJA.

"Mkataa kwao, ni mtumwa."

Imetolewa na:
Mh Wilfred Lwakatare
Mb.Bukoba Mjini.
 
Tatizo la nyie watani wangu, mna mbwembwe na mipango miiiiingi sana, mwisho wa siku hamna kitu.

Muoneni mwenzenu Malinzi hadi anagombea uenyekiti wa mkoa wakati ana uenyekiti wa kitaifa, ambao unamtoa jasho - sifahamu anataka kujifunza mchangani.

Halafu hivyo vitu sijui ahadi za kufuatilia hapo/ vipau mbele mlivyoweka hapo naona ni vya kitoto sana, ambavyo mhaya mmoja tu angevishughulia na nyie mngebaki mnashughulikia mambo mazito.

Haya reserved.
 
Suala la mbwembwe si kwetu tu bali hata serikali kuu, umeona maamuzi mangapi ya kila aina ya mbwembwe yametolewa lakini yanaishia hewani.

Ujenzi wa Soko na Stendi kuu ya mabasi ni vitu ambavyo tumekuwa tukivitaka miaka yote, kila mbunge anayeingia anakuja na ahadi hizo lakini mwisho wa siku mnaingiza siasa na miradi kama hiyo inakufa zaidi tunaoneshwa ramani za miradi hiyo, sasa sijui ramani zinatusaidia nini!!! Tunataka miradi ikamilike. Siasa za kukomoana hatutaki tena Bukoba maana zinazidi kutuumiza sisi wananchi.
 
Wewe mtani,

Unaongelea soko gani? Na stand ipi?
Hivi vyote vipo kwenye mamlaka yenu - local government na si serikali kuu. Hivyo lawama ziwarudie nyie wenyewe na mipango yenu huko huko, mnatakiwa kuachia serikali kuu mambo ya msingi - kama vile mainternational airport, bandari bora, meli kubwa, etc , ila kwa kuwa mmeanza kujitambua basi ninawatakia kila la heri.

Na kwa miradi ambayo ni ya serikali kuu na haijakamilika idaini serikali iikamilishe, ila kwa kuwa nyie ni maskini jeuri mnaweza kuachana na serikali na mkamalizia wenyewe.

Reserved .
 
Shukrani za dhati ziwaendee JF kwa kuona umuhimu wa kuwa na jukwaa kama hili kwa manufaa ya jimbo letu la bukoba. Jambo la msingi ni tushirikishane kwa hoja, maswali, taarifa, maoni, malalamiko na ushauri ili kwa pamoja tulijenge jimbo letu. Karibuni sana
 
inatakiwa pia mpango wa kuondoa/ kuangamiza eishami; ni kero nyingine Bukoba
Kwa hili linahusisha na tafiti za wapi hawa wadudu hutokea, yaani chanzo chake. Kiukweli huwa ni wachafuzi wa mazingira lakini pia ni sumu waingiapo katika mlango wowote wa fahamu wa binadamu.
 
Tatizo la nyie watani wangu, mna mbwembwe na mipango miiiiingi sana, mwisho wa siku hamna kitu.

Muoneni mwenzenu Malinzi hadi anagombea uenyekiti wa mkoa wakati ana uenyekiti wa kitaifa, ambao unamtoa jasho - sifahamu anataka kujifunza mchangani.

Halafu hivyo vitu sijui ahadi za kufuatilia hapo/ vipau mbele mlivyoweka hapo naona ni vya kitoto sana, ambavyo mhaya mmoja tu angevishughulia na nyie mngebaki mnashughulikia mambo mazito.

Haya reserved.
Mtani kiukweli kuna mambo mengi mazuri ambayo nayo yapo katika utekelezaji wake, mazito pamoja na mepesi kama ulivyodai. Tuliyapendekeza haya mepesi ili tuone matokeo yake katika kuyatekeleza chini ya msukumo wa tushirikishane ndani ya muda wa miezi tisa. Baada ya hapo matokeo yake yatatupa taswila ya nini kifanyike, kama tukishindwa kwa haya mepesi basi itakuwa hamna maana ya kuyakabili mazito lakini kama kwa kushirikiana kwa haya mepesi na tukafanikiwa basi tutaenda kujikita kwa hayo mazito. TUSHIRIKISHANE
 
Mtani

Tupo pamoja kabisa, pia nawasifu nyie kwa kuungana na team ya JF kujaribu kupiga hatua kupitia huu utaratibu wa kujipima.

