Mradi wa Tushirikishane (
JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane") umeanza rasmi jimbo la Bukoba mjini chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Mbunge
Wilfred Lwakatare.
Tokana na misingi ya TUSHIRIKISHANE iliyoelemea katika kuwawezesha wabunge wa kuchaguliwa kutekeleza ahadi 4 kati ya jumla ya ahadi walizotoa wakati wa uchaguzi kwa urahisi kwa kushirikiana na wananchi; mada hii itatumika kuwasilisha, kujadili na kupeana taarifa ya kile kinachojiri Bukoba mjini.
Ahadi walizochagua kufuatilia wananchi wa Bukoba mjini kwenye mradi wa TUSHIRIKISHANE
a. Ujenzi wa soko kuu la Bukoba, soko la Kashai na Stendi kuu ya mabasi Bukoba
b. Mikopo ya vikundi vya kijasiriamali vya akina mama na vijana
c. Urasimishaji wa makazi
d. Bima za afya kwa wananchi angalau
View attachment 389799
Meya wa Manisapaa ya Bukoba, Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini na Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media wakisaini makubaliano ya kushiriki katika utekelezaji wa Mradi wa Tushirikishane
Mada hii itatumika zaidi na Wana Bukoba kutupa taarifa.
Baadhi ya Washiriki watakuwa:-
1. Mh. Mbunge
Wilfred Lwakatare
2. Katibu
Alex Xavery (Katibu)
3.
Happiness Essau (Afisa habari Bukoba)
4. Chief Karumuna (Mayor wa Bukoba)
5. Jimmy Kalugendo (Naibu Mayor)
6. Na washiriki wote wa Warsha hiyo na wale wote wenye mapenzi ya Maendeleo ya Bukoba mjini.
Karibuni...
[HASHTAG]#Tushirikishane[/HASHTAG] [HASHTAG]#Bukoba[/HASHTAG]
Kufahamu majimbo mengine yenye mradi huu tembelea -
JamiiForums yazindua rasmi mradi wa "Tushirikishane"
======
UPDATE: 1st December, 2016.
Waendeshajinwa mradi wa [HASHTAG]#TUSHIRIKISHANE[/HASHTAG]. Wanawaalika wana tushirikishane katika kikao chetu kwa pamoja kinachotarajiwa kufanyika mnamo tarehe 02/12/2016 katika ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa Bukoba kuanzia saa nane za mchana.
Ufunguzi rasmi wa kikao utaanza saa tisa kamili bila kujali idadi ya wajumbe.
Kuwahi ni muhimu sana, kuhudhuria kwako ndiyo mafanikio ya taarifa nyeti za halmashauri kuwafikia wananchi moja kwa moja.
Mchango wako wa maoni, maswali, na hoja mbalimbali ndiyo chachu ya maendeleo ya jimbo letu.
Kumbuka wewe ni mwakilishi wa mamia, nao wanakutegemea bila kujua, tenda haki na Mungu atakulipa kwa namna yake.
Njooni tupate kujua miradi yetu imepiga hatua kwa kiwango gani mpaka sasa.
Waweza kukili kuhudhuria kwako kwa msg fupi kwenda namba 0765 82 92 56.
Taarifa hii mfikishie na mwenzio.
Asanteni sana na Mungu awabariki.
Ki msingi nikitazama mikakati ya "tuijenge bukoba yetu" ninachokiona zaidi ni mipango ya kuboresha baadhi ya miundo mbinu iliyoko katika mkoa wa kagera.
bado sijapata picha tunawezaje
Ndugu Wananchi na wadau wa Bukoba Mjini na Kagera; leo nimepata fursa ya kuuliza swali ambalo limetuumiza vichwa wengi kuhusiana na mkoa wetu kuwa kati ya mikoa mitano maskini Tanzania kwa 39% ikizingatiwa kuwa mkoa wa Kagera una historia ya kuwa mkoa tajiri pamoja na Mbeya na Dar es Salaam miaka ya 1960 mpaka tulipokumbwa na vita ya Kagera-Uganda ambayo mpaka leo serikali haijawapa wananchi fidia iliyotolewa na Serikali ya Uganda.
Lakini pia mkoa wetu ulikuwa na shirika la BCU(Bukoba Cooperative Union) ambalo liliweza hata kuikopesha serikali. Leo hii hata Chama cha Ushirika KCU kimesambaratika kwa sababu za kisiasa.
Lakini pia, inatuwia vigumu kiziamini takwimu hizi. Je ni baadhi ya wilaya zenye umaskini au ni Kagera nzima?
Je, serikali imetuwekaje katika Mpango wa Matokeo Makubwa (BRN) ili kurudisha hadhi ya mkoa wa Kagera?
Yafuatayo ni Majibu ya Naibu waziri wa Fedha na Mipango Mh Kijachi.
-Vigezo vilivyotumika katika kubainisha umaskini ni uwezo wa kaya kukidhi mahitaji ya msingi; chakula, mavazi na malazi. Utafiti wa 2011/2012 mkoa wa kagera una kiwango cha 39% ya umaskini.
