TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

IMG-20160922-WA0008.jpg
LEO NIMEWASILISHA RIPOTI YA KIKAO NILICHOKIFANYA NA BAADHI YA WANA KAGERA WAISHIO JIJINI DAR ES SALAAM KWA MKUU WA MKOA KAGERA.
IMG-20160922-WA0021.jpg
IMG-20160922-WA0027.jpg
IMG-20160922-WA0032.jpg
IMG-20160922-WA0023.jpg
IMG-20160922-WA0023.jpg
IMG-20160922-WA0023.jpg
IMG-20160922-WA0019.jpg

MH. MKUU WA MKOA,

KAGERA.

MAAZIMIO YALIYOPITISHWA KWENYE KIKAO KILICHOITISHWA NA MH. WILFRED LWAKARATE(MB), MBUNGE WA JIMBO LA BUKOBA MJINI, KUJADILI ATHARI ZA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA, KUONA JINSI YA KUSAIDIA WALIOPATWA NA MADHARA.TAREHE 18 SEPTEMBA, 2016 KWENYE HOTELI YA KEBBY'S, MWENGE, DAR ES SALAAM.

1. Kwa kauli moja kikao kimetambua na kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua zakuridhisha kufuatia janga hili, ikiwa ni pamoja na ;
i. Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa, (Mb), Waziri Mkuu, pamoja na kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mh. Freeman Aikael Mbowe (Mb) kufika B ukoba mara moja kuona athari za tetemeko na kushiriki mazishi ya watu waliofariki kutokana na janga hili na pia kuwafariji waliojeruiwa na kuathirika kwa namna mbali mbali.

ii. Kuandaa mkutano wa kuishirikisha jumuiya ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na jumuiya ya wafanyabiashara kwa lengo la kukusanya misaada kwa ajili ya kukabiliana na janga hili.

iii. K uandaa matembezi ya hisani kwa ajili ya kukusanya fedha za kusaidia nakukabiliana na madhara ya janga hili.

iv. Viongozi waandamizi mbali mbali waserikali, wakiwemo Mawaziri, Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Makatibu wakuu na wakuu wa vitengo muhimu vinavyo husiana na maafa kufika kwenye eneo la tukio kwa haraka.

2. Kwa kauli moja kumuomba Mh. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa ndiye baba wa nchi, pamoja na shughuli zake nyingi, kutenga siku mapema itakavyo mpendeza kufika mkoani Kagera kuwapa pole wananchi wake kutokana na janga hili. Tunaamini walioathirika watafarijika sana kumuona Rais wao akiwa nao kwenye eneo la tukio.

4. Kwa kuwa janga hili la kitaifa halina itikadi ya siasa, dini, rangi, kabila wala ubaguzi wa aina yoyote ile, hivyo ushiriki wa watu wote ni muhimu sana.

5. Kwa kutambua ukweli wa walioathirika zaidi ni wananchi wa mkoa wa Kagera, inawapasa wao kuwa msitari wa mbele katika kushiriki katika juhudi zote zinazofanyika, kwa njia na jinsi yoyote inayowezekana, iwe ni kwa hali au mali, mshikamano wao katika janga hili ni muhimu sana. Mpaka sasa, imejidhihirisha kwamba ushiriki wa wana Kagera bado ni hafifu sana. Wana kagera wanahimizwa kutokukata tamaa nakuamsha hari ya kushirikiana katika kuusaidia mkoa wao kwa nidhamu ya hali ya juu . Ili kusisitiza umuhimu huo, mfano wa kwamba ili kuweza kupewa msaada wa usafiri (lift) ni lazima uwe njiani, unahusika.