Naamini kama ulivyosema tuanze na hayo madogo then tuone tutafikia wapi na tutaanza vipi kwa yale makubwa.

Hongereni sana, ila nisadie kumuuliza Melo - why huku kwa babu zenu hajafika?
 
Tatizo la nyie watani wangu, mna mbwembwe na mipango miiiiingi sana, mwisho wa siku hamna kitu.

Muoneni mwenzenu Malinzi hadi anagombea uenyekiti wa mkoa wakati ana uenyekiti wa kitaifa, ambao unamtoa jasho - sifahamu anataka kujifunza mchangani.

Halafu hivyo vitu sijui ahadi za kufuatilia hapo/ vipau mbele mlivyoweka hapo naona ni vya kitoto sana, ambavyo mhaya mmoja tu angevishughulia na nyie mngebaki mnashughulikia mambo mazito.

Haya reserved.
Hawajaja hapa leo kuongelea "tatizo lenu" bali kuendelea na utekelezaji wa mipango, hii lugha uliyoitumia hapa haina nafasi kwa sasa... soma vizuri bandiko.
 
Mtani kiukweli kuna mambo mengi mazuri ambayo nayo yapo katika utekelezaji wake, mazito pamoja na mepesi kama ulivyodai. Tuliyapendekeza haya mepesi ili tuone matokeo yake katika kuyatekeleza chini ya msukumo wa tushirikishane ndani ya muda wa miezi tisa. Baada ya hapo matokeo yake yatatupa taswila ya nini kifanyike, kama tukishindwa kwa haya mepesi basi itakuwa hamna maana ya kuyakabili mazito lakini kama kwa kushirikiana kwa haya mepesi na tukafanikiwa basi tutaenda kujikita kwa hayo mazito. TUSHIRIKISHANE
Sasa hebu tupeni kidogo, kuna hatua yoyote ambayo labda ishaanza katika ujenzi rasmi wa mradi wowote kati ya stand na soko make kama ni michoro kwenye tumeiona mda mrefu, vikao vimeshakaa vya baraza la madiwani n.k .Tujulishe mkuu kuna hata jiwe moja limeshawekwa kama starting point ya kujenga msingi? Asante!
 
Hawajaja hapa leo kuongelea "tatizo lenu" bali kuendelea na utekelezaji wa mipango, hii lugha uliyoitumia hapa haina nafasi kwa sasa... soma vizuri bandiko.

Mimi nimeongelea hulka yenu na wala si matatizo yanayowazunguka, naona haujala ndizi leo.
 
Sasa hebu tupeni kidogo, kuna hatua yoyote ambayo labda ishaanza katika ujenzi rasmi wa mradi wowote kati ya stand na soko make kama ni michoro kwenye tumeiona mda mrefu, vikao vimeshakaa vya baraza la madiwani n.k .Tujulishe mkuu kuna hata jiwe moja limeshawekwa kama starting point ya kujenga msingi? Asante!
Unaona na wewe umeanza mbwembwe! Akina nani wamepeleka mawe? Nilidhani ungekuwa unaulizia akaunti namba ili utupie dola za trip 200 za mawe.
 
inatakiwa pia mpango wa kuondoa/ kuangamiza eishami; ni kero nyingine Bukoba
Ila wewe, dah! wahenga wangelikuwepo ungepigwa adhadu, hujui ishami zamani walikuwa wanatengeneza mboga?
teh
 
Ratiba ya utekelezaji iko wapi ili tukienda rikizo Xmass tupitie kuona maendeleo ya utekelezaji labda tunaweza kutupia kwenye account.
 
Kwakweli nafurahi sana kuona mkuu Maxence Melo kwanza..ametupatia chombo huru cha habari cha kueleza maoni yetu..Pili sasa kaja hili swala la maendeleo..Kweli mkuu ubarikiwe na MUNGU na timu yako nzima.
 
Back
Top Bottom