Ifuatayo ni mipango ya serikali katika kuinua uchumi wa Kagera:
1.Kuendeleza maeneo yenye fursa za uwekezaji na viwanda vidogo na vya kati.kwa kuboresha miundombinu.
3. Serikali inahamasisha wananchi kuzitumia fursa na rasilimali zilizopo ili za kuwapatia kipato.
4.Serikali inaboresha upatikanaji wa pembejeo na masoko ya mazao na uvuvi yanayozalishwa na wananchi.
5. serikali ina mpango wa kuendeleza viwanda vya nyama ili kuendeleza sekta ya ufugaji.
7. Serikali iko mbioni kufufua viwanda vya nguo. Haswa mkoa wa Kagera.
8. Serikali mwezi Disemba itaanza utekelezaji wa kujenga reli ya kati kwa kiwango cha geji kuelekea Mikoa ya Magharibi ikiwemo Kagera ili kufungua fursa za uchumi.
NITUMIE FURSA HII KUWAAMSHA WAZAWA WA KAGERA WALIOKO NDANI NA NJE YA NCHI, KURUDI NA TUIJENGE BUKOBA KWA PAMOJA.
"Mkataa kwao, ni mtumwa."
Imetolewa na:
Mh Wilfred Lwakatare
Mb.Bukoba Mjini.
Ni jambo la kupongeza pale wana kagera wanapojaribu kutumia utandawazi kutafakari maendeleo ya kagera.
sioni sababu ya kubishana na Takwimu zinazoonyesha kuwa mkoa wa kagera ni miongoni mwa mikoa 5 masikini Tanzania.
ki msingi mimi binafsi kwa kutumia macho ya juu juu naweza kusema jambo hili linawezekana kuwa ni ukweli kwa kutumia vigezo vifuatavyo.
1. najaribu kujiuliza wahaya wanazalisha nini? jibu la haraka ni ndizi na kahawa.
leo hii ukitembea mkoa wa kagera ukitizama familia moja baada ya nyingine migomba imekumbwa na ugonjwa, haistawi tena. migomba imegeuka mimea ya historia kwa maana wahaya wanajisikia fahari kuzungukwa na shamba lenye mimea hii lakini mingi haitoi matunda ambayo ni ndizi. pale mtu anapolima shamba halitoi mazao ndugu zangu huu ndio umasikini wenyewe.
kilimo cha kahawa hakina mvuto katika maisha ya kisasa. kahawa zinachukua mda mrefu kuanza kutoa matunda lakini ukipiga mahesabu mtu akilima shamba la kahawa ambazo msimu wake ni mmoja kwa mwaka je ili kwa maisha ya sasa mtu apate wastani wa laki 3 kwa mwezi ambazo ni milioni 3 na laki sita kwa mwaka je mtu huyu inabidi auze gunia ngapi za kahawa kwa msimu? je kuvuna kiasi hiki cha kahawa ni shamba la ukubwa kiasia gani na matunzo yake yakoje? kwa kifupi kilimo cha kahawa kimekosa mvuto kwa viajana kwa maana hakiwapi matumaini ya kupata maisha yanayoendana na wakati. kahawa zimebaki kwenye mashamba ya asili ya wazee na baadhi ya wastaafu au watu wanaoishi mijini wenye ziada ya kuwekeza katika mashamba mapya.
kama migomba inakufa, vijana hawajishughulishi na kilimo cha kahawa hivi kagera leo hii shughuli zao za kiuchumi ni zipi? ki msingi umasikini umeingia katika mkoa wa kagera. si wakati wa kuvaa suti na kufunga tai kujifanya hakuna tatizo lolote, tukibishia takwimu bali kukaa chini takatafakari hivi kagera inaelekea wapi?
nikiangalia mikakati inayotajwa ya tuijenge kagera yetu imejikita katika kujenga masoko, stendi ya mabasi, kurasimisha makazi, haya ni muhimu kwa ajili ya kuboresha maisha ya wakazi wa kagera lakini tujiulize hivi tukifanya haya tu kweli umasikini huu tunaoambiwa utaondoka?
nijambo lililo wazi leo kuwa wana kagera wengi vijijini ama wanafanya shughuli za kujikimu tu, kutunza mashamba ya migomba ambayo yanasubiri msimu wa mahindi na maharage, kulima viazi na mihogo kwa ajili ya kujikimu. lakini pia kutokana na wana kagera wengi kuishi nje ya kagera wanavijiji wengi wanaishi kwa ruzuku kutoka kwa ndugu zao.
tunapowaza maendeleo ya kagera ambayo ni endelevu ni vema tuwaze mambo ambayo yatafanya uzalishaji katika mkoa wa kagera kuongezeka kwa ajili ya wanakagera na pia kuuza nje ya kagera, ni vema kuwaza mbinu za kuongeza mzunguko wa pesa ndani ya wanakagera walioko kagera na ni vema kuwaza mbinu za kuongeza ubora wa maisha katika kagera.
mkoa wa kagera ni moja ya mikoa yenye rutuba nzuri, hali nzuri ya hewa, misimu miwili ya mvua kwa mwaka. kwa hili tu kunafursa pana sana ya kutumia kilimo kuikomboa kagera.
kwa kuongezea katika yale yaliyokwisha semwa kama mikakati ya kuinua kagera nadhani kuna haja ya kupanua wigo kwa kuongeza mengine kama haya na kila mmoja mwenye wazo awe anachangia ili mwisho kamati itachambua yale yanayofaa.
