TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] 4 years no update, viongozi waone aibu,
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] 4 years no update, viongozi waone aibu,
Hapo manispaa si CCM si wapinzani wote ni majanga, kiufupi hawajitambui na wanapenda sana kuwa wa mwisho katika kila jambo
 
[emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji15] 4 years no update, viongozi waone aibu,
Hapo manispaa si CCM si wapinzani wote ni majanga, kiufupi hawajitambui na wanapenda sana kuwa wa mwisho katika kila jambo
 
Huu ujenzi unaanza lini na hizo hatua zimefikiwa lini dada make isije kuwa ni mambo yaliyokwishafikiwa toka miaka hiyo mpaka leo hatua ni zile zile za miaka 3 iliyopita
 
Dada hebu tusaidie utujulishe pia na ile miradi yetu ya tushiriishane kipi kimeendelea toka mwezi jana ni hatua gani imefikiwa
 
Asanteè...mbunge wa bukoba mjini kiukweli anafaa japokuwa sio mbunge wa jimbo langu ila siku moja nilibahatika kukaa naye karibu ...ana mikakatii mizitooo...tumuombee
 
Sio Mbunge pekee bali pia Meya na naibu meya nao wote wamekaa kimya sana hawasemi chochote wala kujibu hoja zetu.
Hii ni dharau ya hali ya juu na ni aibu kubwa kumuona naibu meya akiwa concerned na mambo yanayoendelea kwa wenzao lakini wakashindwa kujibu hoja zilizotoka kwa wananch wao.
mi nasubiri uitishwe mkutano wowote wa wananchi na Mbunge siku hiyo watakimbia jukwaa maana sasa wameudhihirishia umma wa wanasiasa wote baba yao mmoja.
Mh. Lwakatare anatakiwa kufahamu kuwa alichaguliwa kuwa mbunge kwakuwa hakukuwa na jinsi na ili ndo tatizo kubwa ambalo linai face bukoba nadhani ni muda sasa vijana wenye machungu ya maendeleo kuanza kujiandalia njia maana huyu mbunge hiki ndo kipindi chake cha mwisho.
hatambui kuwa kuna nguvu kubwa ilifanya kazi ya ziada bila hata kumtaarifu yeye nguvu hii ilitokana na vijana wazalendo wenye tamaa ya kuiona bukoba ikipiga hatua sasa tumwambie tu kuwa nguvu ile ile itatumika 2020 kumuweka pembeni akapumzike. Tumechoka na ahadi hewa.
 
Asanteè...mbunge wa bukoba mjini kiukweli anafaa japokuwa sio mbunge wa jimbo langu ila siku moja nilibahatika kukaa naye karibu ...ana mikakatii mizitooo...tumuombee
Mikakati mingi mda wake unafikia ex.date hata kuanza haijaanza ...siku ikianza ndo muda muafaka wa kupongeza
 
Asanteè...mbunge wa bukoba mjini kiukweli anafaa japokuwa sio mbunge wa jimbo langu ila siku moja nilibahatika kukaa naye karibu ...ana mikakatii mizitooo...tumuombee

Livinus Mikakati isiyo na utekelezaji au isiyoonyesha mwelekeo ni mikakati mfu. kwenye miradi ya Tushirikishane hawakutakiwa kuji commit kuleta mikakati mizito wasiyoweza kuibeba walitakiwa waweke malengo yaliyo ndani ya uwezo wao. sioni kama hiyo miradi tajwa ina uelekeo wa kutekelezwa zaidi ni adithi za alinacha tu.
 
Reactions: Lee
Ni kweli unachokisema mkuu..na vizuri ata huyu mwenye mawazo ata kama hayatotekelezwaa yote ila atlest anakuja na changamoto
 
Mkuu nakuunga mkono 200%. Hawa jamaa wana matatizo sana aisee, mie sikuwepo kwenye mkutano wa bumudeco 2015 lakini muhtasari wa kilichosemwa na majukumu yalivyowekwa niliyapata walau kwa kiasi.