6. Kwamba kutokana na mkoa wa Kagera kukumbwa na maafa makubwa na mengi mfululizo kuanzia miaka ya 1970 zilipoanza chokochoko za nduli Iddi Amini wa Uganda, vita vya Uganda , Ukimwi, mdudu wa migomba (ekiuka), madhara ya wakimbizi kutoka nchi jirani yaliyo leta ujambazi , kufa kwa Vyama vya Msingi vya Ushirika na Chama Kikuu cha Ushirika (BCU/ KCU) kulikoambatana na kuanguka kwa bei ya zao la kahawa, kuanguka kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kulikosababisha bei za bidhaa za viwandani ambavyo vingi vipo Dar es salaam, kuwa juu kuliko sehemu nyingine yoyote ya Tanzania, ugonjwa wa mnyauko ambao umeangamiza kabisa migomba na zao lake ndizi, na sasa ni janga la tetemeko. Majanga hayo yote ni sababu kubwa kwa mkoa wa kagera kushuka sana kiuchumi kutoka kati ya mikoa mitatu tajiri miaka ya 70 - 80 hadi kuwa kati ya mikoa mitano masikini sana nchini. Serikali inaombwa ichukue hatua za makusudi kutoa upendeleo wa kisera wa kuusisimua upya uchumi (a stimulus package) kwa mkoa wa Kagera kwa kufanya yafuatayo :

i. Kutoa msamaa wa kodi zote kwenye bidhaa zote za ujenzi zinazouzwa mkoani Kagera kwa kipindi cha miaka kumi.

ii. K wa kutambua madhara ya mdororo wa uchumi wa mkoa wa Kagera kwa muda mrefu hivyo kuwepo tatizo kubwa la ajira na umasikini, miradi yote ya ujenzi wa miundombinu ya kijamii kama mashule, zahanati, vituo vya afya na majengo mengine ya serikali yatakayo jengwa upya au kukarabatiwa, ugawaji wa kandarasi ufanywe kwa mtindo wa uwezeshaji kwa makampuni yaliyopo na yanayoendesha shughuli zao mkoani kagera yenye uwezo, wakishirikiana na makampuni ya wana -Kagera walioko nje ya mkoa pale inapobidi . Vigezo vitaandaliwa ili vizingatiwe.

7. Kwa kutambua kuwa serikali imeunda kamati za maafa za Kitaifa na Mkoa ambapo Wabunge wa mkoa wa Kagera wameshirikishwa, ni vyema ushiriki kwenye kamati hizo upanuliwe na kuzijumuisha taasisi za dini ambazo mkoani kagera zimekuwa na mchango mkubwa katika utoaji wa huduma za jamii kwa miaka mingi. Hatua hii itasaidia kuongeza ufanisi katika zoezi zima la uthamini wa madhara, ukusanyaji wa taarifa na usambazaji wake. Aidha kwenye hizo kamati uwepo umuhimuwa ku wahusisha wataalam wa habari kuongeza ufanisi katika upashanaji wa habari .

8. Kwa kuzingatia mamlaka ya Mbunge anayopewa na katiba ya jamhuri ya Muungano wa T anzania, mifuko ya majimbo pia itumike kusaidia kwenye majanga yamaafa kama haya.

9. Kwa kukubali kwamba bado uitikiaji na ushiriki wa wana -Kagera bado ni hafifu sana, juhudi mpya zifanyike kwa kuishirikisha Serikali ya mkoa wa Kagera, Wabunge wote wa mkoa na viongozi wa dini zote kuitisha mkutano/ kusanyiko jingine haraka iwezekanavyo hapa dar es salaam kwa lengo la kuwashirikisha wana-Kagera na wadau wengine wote wenye mapenzi mema, katika kuonyesha kuguswa kwetu kama jamii na tatizo hili, tukusanye rasilimali kusaidia kwenye janga hili. Ndiyo njia pekee ya kuonyesha kuwa tunahitaji kupatiwa msaada wa usafiri (lift), hivyo ni vyema tukawa njiani.

NB : Katika kikao hicho cha wana kagera ahadi za jumla ya Tshs. 6,780,000/= zilitolewa na pesa taslimu Tshs. 1,480,000/= na kuleta jumla ya Tshs. 8,260,000/=

Sekretarieti iliyoundwa inaendelea kuratibu ukusanyaji wa michango hiyo ili itakapokamilika iwasilishwe sehemu husika.