1. uwepo mkakati wa kuinua shughuli za kilimo katika mkoa wa kagera kwa ajili ya kuuza nje ya kagera ili kuinua uchumi wa kagera. Sijui kama KCU na Chama cha ushirika cha karagwe vinahusika na kahawa tu au vina wigo unaoawawezesha kuwaendeleza wakulima mkoani kagera kwa kuangalia ni mazao gani yenye tija kulingana na hali ya hewa ya kagera na kuwaunganisha wakulima kulima mazao hayo, kuwatafutia masoko nje ya kagera.
hii inajumuisha kuondoa kutumia sheria vibaya kukandamiza wakulima, mfano jambo lolote linaloweza kupata soko kuuzwa nchi jirani kutokea mkoa kagera ni ruksa na sheria zitumike kuweka mazingira mazuri ya biashara hiyo lakini sijasema kutoa bidhaa huko kuleta kagera hilo linahitaji tafakari kwanza.
mazao mengi yanastawi mkoa wa kagera yakiwemo matunda mbalimbali, ufugaji wa kuku na kadhalika hivyo vyama vya ushirika vinaweza kufungua masoko katika mikoa mbalimbali na kuwawezesha wakulima hawa kuungana na kuuza mazao yao katika mikoa mbalimbali ndani ya nchi.
vyama vya ushirika vinaweza kutafuta masoko ya mazao mbalmbali nje ya nchi na ikiwezekana kuwaunganisha wakulima katika kuomba tax exemptions katika exports.
yapo masoko tunaambiwa nchi yetu inaruhusiwa kuuza mazao ya kilimo bila ushuru kama marekani lakini ni vigumu kwa mkulima mmoja mmoja kuyafuatilia masoko haya. ni wakati sasa vyama vya ushirika kuwaunganisha wakulima na kuanza kuyafuatilia masoko hayo. Kilicho cha msingi ni wakulima wawe na chombo kinachowaunganisha kutazama kilimo kibiashara na kuanza kuwajengea tamaduni za kulima kibiashara kuendana na soko.
2. utalihi katika mkoa wa kagera.
tunaposema utalihi wengi wanawaza wazungu kutoka ulaya kuja kagera lakini nadhani tabia kama ya wachaga ya kwenda nyumbani wakati wa sikukuu ni mojawapo ya aina ya utalii wa ndani. wana kagera wanaweza kukopa tabia hii kwa wenzetu kwa maana ina tija kubwa sana kiuchumi katika mkoa wa kagera. ukijenga tamaduni ya wana kagera kurudu nyumbani katika wakati fulani katika mwaka na wakati huo kuwahasisha wakati wa kurudi nyumba wabebe fedha tu wasibebe bidhaa, hawa watakuwa kama watalii katika mkoa wao wanaoingiza fedha katika mzunguko wa fedha katika mkoa wa kagera.
3. ubora wa mkazi na mandhari katika mkoa wa kagera
ingawa mikakati inaonyesha upo mpango wa kurasishimisha makazi lakini ni lazima tutambue makazi yalisiyo na mpangilio ni tatizo kubwa katika mkoa wa kagera. ni vema kuweka sheria za makazi katika miji na vijiji, kuweka mkakati wa kuboresha makazi ili yafikie viwango vilivyoweka katika sheria kwa kutazama wajibu wa vyombo vya wananchi na wajibu wa wananchi wenyewe kila mmoja akihamasishwa kutimiza wajibu wake. ubora wa makazi sio lazima yawe magorofa marefu au ubora wa mji sio magorofa marefu bali ni kuwa na mpangilio unaoeleweka, nyumba zikawekwa katika hali ya unadhifu haijalishi ni hali ya kipato ya mwenye nyumba. katia sheria za makazi angalau kiwanja kiwekewe ukubwa wa chini na wa juu kwa mijini, iwe ni lazima kila kiwanja kuwa na barabara ili hata kama serikali imeshindwa kupangilia makazi lakini wanachi wenyewe kwa kushirikiana na serikali za mitaa na sheria za makazi wajiwekee mpangilio wa makazi. Sio huu ujenzi holela tunafanya, kila mtu anajenga anavyojisikia, leo hii ukitazama ujenzi unavyoendelea katika milima iliyozunguka bukoba, nyumba hazifikiki kwa barabara mpaka unajiuliza hivi haya tunayanya katika ulimwengu huu wa leo? wazazi wetu huko nyumba walikuwa wanatengeneza miji mitaa inaeleweka, nyumba kama zimepangwa kwenye mistari kwa kamba katikati kuna barabara. leo hii watu wanaojiona wanajua kuliko watu wa zamani tunafanya upuuzi mtupu. na kibaya serikali zetu zinakuja eti kurasimisha makazi hayo yaliyoholela.