TATHMINI YA MIEZI MITATU (3) YA HALI YA USHIRIKISHWAJI WA WAWANCHI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO TOKA KUANZA KWA MRADI WA "TUSHIRIKISHANE"
Hiyo[emoji115] ndio dira ya BMC. Dira hii mpk sasa imefanikiwa kwa 10% tu kwa kuwa na halmashauri na watendaji wa mitaa na kata.
Vinginevyo, ushiriki wa wananchi katika swala zima la maendeleo si wa kuridhisha. Wananchi hawafahamu kinachoendelea katika mipango na utekelezaji wa miradi yote ya manispaa na hawana jinsi ya kupata taarifa. Hii inatokana na kwamba;
-Website ya BMC inataarifa za 2012, idara ipo na inawatumishi kadhaa wengine wana masters.
-Meya hana kurasa za mitandao ya kijamii kama JF, fb, twitter, IG ambayo angeweza itumia kutoa taarifa
-Naibu meya kwa kurasa zake zote hakuna haongelei chochote cha Bkb au Nshambya ambayo ni kata yake. Anatumia kurasa zake kuongelea mambo mengine ya kitaifa.
-Mbunge kama taasisi ana ukurasa maalum fb lkn anapost mara chache sana kwa kadirio la mara moja kwa miezi miwili au hata zaidi. Mipango, utekelezaji na ahadi haviko katika ukurasa wake.
-Mkurugenzi wa manispaa ni mgeni. Lakini pia watendaji wengine wa BMC kama wakuu wa idara hawaongelei chochote popote na sheria haziwaruhusu
-Mkanasha huu wa JF ulilenga kusaidia mbunge na katibu wake pamoja na halmashaufi kujibu maswali na kuwapa mwelekeo wa halmashauri wananchi lkn bado haujatumika ipasavyo.
-Ukurasa wa katibu wa mbunge katika mitandao ya kijamii pia hauna msaada kwa yeyote anayetaka taarifa.
-Ukifika manispaa kupata taarifa yeyote unaambiwa uandike barua kwa mkurugenzi kwanza ili idara ziruhusiwe kutoa taarifa. Hivyo njii hii si rahisi sana kwakua inakua na mlolongo mrefu
-Viongozi hawajaweza kutumia radio zetu na Tv kuelezea chochote kuhusu BMC, maendeleo n.k
-Kuna njia zilipendekezwa kwenye warsha ya "Tushiikishane" za namna ya kuwafikishia wananchi taarifa kama kuandaa namba maalumu na kutuma jumbe fupi kupitia simu, bado hazijafanyiwa kazi
Katika kata kadhaa nilizopita kufatilia maendeleo ya mradi wa Tushirikishane, watendaji wake wote hawajawahi sikia kuhusu mradi, hawafahamu hatua zilizofikiwa katika ujenzi wa soko kuu na stand, mtendaji wa Nyaga tu ndo alikua anafahamu kuh ujenzi wa stand. Mahojiano mbali mbali niliyofanya na wananchi wa kawaida, wengi hawafahamu chochote. Nilifanikiwa kuhoji hata bodaboda wa pale nje ya ofisi za manispaa nao hawafahamu chochote
Aidha, ninampongeza na kumshukuru Mh. mbunge pamoja na halmashauri, wameahidi kulifanyia kazi swala hili kwa haraka sana. Na kwa kuanza wameahidi kuwa baraza la madiwani litakua likirushwa moja kwa moja katika radio zetu na Tv ili wananchi wengi zaidi waweze kufikiwa na taarifa. Hii ni habari njema sana[emoji120]
Bukoba Kazi, Amani na Maendeleo!