Nashukuru kwa ufuatiliaji wa kila mmoja wetu na hamu ya kujua kinachoendelea. Mchakato wa kufanya formalities zote zinazotakiwa kisheria na kiutaratibu zinaendelea. Na kwa bahati mbaya taratibu za serikali yetu ni ndefu mno na zenye kujaa vikorikoro vingi. Tuko makini tutavuka na tutapeana taarifa ipasavyo
Sent from my TECNO-J8 using
JamiiForums mobile app
Mh. mbunge, pole na majukumu yako kwa ujumla. Nianze kwa kukushukuru walau kuja jukwaani kwa mara nyingine tena, na mara hii kusema kweli tuna mambo mchanganyiko lakini kuu kupita yote ni miradi mikubwa miwili, stand na soko kuu.
Kwa kuanza, tunakupongeza kwa kumpata huyu dada yetu Happy katika tushirikishane yetu, hakika huyu dada atakusaidia sana kufikia malengo yako kwa haraka endapo utampa ushirikiano ili naye akusaidie kupitia vipawa vyake alivyojaaliwa na muumba. Tumefurahi kuona ujenzi wa barabara ya mafumbo ukiwa unamuonekano mzuri kabisa, tumefurahi pia kuona ujenzi wa barabara ya n/housing ukiwa umeshika kasi na inshallah nao utakamilika vyema kabisa, kwa haya tunakupongeza sana na chini yako na mayor wako tunaamini manispaa inaweza kufanya mengine mengi zaidi na zaidi.
Kusema kweli ni furaha yetu sote, na kama tu unaweza walau kwenda kwa mwendo huu basi naamini wananchi watakuwa radhi tena na tena uendelee kuwepo, hatuna nongwa kwani kiu yetu kubwa ni kumpata mtu wa kuipendezesha upya Bukoba yetu ( kaitu kaila).
Jambo la pili ni jambo kuu, miradi. Tunakuomba kwa maombi yote ya kiasiri na kimungu utwambie, leo hii ofisi yako iko hatua gani. Ni vyema umesema ni "formalities" na mambo ya kiserikali yana mlolongo, sasa tueleza (nichwe bamoi). Leo mko hatua ipi haswa, najua mpaka miradi hii isimame kunaweza kuwa na hatua hata 10, sasa nyinyi leo mko hatua ya ngapi na inaendelea ama inaonesha kukwama? Huko serikalini ni nini tatizo?
Nasema hivi kwani naelewa, rais mwenyewe alishasema atakayetaka kumkwamisha kuhusu mipango ya maendeleo atambomoa, sasa hizo kona ni nani anaziweka tena kufifisha maendeleo ya wananchi? Huku mtaani pia, inasikika huu mradi umezuiwa kimakusudi na serikali kisa hapo ni kwa wapinzani, wewe hili umeliona, unalijua na linakuingia?
Mara ya mwisho taharifa iliyokuja hapa ilisema tayari UTT wameshakubali kutoa pesa, na kiasi kingine kutoka BMC. Na kwamba ilibaki ofisi ya BMC kushauliana na UTT kujenga soko la mda katika eneo lililo tayari, sasa haya yote baada ya kuwa yamefikiwa miezi 2 iliyopita leo tena mmefikia wapi? Mnafikiri hapo mlipo mtatokaje wakati mwingine pasipo kuhusisha wananchi ili kuchanga upya mawazo?
Hii miradi ni kipimo kwako mh. kwani kama manispaa iko chini yako na ramani na maeneo vyote vilishakuwepo ni wewe sasa kutuita wananchi kila mara ili tusaidiane, tushirikishane ili kuondoa baadhi ya mikwamo, sote tunahangaika kwa ajiri ya Bukoba mpya (a banana city).