Imewasilishwa leo tarehe 22/09/2016

Ofisi ya mkuu wa mkoa.

Wilfred Muganyizi Lwakatare (Mb)

Jimbo la Bukoba Mjini.

K. N.Y Wana Kagera wanaoishi Dar es Salaam (Waliohudhuria kikao hicho).

NAKALA KWA;

Mh. Waziri Mkuu.

Viongozi wakuu wa madhehebu ya kidini.

Viongozi wa vyama vya siasa.

Waheshimiwa wabunge wote wa mkoa Kagera.

Waandishi wa Habari.
 
Tatizo la nyie watani wangu, mna mbwembwe na mipango miiiiingi sana, mwisho wa siku hamna kitu.

Muoneni mwenzenu Malinzi hadi anagombea uenyekiti wa mkoa wakati ana uenyekiti wa kitaifa, ambao unamtoa jasho - sifahamu anataka kujifunza mchangani.

Halafu hivyo vitu sijui ahadi za kufuatilia hapo/ vipau mbele mlivyoweka hapo naona ni vya kitoto sana, ambavyo mhaya mmoja tu angevishughulia na nyie mngebaki mnashughulikia mambo mazito.

Haya reserved.
Huyo malizi bora afunge virago sioni anachofanya
 
Wilfred Lwakatare hongera sana kwa kuwafikia wanakagera waishio Dar na mikoa ya karibu na Dar maana wanasema ''Akanyonyi katagenda tikamanya ihanga elyeza obhuro'' Tshs. 8,260,000/= si haba ila kinahitajika kiasi kikubwa zaidi ili wahanga wapate shufaa. Dar kuna wahaya wengi wana pesa na wanaweza kuchanga pesa zaidi ya hiyo, sasa majigambo na vurugu mjini za nini kama wanakuwa mabahiri hivi au ndio ''Akawe, kawe kajunda nokara'' ila Mungu ni wetu sote, wamesahau.

Serikali mpaka sasa bado hakijaeleweka, mara tusisubirie misaada ya serikali maana tetemeko halijaletwa na ccm. Haya maneno yatawakaanga wenyewe, Bati akati akalakusiga amazi onya okalibatile.

Usikate tamaa wewe wasaidie wahanga wakati huu wa shida, watakumbuka fadhira zako 2020 maana tugamba ''Akutwala ekilo omusima omushana''
 
Wapendwa,

Salaam.

Kipindi hiki kilikua kigumu sana kwetu lakini nashukuru Mungu alikua pamoja nasi[emoji120] Natumai wengi mmerejea kwenye shughuli zenu za kila siku.

Pamoja na shida nyingi tulizopata kutokana na tetemeko bado hatujasahau sababu iliyotuunganisha sisi hapa kwa maana tetemeko limepita/litapita na maisha lazima yaendelee, na ndoto zetu kuzitimiza kwa pamoja

Niwakumbushe juu ya vipaumbele vyetu vinne;
-Ujenzi wa Soko Kuu, soko la Kashai na Stand Mpya ya Mabasi
-Urasimishaji Makazi
-Mikopo kwa Wanawake na Vijana na
-Bima ya Afya

Ukiacha kamati ya maafa ambayo inasimamiwa na Mkuu wa Mkoa, shughuli nyingine zote zinaendelea kama kawaida katika maeneo na taasisi nyingine zote ikiwemo ofisi ya Manispaa ya Bukoba. Hivyo basi, pamoja na kuumizwa sana na tetetemeko na athari zake ambavyo hatuwezi acha zungumzia, tujikite pia katika kuulizia na kufatilia vipaumbele vyetu vimefikia hatu zipi za ufanikishaji. Hii inatokana na ukweli kwamba si siku nyingi sana tutagundua kuwa bado hatupendi soko letu, stand yetu, vijana na wanawake hawana mitaji, upatikanaji wa huduma za afya bado ni changamoto n.k.

Nirudie tena kuwapa pole nyote mliopatwa na athari kubwa ya tetemeko. Niwatakie pia siku njema!

