NTARE II
Member
- Sep 14, 2016
- 36
- 25
![]()
Huo[emoji115] ni mwonekano wa ndani wa stand mpya ya mabasi itakayojengwa eneo la Kyakailabwa.
![]()
[emoji115] Mwonekano wa nje wa stand mpya ya mabasi ya kyakailabwa
![]()
Huo[emoji115] ni mwonekano wa ndani wa stand mpya ya mabasi itakayojengwa eneo la Kyakailabwa.
![]()
[emoji115] Mwonekano wa nje wa stand mpya ya mabasi ya kyakailabwa
Happiness Essau. Nakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya ya kutuhabarisha lakini pia kutukumbusha juu ya kile macho na masikio ya wanakagera wapenda maendeleo wangependa kukiona au kukisikia leo hii.
Kwa masikitiko makubwa inanilazimu niandike hapa asubuhi ya leo hii juu ya miradi tajwa katika mji wetu wa bukoba zikiwa zimebaki siku tano kutimia mwaka tangu wanabukoba walipoamua kufifisha sumu chuki na unafiki vilivyokuwa vimeanza jenga matabaka kutokana na sababu zisizo za msingi hasa ninazoweza ziita uchu wa madaraka.
wana bukoba waliamua kumpa kura Mh. Lwakatare kuwa na madiwani hasa wale waliowaamini kuwa wataweza kaa meza moja kujadili na kulisukuma gurudumu la maendeleo liende mbele hasa baada kuziona siasa zilizokwamisha mawazo na maono ya kuufanya mji wa bukoba ung'are.
Kinachonisikitisha ni ukimya wa wawakilishi wetu katika miradi ambayo kwa sasa imekuwa ndo inasubiriwa kwa hamu ianze kwakuwa inategemewa kuleta sura mpya ya mji wa bukoba. Mh. Mbunge hatoi mrejesho wa nini kinaendelea juu ya maandalizi na utekelezaji wa miradi hiyo.
Mbali na Mbunge tunaye Meya na naibu Meya tena mbao kwa bahati nzuri wote ni viongozi wanaotoka chama kimoja hivyo imani ya wana bukoba ni kubwa kwao kwakuwa hatutarajii msuguano wa kimasilahi katika kutekeleza miradi hiyo.
Swali langu hapa je wanabukoba waendelee kukibeba kimya hiki kwa kutaraji ule usemi wa kimya kingi kina mshindo? Je, kuna namna yoyote ya kuzuiliwa utekelezaji wa miradi hiyo na ndio sababu ya kuwa na kigugumizi kiasi hiki? Madiwani wetu mnaweza kutueleza lipi katika hili?
Mh. Mbunge na baraza zima la madiwani wa manispaa kwanza niseme nyinyi ni watu mna bahati sana na mshukuru sana kwakuwa mgogoro baina ya Mbunge na Meya waliopita umewanufaisha sana kwakuwa hata hiyo miradi tunayolilia kuona ikianza si mawazo bali mmekuta tayari watu walishaibuni na master za miradi hiyo zipo kazi yenu ilikuwa ni kuweka mambo kwenye msitari na kuanza utekelezaji wake.
Inasikitisha sana ukimya huu ambao hatuuelewi ni mgomo wa ndani kwa ndani au ndo yale yale kuwa mlipochaguliwa na kuaminiwa kazi yenu imekwisha?
Bukoba uchuguzi wa mwaka 2015 ndo ulifungua fursa maana wananchi walipata walichostahili lakini binafsi naona kama tumeingia chaka tena chaka baya watoto wa mjini kama wasemavyo watoto wa mjini.