TAARIFA YA KIKAO CHA TATHMINI YA MAENDELEO YA MRADI WA TUSHIRIKISHANE KILICHOKAA TAREHE 2 DECEMBER, 2016 KATIKA UKUMBI WA MANISPAA BUKOBA
Kikao kilihudhuriwa na Meya, Mbunge, Naibu Meya, Afisa Habari wa Jamiiforums, Katibu wa Mbunge, Waandishi wa Habari na Wananchi wa jimbo la Bukoba. Mstahiki Meya alitoa taarifa ya maendeleo ya vipaumbele vyote vinne vya mradi, kuanzia August mpk October) ambayo ipo hapa katika mkanasha (rejea taarifa ya August - October). Aidha, mstahiki meya aligusia hatua mpya zilizofikiwa katika zoezi la urasimishaji makazi na kupatikana kwa vyeti vya tathmin ya kimazingira ya mradi wa soko kuu, soko la Kashai na stand mpya.
Hivyo, zifuatazo ni hatua zilizokua zimefikiwa katika vipaumbele vya mradi hadi mwisho wa mwezi November.
1. Ujenzi wa Soko Kuu
Halmashauri ya Manispaa imefanikiwa kupata barua ya awali ya mkopo kutoka TIB Development Bank. Katika hatua ya sasa Halmashauri inaendelea na jitihada za kukamilishaji masharti ya mkopo ikiwa ni pamoja na kukamilisha andiko la mradi. Halmashauri imemuajiri Mshauri-mwelekezi aitwaye OGM consultant kwa ada ya TZS 50 milioni kukamilisha andiko.
Pia halmashauri itatakiwa kuchangia asilimia 30 ya ghalama za mradi kama mubia
Kukamilishwa kwa masharti ya TIB Bank kutawezesha mradi kuendelea na hatua inayofuata ambapo zabuni ya ujenzi itatangazwa.
2. Ujenzi wa Stand
Mradi huu bado uko katika hatua za awali. Halmashauri inafikiri kukaribisha wawekezaji wadogo ambao watajenga sehemu zao za biashara kwa mkataba. Mipango itakapokamilika, Meya atatangaza kwaajili ya watu kuomba mnamo December, 2016.
3. Ujenzi wa Soko la Kashai
Kama ilivyo katika mradi wa Stand Kuu, mradi wa ujenzi wa soko la Kashai bado uko katika hatua za awali. World Bank watafadhili ujenzi wa soko hili
4. Mikopo kwa Wanawake na Vijana
zoezi hili limekua gumu kutokana na urasimu uliopo katika SACCOS mpaka kupelekea madiwani kuomba Mikopo itolewe kwa mkurugenzi jambo ambalo limeonekana kukwama kwasababu ya changamoto za ukusanyaji rejesho la mikopo na kuwa ni kukiuka taratibu za serikali. Utaratibu mzuri wa kutoa mikopo kupitia SACCOS unawekwa
5. Urasimishaji Makazi
-Mtaa wa Mtoni na Nyakanyasi kata Bakoba nyumba 1000 tayari zimepata mchoro ambao umeshapitishwa na kamati ya Mipango Miji na Mazingira na kupelekwa wizarani kwaajili ya taratibu nyingine za kupata namba za viwanja
-Kata ya Miembeni eneo lote la mtaa wa Nyamkazi lenye nyumba 284 limeshapata mchoro na umekwishakupitishwa katika kamati ya Mipango Miji na Mazingira
-Kata kahororo vimefanyika vikao katika mtaa wa Kyaga na tayari zimekwisha kusanywa shilling million 7 kwaajili ya zoezi la urasimishaji makazi
-Zoezi la uchukuaji data (mipaka ya viwanja kwaajili ya mchoro wa TP) linaendelea Kashai
5. Bima ya Afya
Zoezi hili halijaanza kama tulivyokua tumekubaliana kwasababu si agenda kuu katika halmashauri. Bima ya afya imekua haiongelewi katika vikao vya baraza, haizungumziwi pia katika mikutano ya kisiasa. Aidha kuna mpango wa kitaifa wa kutoa bima ya afya kupitia halmashauri.
Utekelezaji wa kipaumbele hiki kama tulivyokua tumekubaliana katika kikao ilikua ni ofisi ya Meya, Mbunge, Idara ya Maendeleo ya Jamii na Idara ya Afya kwa kushirikia na Wagani kuandaa mikutano ya kata na kualika mashirika mbalimbali yanayotoa bima ya afya kwa gharama nafuu katika kata zote ili kutoa elimu, kuhamasisha na kuunganisha wananchi katika bima ya afya
Aidha, kakao hicho kilitumika pia kuelimisha viongozi juu ya umuhimu wa kutoa taarifa na kushirikisha wananchi katika maswala yote ya maendeleo kwa maana taarifa si mali yao bali ni mali ya wananchi. Viongozi walielimishwa pia juu ya njia mbali mbali za kisasa za kuwafikishia taarifa wananchi ili kuachana na mifumo na njia za kizamani ambazo kwa zama hizi zimepoteza tija sana.