Bwana atuwezeshe[emoji120]
 
Misaada ya waathirika wa tetemeko imeishiwa wapi? Naona muda unayoyoma hakuna suala la kueleweka.
 
Misaada ya waathirika wa tetemeko imeishiwa wapi? Naona muda unayoyoma hakuna suala la kueleweka.
Huo sio msaada tena mkuu kwasababu msaada huwa na maana pale unapokidhi maana haswa ya msaada (ajuna akanyonyi akajuna kakyahalala)

Haiwezi kuwa na maana tena mtu aombe msaada leo halafu wewe umwambie labda mwakani, ikitokea hivyo, mwingine anaweza kabisa akakwambia basi acha make haitakuwa na maana. Na mwingine anaweza asikwambie lakini akakuacha tu wewe ujipime na ujiulize kama kweli hicho kitakuwa bado ni msaada ama utakuwa unafanya kutimiza tu wajibu ( kabambone). Kwa hapa tulipofika, hata ikitolewa itakuwa ni kutimiza tu wajibu na si kusaidia

Imagine mtu alianza hana pa kulala wiki nzima na hukumsaidia, baadae akajikokota akapata bati mbili akapata pa kuweka kichwa, eti leo amepata bati zake 15 ndo unajifanya kwenda kumsaidia umpe bati 5 eti asinyeshewe, alipokuwa ananyeshewa kwa wiki mbili zote mfululizo wewe ulikuwa uko wapi? Haya mpaka mwezi umeisha bado tu utasema umeenda kusaidia?
 
Dah afadhali nilikuwa nautafuta Uzi huu kwa muda mrefu. Hongereni sana kwa mradi huu wenye msukumo na chachu ya kuleta maendeleo natumaini safari hii tutaona umuhimu wa wawakilishi wa wananchi kuliko zile sanaa tulizoziona kwa miaka iliyopita. Natumaini mradi huu Utakuwa chachu ya kiutendaji na utapelekea wananchi kuhukumu kwa haki ifikapo 2020. Hongera wana Tushirikishane kwa kuthubutu. Nimwombe mbunge wangu sasa akubali kumshirikisha Mh. Amani kwenye miradi tajwa maana tayari ana mwanga kwakuwa alishauanza mchakato wa miradi hiyo.
 
Wapendamaendeleo wa Bukoba,

Salaam.

Napenda kuwafahamisha kuwa kuanzia jumaatatu ya tarehe 10-10-2016 nitaweza kuleta kwenu taarifa zote za hatua za mradi wetu wa "Tushirikishane" baada ya kushindwa kuwajulisha hatua zilizofikiwa na mradi kwa takriban mwezi mzima.

Kuchelea kwetu katika hili kwa muda huo wote kumetokana na sababu ya ofisi ya mbunge ambayo ndiyo tunafanya nayo kazi moja kwa moja kujikita katika shughuli za "tetemeko". Kwa sasa ofisi ya mbunge imerejea katika shughuli zake za awali.

Nitawafahamisha kila hatua zinazofikiwa na mradi katika vipaumbele vyetu vinne ambavyo ni;

i) Ujenzi wa Soko Kuu, Soko la Kashai na Stand Mpya ya Mabasi

ii) Urasimishaji Makazi

iii) Mikopo kwa Wanawake na Vijana, na

iv) Bima ya Afya

Kama ilivyokwisha elezwa awali kuwa vipaumbele hivi vinne ni makubaliano ya pamoja kati ya Mbunge, Jamiiforums na Wananchi na kuwa ndivyo vitakavyoshughulikiwa katika kipindi chote cha mradi

Mradi wa "Tushirikishane" ni wa miezi tisa (9). Miezi miwili imekwisha kupita, tunatarajia miezi saba (7) iliyopo mbele yetu kuwa ya mafanikio zaidi


Bwana atuwezeshe!!
 
Naomba kuchukua fursa hii kuwaomba radhi wana tushirikishane humu ndani kwa ukimya ambao umekuwa ukiendelea humu ndani hasa wa mbunge na taasisi nzima ya ubunge wa bukoba mjini kwa kutotoa taarifa juu ya maazimio ya tushirikishane.