Hebu tuanze na BUMUDECO, na ikumbukwe Mbunge ndo alikuwa mwandaaji wa tukio hilo. Alizunguka kila kona kutangaza na kwa sifa kedekede kwamba sasa tumuamini kabadirika, sahivi yuko na wapiga kura, anataka kuwa wa mfano n.k, na baada ya hapo yakapitishwa maazimio na kwa kiasi kikubwa ofisi yake kupitia kwa mayor wake ilipewa maagizo ya kuchukua na kufanya. Cha hajabu hadi leo mwaka unaelekea kuisha hatujawahi kumsikia hata popote pale na wala kufanya mkutano jimboni kuwaambia wananchi ni nini kilipangwa ama kutoa taharifa ya utekelezaji kwa yale yaliyotokana na BUMUDECO, yeye na meya wako wamekuwa wasiri kweli kweli, wamekuwa manunda na mabubu. Ila wanasema tuwasaidie, unamsaidiaje asiyetayari kusaidika na ni wapi wananchi wakakataa kupokea habari nzuri za miradi yao wenyewe?

Likaja la pili, Leo tunaona picha za miradi ile ile iliyoletwa mtandaoni tokea 2012. Tunajua wakati ule ilikwama kwasababu ya kugawanyika kwa baraza la madiwani, lakini leo chini ya mayor b.la madiwani liko chini ya chama chake na hakuna mgawanyiko, bado mpaka leo tunaoneshwa picha, kazi imekwama nini katika baraza hili hawataki kusema. Wamemaliza mwaka sasa hakuna hata jiwe moja la msingi lililopelekwa pale site. Hawa hawa ukiwasikiliza ndo wanaochambua mwaka 1 wa JPM kafanya nini na kashindwa nini ila ukiwauliza wao wapi wameweza hapo unawatafuta ubaya, kana kwamba wao hawakupewa majukumu kwenye maeneo/kata na manispaa zao.

Sasa huyu mbunge anaweza akawa hajui kiini haswa cha yeye kupewa kura 2015. Yawezekana kasahau unyenyekevu wake alipochaguliwa na jinsi wanabukoba walivyosimama kumpigania hadi wabibi wakikesha siku 3 vituoni kusubiri kupiga kura kwenye BVR. Leo haonekani akiitisha mikutano, haonekani Jf wala kwenye mitandao akingea na waliompeleka Dodoma, ameshindwa kusahihisha makosa yake tena kwa mara ya pili. Tunakaa hapa tunamuuliza Happy maswali ambayo alitakiwa kuulizwa mbunge na timu yake chini ya meya, ila hawapo na hawako tayari.

Hakika, mwaka 2020 hautapita hawa watu hawajaojiwa. Ni Bukoba na Tabora kisiasa panajulikana, msimu mmoja waweza kutosha kuwapa wananchi kukufanyia tathimini na ukaondoka, ila kwa Lwakatare kusuka na kunyoa atachagua mwenyewe na anayo hiyo nafasi bado ya kuchagua palipo sahihi.
 

Ndugu Umeongea kweli tupu.
Binafsi niliudhuria kongamano la BUMUDECO mwaka jana lilikuwa ni kongamano lilikuwa na mtazamo mpana na wenye kujenga shauku kwa wengi walioudhuria wakiwa na nia ya kuona mkwamo wa kimaendeleo kwa Bukoba ukifika kikomo.
wanakagera na wapenda wmaendeleo wengi walisupport na kumuona mbunge kuwa sasa kaja kivingine lakini ukiwauliz walio wengi kama kuna uelekeo kwa kile walichokitegemea nadhani wengine watakupiga makofi. Lilikuwa ni kongamano lililorudisha matumaini mapya. nakumbuka Mzee Rugemalira alitoa taarifa kuwa alitaka kufanya uwekezaji mkubwa kwa kujenga Hospital kubwa ya moyo. sasa kinachoshangaza manispaa kwa sasa iko mikononi mwa watu wanaozungumza lugha moja hapa namaanisha kuwa Mbunge, Meya na Naibu Meya na idadi kubwa ya madiwani wanatokea chama kimoja je kama hiyo miradi yao bado haijawa na mwelekeo wanashindwa nini kusaidia na kusukuma mradi huu wa ujenzi wa hospital kubwa ambayo tayari mwekezaji tena ambaye ni mzawa yuko tayari?

Nimwambie tu mbunge wetu kuwa asione wananchi wako kimya akadhani ukimya wao unamuweka in a safe side bali atambue tu kuwa anajikaanga kwa mafuta yake na kama anatuona sisi tunaozungumza hapa akatuchukulia kama wapinzani wake basi asubiri siku akiitisha mkutano wa wananchi ndo haya haya atakutana nayo maana wengi hawana pa kuyasemea na tunaposikia tunajitahidi kuyaleta sehemu amabako tunaamini yanamfikia moja kwa moja.
 

