View attachment 404994 LEO NIMEWASILISHA RIPOTI YA KIKAO NILICHOKIFANYA NA BAADHI YA WANA KAGERA WAISHIO JIJINI DAR ES SALAAM KWA MKUU WA MKOA KAGERA.
View attachment 405000 View attachment 405001 View attachment 405002 View attachment 405003 View attachment 405003 View attachment 405003 View attachment 405004
MH. MKUU WA MKOA,
KAGERA.
MAAZIMIO YALIYOPITISHWA KWENYE KIKAO KILICHOITISHWA NA MH. WILFRED LWAKARATE(MB), MBUNGE WA JIMBO LA BUKOBA MJINI, KUJADILI ATHARI ZA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA, KUONA JINSI YA KUSAIDIA WALIOPATWA NA MADHARA.TAREHE 18 SEPTEMBA, 2016 KWENYE HOTELI YA KEBBY'S, MWENGE, DAR ES SALAAM.
1. Kwa kauli moja kikao kimetambua na kuishukuru serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa hatua zakuridhisha kufuatia janga hili, ikiwa ni pamoja na ;
i. Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa, (Mb), Waziri Mkuu, pamoja na kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya upinzani bungeni Mh. Freeman Aikael Mbowe (Mb) kufika B ukoba mara moja kuona athari za tetemeko na kushiriki mazishi ya watu waliofariki kutokana na janga hili na pia kuwafariji waliojeruiwa na kuathirika kwa namna mbali mbali.
ii. Kuandaa mkutano wa kuishirikisha jumuiya ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini pamoja na jumuiya ya wafanyabiashara kwa lengo la kukusanya misaada kwa ajili ya kukabiliana na janga hili.
iii. K uandaa matembezi ya hisani kwa ajili ya kukusanya fedha za kusaidia nakukabiliana na madhara ya janga hili.
iv. Viongozi waandamizi mbali mbali waserikali, wakiwemo Mawaziri, Viongozi mbalimbali wa kisiasa, Makatibu wakuu na wakuu wa vitengo muhimu vinavyo husiana na maafa kufika kwenye eneo la tukio kwa haraka.
2. Kwa kauli moja kumuomba Mh. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa ndiye baba wa nchi, pamoja na shughuli zake nyingi, kutenga siku mapema itakavyo mpendeza kufika mkoani Kagera kuwapa pole wananchi wake kutokana na janga hili. Tunaamini walioathirika watafarijika sana kumuona Rais wao akiwa nao kwenye eneo la tukio.
4. Kwa kuwa janga hili la kitaifa halina itikadi ya siasa, dini, rangi, kabila wala ubaguzi wa aina yoyote ile, hivyo ushiriki wa watu wote ni muhimu sana.
5. Kwa kutambua ukweli wa walioathirika zaidi ni wananchi wa mkoa wa Kagera, inawapasa wao kuwa msitari wa mbele katika kushiriki katika juhudi zote zinazofanyika, kwa njia na jinsi yoyote inayowezekana, iwe ni kwa hali au mali, mshikamano wao katika janga hili ni muhimu sana. Mpaka sasa, imejidhihirisha kwamba ushiriki wa wana Kagera bado ni hafifu sana. Wana kagera wanahimizwa kutokukata tamaa nakuamsha hari ya kushirikiana katika kuusaidia mkoa wao kwa nidhamu ya hali ya juu . Ili kusisitiza umuhimu huo, mfano wa kwamba ili kuweza kupewa msaada wa usafiri (lift) ni lazima uwe njiani, unahusika.