Tujue na tukubaliane kwa pamoja kwamba janga la tetemeko limevuruga kila kitu na utaratibu wote wa maisha katika mkoa kagera hasa ndani ya manispaa ya bukoba.

Mbunge kama mwakilishi wa wananchi wa jimbo zima umekuwa wajibu wake kuhakikisha kila linalowezekana kwa hali na mali vilio vya wahanga vinasikika kwa serikali na wadau mbalimbali kutoka kila pembe ya dunia ili wapate misaada inayostahili, haya yote yamefanyika mchana na usiku japo mengine hayaonekani kwa uwazi (invisible).

Tunashukuru Mungu baada ya wiki kadhaa za taharuki sasa hali imeanza kutulia na kuhisi tetemeko linaweza kutorejea kwa siku za hivi karibuni.

Pamoja na kwamba madhara ya tetemeko la ardhi yanazidi kuongezeka badala ya kupungua ila pia serikali, rasmi imejitoa katika swala la kuwasaidia waathirika mmoja mmoja kwa maswala ya ujenzi wa makazi yaliyoharibika kwa kudai inao mzigo mkubwa wa kurekebisha miundo mbinu ya taasisi kama mashule, dispensali na barabara vilivyoathiriwa na tetemeko la ardhi.

Imetuwia vigumu sana kama taasisi ya mbunge kufikisha huduma za msingi kwa wahanga kutokana na serikali kupitia kamati ya maafa ya mkoa kuhodhi kila kitu kuhusu misaada kwa wahanga, ukusanyaji na ugawaji wa misaada. Lakini mwisho wa siku misaada ya msingi kutowafikia kikamilifu wahanga.

Lawama zimekuwa nyingi sana kutoka kwa wananchi kuwaelekea viongozi wao wa kuchaguliwa (wawakilishi), mbunge, madiwani, wenyeviti wa mitaa na wajumbe wao bila kujua ki uhalisia kuwa hawajahusishwa kikamilifu katika uratibu mzima wa shughuri za maafa kuanzia kuwabaini waathirika pamoja na ugawaji wa misaada ya vyakula, maturubai na magodoro vilivyotolewa kwa uchache sana mpaka sasa.

Tangu tarehe 04/08/2014 ofisi ya mstahiki Meya wa manispaa ya bukoba kwa kushirikiana na ofisi ya mbunge bukoba mjini wameanza ziara ya jimbo zima kupitia kata kwa kata na kufanya vikao vya ndani vya kata ili kusikiliza maoni, maswali, ushauri na changamoto wanavyokutana navyo na zaidi uhitaji wa wahanga kuringanisha na huduma zilizokwishatolewa na kamati ya maafa mkoa, kisha ofisi ya mstahiki Meya kwa kushirikiana na ofisi ya mbunge bukoba mjini watafanya majumuisho na kutengeneza ripoti itakayokabidhiwa serikalini kwa ajili ya hatua za ziada.

Asanteni kwa uvumilivu mliouonesha kwa kipindi hiki kigumu kilichotukuta, Inshallah wiki ijayo tutarejea katika maazimio yetu kama *Jamii Forum Tushirikishane jimbo la bukoba mjini* ili tuone kama pamoja na haya majanga lakini tunaweza kufanikisha malengo yetu na maisha lazima yaendelee.

Tuombeane uzima ili tuzidi kwa pamoja kuwatumikia watu wa Mungu kwa sababu ndiyo maisha tuliyoyachagua.