Unafiki na siasa zisizo na mlengo ndo zinazotupeleka kusiko. Meya na baraza lake la madiwani ndo dira ya halmashauri kukiwa na meya ambaye ana vision na akawa creative basi mambo yataflow. hivi manispaa yetu imeingia mkenge kwa siasa hizi hizi unafiki pamoja na kwamba jimbo liko mikononi mwa wapinzani lakini kwenye nafasi ya meya walikosea kabisa maana, tayari Mh. Amani ni part ya ukawa na kwakuwa lengo lilikuwa ni kusonga mbele huyu ndiye alikuwa right candidate angeweza kuisukuma hii miradi kwakuwa yeye ndiye master planner wa miradi hii. Kwakuwa unafiki ndo unaowasukuma viongozi wetu sidhani kama hata kumtumia kupata consultation yake katika utekelezaji wa hii miradi kupo. kwa hali hii tusitarajie jipya unless ashuke malaika aje afutilie mbali hiki kizazi, zaidi zaidi tutegemee yaleyale ya "ABANA BASHOME"
 
MBUNGE AIOMBA SERIKALI KUONDOA KODI YA VIFAA VYA UJENZI KWA MKOA WA KAGERA KUTOKANA NA TETEMEKO

Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare ameiomba Serikali kuangalia uwezakano wa kuwaondolea kodi wananchi wa mkoa wa Kagera kwenye vifaa vya ujenzi kutokana na maafa waliyoyapata lilipotokea tetemeko la ardhi.

Lwakatare aliyasema hayo alipokuwa akichangia mjadala bungeni kuhusu mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa Taifa unaokusudiwa kutekelezwa na Serikali pamoja na mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya serikali kwa mwaka wa fedha 2017 / 2018, mjini Dodoma.

Picha na Edwin Mjwahuzi

 
ATHARI YA TETEMEKO LA ARDHI

Anaandika Mutalemwa Alex

Tunataka kujua kwanini serikali ya ccm inatuchukia hivi sisi wana Bukoba? Kwanini hela ya waanga na vifaa mpaka leo hatujui iko wapi? Iweje tunafungua akaunti ya maafa ya Bukoba na baada ya watu kuanza kupiga kelele kuhusu kutopewe hiyo misaada akaunti inabadirishwa jina kutoka Waanga wa Tetemeko kwenda Kamati ya mahafa Bukoba.. Je imechangwa kiasi gani na kiasi gani kimetumika kwa waanga wa tetemeko... Miundombinu serikali itumie kodi zetu nasio misaada ya waathirika wa tetemeko.. Period

Kwasasa tunaomba mvua isinyeshe kabisa maana hatuna pa kulala na nyumba zitaanguka

Geofray Kamugisha[emoji116] [emoji116]

Serikal hii hakika imeoza mtu kapigwa hasara kibao eti wao wanatoa mifuko mi5 ya cement ivi inaingia akilin kwel?. pongezi kwa mh Willbroad lwakatare kwa juhud zake za kuendelea kuwatetea wananch wa bk town

Flora Ngaiza[emoji116] [emoji116] [emoji116]

Kweli kabisa adi inasikitisha kwakweli mana dunia nzima imetoa mchango ajili ya wahanga wa tetemeko bk lakini kilichonishangaza nimekuta vijijini wanapewa sukari nusu kilo na mchele kilo 1 kweli kwa kila kaya na unakuta mtu anafamilia ya watu kuanzia 4 na kuendelea mh kweli serikali iliangalie ilo inasikitisha xna xna.
 
 
Hakuna lolote hapa,miaka mitano sio mingi mtakuja humu humu kumuuliza alichokifanya,lakini hili litakuwa fundisho na limeshakuwa fundisho kwa wapiga kura kukurupuka na kufanya maamuzi bila kuwaza mbele kutatokea nini,hii ni sawa tungemrudisha Mujuni Joseph Kataraia tungetegemea jipya gani katika yeye?ni mwak sasa hakuna mrejesho wowote?hakuna mkutano wowote?hakuna lililofanywa lolote na alikuwepo jimboni anazunguka na gari limejaa vijana tuache ushabiki wanabukoba mjini hatuitaji mtu wa kusemasema tu bungeni tunahitaji kiongozi/mbunge mwenye uthubutu ndani yakw sio kila kitu wewe uililie serikali bana
 
ANAANDIKA FAHAMI MATSAWILI


Bukoba haipaswi kuwa na njaa kuna sehemu kuna Tatizo.....