6. Kwamba kutokana na mkoa wa Kagera kukumbwa na maafa makubwa na mengi mfululizo kuanzia miaka ya 1970 zilipoanza chokochoko za nduli Iddi Amini wa Uganda, vita vya Uganda , Ukimwi, mdudu wa migomba (ekiuka), madhara ya wakimbizi kutoka nchi jirani yaliyo leta ujambazi , kufa kwa Vyama vya Msingi vya Ushirika na Chama Kikuu cha Ushirika (BCU/ KCU) kulikoambatana na kuanguka kwa bei ya zao la kahawa, kuanguka kwa Shirika la Reli Tanzania (TRC), kulikosababisha bei za bidhaa za viwandani ambavyo vingi vipo Dar es salaam, kuwa juu kuliko sehemu nyingine yoyote ya Tanzania, ugonjwa wa mnyauko ambao umeangamiza kabisa migomba na zao lake ndizi, na sasa ni janga la tetemeko. Majanga hayo yote ni sababu kubwa kwa mkoa wa kagera kushuka sana kiuchumi kutoka kati ya mikoa mitatu tajiri miaka ya 70 - 80 hadi kuwa kati ya mikoa mitano masikini sana nchini. Serikali inaombwa ichukue hatua za makusudi kutoa upendeleo wa kisera wa kuusisimua upya uchumi (a stimulus package) kwa mkoa wa Kagera kwa kufanya yafuatayo :
i. Kutoa msamaa wa kodi zote kwenye bidhaa zote za ujenzi zinazouzwa mkoani Kagera kwa kipindi cha miaka kumi.
ii. K wa kutambua madhara ya mdororo wa uchumi wa mkoa wa Kagera kwa muda mrefu hivyo kuwepo tatizo kubwa la ajira na umasikini, miradi yote ya ujenzi wa miundombinu ya kijamii kama mashule, zahanati, vituo vya afya na majengo mengine ya serikali yatakayo jengwa upya au kukarabatiwa, ugawaji wa kandarasi ufanywe kwa mtindo wa uwezeshaji kwa makampuni yaliyopo na yanayoendesha shughuli zao mkoani kagera yenye uwezo, wakishirikiana na makampuni ya wana -Kagera walioko nje ya mkoa pale inapobidi . Vigezo vitaandaliwa ili vizingatiwe.
7. Kwa kutambua kuwa serikali imeunda kamati za maafa za Kitaifa na Mkoa ambapo Wabunge wa mkoa wa Kagera wameshirikishwa, ni vyema ushiriki kwenye kamati hizo upanuliwe na kuzijumuisha taasisi za dini ambazo mkoani kagera zimekuwa na mchango mkubwa katika utoaji wa huduma za jamii kwa miaka mingi. Hatua hii itasaidia kuongeza ufanisi katika zoezi zima la uthamini wa madhara, ukusanyaji wa taarifa na usambazaji wake. Aidha kwenye hizo kamati uwepo umuhimuwa ku wahusisha wataalam wa habari kuongeza ufanisi katika upashanaji wa habari .
8. Kwa kuzingatia mamlaka ya Mbunge anayopewa na katiba ya jamhuri ya Muungano wa T anzania, mifuko ya majimbo pia itumike kusaidia kwenye majanga yamaafa kama haya.
9. Kwa kukubali kwamba bado uitikiaji na ushiriki wa wana -Kagera bado ni hafifu sana, juhudi mpya zifanyike kwa kuishirikisha Serikali ya mkoa wa Kagera, Wabunge wote wa mkoa na viongozi wa dini zote kuitisha mkutano/ kusanyiko jingine haraka iwezekanavyo hapa dar es salaam kwa lengo la kuwashirikisha wana-Kagera na wadau wengine wote wenye mapenzi mema, katika kuonyesha kuguswa kwetu kama jamii na tatizo hili, tukusanye rasilimali kusaidia kwenye janga hili. Ndiyo njia pekee ya kuonyesha kuwa tunahitaji kupatiwa msaada wa usafiri (lift), hivyo ni vyema tukawa njiani.
NB : Katika kikao hicho cha wana kagera ahadi za jumla ya Tshs. 6,780,000/= zilitolewa na pesa taslimu Tshs. 1,480,000/= na kuleta jumla ya Tshs. 8,260,000/=
Sekretarieti iliyoundwa inaendelea kuratibu ukusanyaji wa michango hiyo ili itakapokamilika iwasilishwe sehemu husika.
Imewasilishwa leo tarehe 22/09/2016
Ofisi ya mkuu wa mkoa.
Wilfred Muganyizi Lwakatare (Mb)
Jimbo la Bukoba Mjini.
K. N.Y Wana Kagera wanaoishi Dar es Salaam (Waliohudhuria kikao hicho).
NAKALA KWA;
Mh. Waziri Mkuu.
Viongozi wakuu wa madhehebu ya kidini.
Viongozi wa vyama vya siasa.
Waheshimiwa wabunge wote wa mkoa Kagera.
Waandishi wa Habari.