*Na Alex Xavery-Katibu wa Mbunge jimbo la Bukoba mjini*
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Baadhi ya mambo yaliyoko nje ya mradi lakini ni ya faraja sana kwa watu wa BMC ni ujenzi wa barabara ya mafumbo kwa kiwango cha rami (picha hapo juu). Barabara hii ilikua kero ya muda mrefu kutokana na kuwa na mashimo mengi hivyo kupitika kwa shida, lakini kwa sasa ni shangwe kwa wakazi wote wa ukanda huo......wanatereza tu[emoji28]. Hongera sana kwa uongozi wa BMC
 
Hakika ni jambo la kujivunia pongezi kwao wote waliowezesha kufanikiwa kwa ujenzi wa kiwango cha lami. Maendeleo hayaji kwa maneno tu bali kwa vitendo nina imani sasa tutayaona Yale tuliyokuwa tukiyalilia kila kukicha
 
325ff1dcbd99554a642d184058280b1a.jpg
42102f43cf3c608c0409e4534b0655e7.jpg
5823fe20749056d4d5b8bb180085cc4d.jpg
aeeaa71058d31f61186fdcf0393ed84b.jpg
5594289cd982ef011e018caa90b93824.jpg


Mwonekano wa soko la Kashai leo 10-10-2016. Ujenzi wa Soko hili ni moja kati ya vipaumbele vya "Tushirikishane"

Kashai ni kata yenye mitaa mingi kuliko kata nyingine zote, mitaa tisa (9). Lakini pia ni kata ambayo ina wakazi wengi zaidi katika manispaa ya Bukoba. Na soko la Kashai ndio soko linalofuatia kwa kuhudumia watu wengi wa BM baada ya Soko Kuu
 
325ff1dcbd99554a642d184058280b1a.jpg
42102f43cf3c608c0409e4534b0655e7.jpg
5823fe20749056d4d5b8bb180085cc4d.jpg
aeeaa71058d31f61186fdcf0393ed84b.jpg
5594289cd982ef011e018caa90b93824.jpg


Mwonekano wa soko la Kashai leo 10-10-2016. Ujenzi wa Soko hili ni moja kati ya vipaumbele vya "Tushirikishane"

Kashai ni kata yenye mitaa mingi kuliko kata nyingine zote, mitaa tisa (9). Lakini pia ni kata ambayo ina wakazi wengi zaidi katika manispaa ya Bukoba. Na soko la Kashai ndio soko linalofuatia kwa kuhudumia watu wengi wa BM baada ya Soko Kuu
Naam, ujenzi wa soko hili ukitekelezwa na kukamilika utakuwa wa tija sana kwa maendeleo ya kata hii ya Kashai. Mungu atuongoze kutekeleza
 
Naam, ujenzi wa soko hili ukitekelezwa na kukamilika utakuwa wa tija sana kwa maendeleo ya kata hii ya Kashai. Mungu atuongoze kutekeleza
Lijengwe na kuboreshwa Soko Kuu ndo ilo la kashai liboreshwe, haiwezekani kuacha soko linatoa huduma karibu ya kila kitu tukimbilie la Kashai wanalouza samaki,ndizi,viazi na mihogo.

Hivi mbunge wangu bado yuko Bukoba au kasharudi KWAKE Kimara?
 
Baadhi ya mambo yaliyoko nje ya mradi lakini ni ya faraja sana kwa watu wa BMC ni ujenzi wa barabara ya mafumbo kwa kiwango cha rami (picha hapo juu). Barabara hii ilikua kero ya muda mrefu kutokana na kuwa na mashimo mengi hivyo kupitika kwa shida, lakini kwa sasa ni shangwe kwa wakazi wote wa ukanda huo......wanatereza tu[emoji28]. Hongera sana kwa uongozi wa BMC

Hii ndio inaelekea Mafumbo na Kahororo? Kama ndio yenyewe basi shukrani sana maana hii ilikuwa ni aibu sana.
 
Lijengwe na kuboreshwa Soko Kuu ndo ilo la kashai liboreshwe, haiwezekani kuacha soko linatoa huduma karibu ya kila kitu tukimbilie la Kashai wanalouza samaki,ndizi,viazi na mihogo.

Hivi mbunge wangu bado yuko Bukoba au kasharudi KWAKE Kimara?
Ujenzi wa soko kuu, soko la Kashai na stand ya mabasi utafanyika kwa pamoja na hiki ni kipaumbele namba moja katika "Tushirikishane Bukoba"
 
Back
Top Bottom