Wilaya ya Bukoba ni kati wilaya 8 zinazounda Mkoa wa kagera . kisiasa wilaya ya Bukoba imegawanyika katika majimbo mawili ya Ubunge, Bukoba Vijijini na Bukoba Mjini. Kiutawala Bukoba inaundwa na Halmashauri ya Bukoba Vijijini na Bukoba Mjini.

Katika Halmashauri ya Bukoba mjini shughuli ya kiuchumi ni Biashara, Uvuvi ziwa Victoria na Ujasiriamali.

Wapo wafanyabiashara wakubwa wana changamoto zao za kisera na kikodi ambazo ni muhimu kuzitazama kwa jicho la kuwandolea vikwazo.

Wapo wafanyabiashara ndogo ndogo na wajasiriamali kama boda boda, mama ntilie, machinga hawa nao wanazo changamoto kadhaa zikiwemo za mitaji, maeneo ya kufanyia biashara kutokuwa rafiki, kutotambuliwa rasmi..

kuna vijana wengi mfano. Fundi uashi, seremala, Fundi gereji, lakini tangu waanze kazi katika maeneo yao hawajawahi kufikiwa na viongozi wa kisiasa hivyo kwenye mipango na budget zinazopangwa bira shaka hawafikiliwi namna ya kuwanyanyua...

Wapo wananchi wanaojishughulisha na sekta ya uvuvi Wilaya Bukoba imepakana na ziwa Victoria wananchi wetu wanatumia fursa hiyo kuendesha shughuli za uvuvi.

Lakini bado wanakabiliana na changamoto kadhaa zikiwemo za kikodi, za mitaji, zana za uvuvi za kizamani, samaki kupungua ziwani, n.k

Lazima wananchi wetu wasaidiwe..

Eneo la ziwa Victoria, Ziwa ikimba na MTO Ngono, ni sehemu ambazo zina uwezekano mkubwa wa kufuga samaki wa kibiashara. Watu wanaweza kujiunga katika vikundi au wenye uwezo wanaweza kujenga mabwawa ya kufugia samaki. Kama viongozi wa kisasa watalihamasisha kwa weledi mzuri..

Halmashauri ya Bukoba Vijijini asilimia 85 ya wananchi hutegemea kilimo kuendesha maisha yao..

Wananchi wengi ni Wakulima wadogo wenye mashamba ya Wastani ya ukubwa wa hekta 1.5. Hivyo mabadiliko yoyote ya kuleta mapinduzi ya kilimo yanapaswa kuwa ni kubadilisha mashamba madogo kuwa ya kisasa...

Mazao yanayozalishwa ni pamoja na Maharage, Ndizi, kahawa, muhogo, viazi mviringo na chai.
Lazima tuweke mikakati madhubuti kuwasaidia wananchi hawa.

1. Kuwapatia Wakulima kanuni za kilimo bora kupitia kwa maafisa kilimo, mashirika binafsi kupitia semina ili wakulima wetu waweze kuzalisha kwa tija.

2. Kuanzishwe mashamba makubwa ya mfano ili kutoa Ushauri kwa wakulima kwa njia ya mashamba darasa, katika vikundi, mitandao ya wakulima na mkulima mmoja mmoja.

Matumizi Bora ya zana za kilimo. Halmashauri lazima inunue angalau trekta 20 kwa uchache kwa sababu halmashauri ina kata 29. Ili kuchochea kilimo cha kisasa na kuachana na kilimo cha mkono.

3. Uhimizaji wa matumizi ya mbolea kwa maana mbolea ya asili na viwandani kazi hii inaweza kufanyika kupitia mashamba darasa na vikundi vya ushauri...

Tunahitaji viwanda ili kuwa na uhakika wa mazao yetu lakini na viwanda vinahitaji uhakika wa malighafi za kutosha sio wa msimu mmoja hapa ipo kazi ya kufanya.
 
MCHORO WA STAND MPYA YA MABASI NA MALORI



Ujenzi wa stand pia ni kipaumbele namba moja. Kujua hatua zilizofikiwa rejea katika report ya mwezi post za nyuma kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…