DON SINYORI
JF-Expert Member
- Aug 3, 2016
- 511
- 417
hehhehe hivi ule mpango wenu wa kuigeuza bikoba kuwa dubai umefikia wapi? naomba updates plz
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ujenzi wa stand mpya maendeleo yaliyofanywa karibuni ni kulipa fidia kwa watu watatu waliokuwa wamegoma sh 12,000,000 kama walivyokubali baadae na watu wa Nemc kuja kufanya tathimini tayari. Tunasubiri kupata certificate yao soon. Hatutakuwa na kikwazo zaidi.Sasa hebu tupeni kidogo, kuna hatua yoyote ambayo labda ishaanza katika ujenzi rasmi wa mradi wowote kati ya stand na soko make kama ni michoro kwenye tumeiona mda mrefu, vikao vimeshakaa vya baraza la madiwani n.k .Tujulishe mkuu kuna hata jiwe moja limeshawekwa kama starting point ya kujenga msingi? Asante!
Ujenzi wa soko maandalizi yanakwenda vizuri. Wiki ijayo consultant na watu wa TIB watakuwa hapa Bukoba kwa mazungumzo. Kila kitu kinaendelea vizuri.Sasa hebu tupeni kidogo, kuna hatua yoyote ambayo labda ishaanza katika ujenzi rasmi wa mradi wowote kati ya stand na soko make kama ni michoro kwenye tumeiona mda mrefu, vikao vimeshakaa vya baraza la madiwani n.k .Tujulishe mkuu kuna hata jiwe moja limeshawekwa kama starting point ya kujenga msingi? Asante!
Nimeeleza hatua tulizofikia katika utekelezaji nikijibu hoja ya mjumbe mmoja wapo humuRatiba ya utekelezaji iko wapi ili tukienda rikizo Xmass tupitie kuona maendeleo ya utekelezaji labda tunaweza kutupia kwenye account.
Anaweza kuja kujibu mwenyewe lkn taarifa ni kwamba mradi umeanzia kwa majaribio ndani ya majimbo 8 kama sio 9 kwa tanzania nzima, then ikionyesha inaleta tija basi majimbo yote yatafikiwa. Jifunze kwanza kupitia huku kwetu.Mtani
Tupo pamoja kabisa, pia nawasifu nyie kwa kuungana na team ya JF kujaribu kupiga hatua kupitia huu utaratibu wa kujipima.
Naamini kama ulivyosema tuanze na hayo madogo then tuone tutafikia wapi na tutaanza vipi kwa yale makubwa.
Hongereni sana, ila nisadie kumuuliza Melo - why huku kwa babu zenu hajafika?
Kwa kweli ni jambo la kupongezwa.Kwakweli nafurahi sana kuona mkuu Maxence Melo kwanza..ametupatia chombo huru cha habari cha kueleza maoni yetu..Pili sasa kaja hili swala la maendeleo..Kweli mkuu ubarikiwe na MUNGU na timu yako nzima.
Tuko pamoja, michango yenu ya mawazo ni muhimu sanaSafi, tunasubiria kujifunza kutoka Jimbo la Bukoba mjini...
Kwa kipindi hiki figisu figisu hazina nafasi. Kazi zinaendelea, ondoa shaka.Suala la mbwembwe si kwetu tu bali hata serikali kuu, umeona maamuzi mangapi ya kila aina ya mbwembwe yametolewa lakini yanaishia hewani.
Ujenzi wa Soko na Stendi kuu ya mabasi ni vitu ambavyo tumekuwa tukivitaka miaka yote, kila mbunge anayeingia anakuja na ahadi hizo lakini mwisho wa siku mnaingiza siasa na miradi kama hiyo inakufa zaidi tunaoneshwa ramani za miradi hiyo, sasa sijui ramani zinatusaidia nini!!! Tunataka miradi ikamilike. Siasa za kukomoana hatutaki tena Bukoba maana zinazidi kutuumiza sisi wananchi.
Asante sana, michango yenu ya mawazo ni muhimu pia ili tushirikishane kikamilifu kuhakikisha tunasonga mbeleAsante sana Jamii Forums,,,,,
kwa hili najua maendeleo lazima yapatikane,,,
Asante pia wakuu viongozi husika kwa kukubali wito maana kwa kufanya hivyo ndiyo njia pekee ya kuweza kufikia malengo
Hata mbuyu ulianza kama mchichahehhehe hivi ule mpango wenu wa kuigeuza bikoba kuwa dubai umefikia wapi? naomba updates plz
Kwa kushirikishana, kimawazo, maoni, ushauri na hoja mbalimbaliBukoba isonge mbele.naimani itawezekana
Mradi wa Tushirikishane (JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") umeanza rasmi jimbo la Bukoba mjini chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Mbunge Wilfred Lwakatare.
Tokana na misingi ya TUSHIRIKISHANE iliyoelemea katika kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi 4 kati ya jumla ya ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi kwa kushirikiana na wananchi; mada hii itatumika kuwasilisha, kujadili na kupeana taarifa ya kile kinachojiri Bukoba mjini.
Ahadi walizochagua kufuatilia wananchi wa Bukoba mjini kwenye mradi wa TUSHIRIKISHANE
a. Ujenzi wa soko kuu la Bukoba, soko la Kashai na Stendi kuu ya mabasi Bukoba
b. Mikopo ya vikundi vya kijasiriamali vya akina mama na vijana
c. Urasimishaji wa makazi
d. Bima za afya kwa wananchi angalau
View attachment 389799
Mawazo ni mazuri ingawa wengi wetu tulitegemea haya mambo tuyaone kama taarifa katika utekelezaji wake na wala siyo kukusanya mawazo kupitia JF.
USHAURI WANGU
Kwa viongozi wa halmashauri mnaohusiki msipo angalia mtamaliza vipindi vyenu hata kufanya chochoe. Hii ni kwa Mhs Mbunge na Mayor etc.
Cha kufanya kwa mwendo wa KASI, ninapendekeza kwa issue ya SOKO na Stand, weka mikakati kwa kushirikiana na Bank mojawapo ili mpate mkopo wenye uafadhari wa masharti na kusimamia nyie hizo projects. Isimamiwe kama unavyosimamia ujenzi wa nyumba yako mwenyewe otherwise watu wa BKB ni watu wa deal na mtaanguka. Na mkicheza bila kufanya haya hata katika chaguzi zijazo hamna lenu, maana tunawasubiri katika hili. Nafasi mnayo na sasa fanya kazi.
NB: Tafuta mchumi mzuri na alipwe ili aifanyie kazi. Ikishindikana kaangalie halmsahauri zilizofanikiwa hapa Tanzania na copy ili haya mambo yafanyike haraka sana.
Haya tunawasubiri.......
Meya wa Manisapaa ya Bukoba, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane
Mada hii itatumika zaidi na Wana Bukoba kutupa taarifa.
Baadhi ya Washiriki watakuwa:-
1. Mh. Mbunge Wilfred Lwakatare
2. Katibu Alex Xavery (Katibu)
3. Happiness Essau (Afisa habari Bukoba)
4. Chief Karumuna (Mayor wa Bukoba)
5. Jimmy Kalugendo (Naibu Mayor)
6. Na washiriki wote wa Warsha hiyo na wale wote wenye mapenzi ya Maendeleo ya Bukoba mjini.
Karibuni...