TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

Tutabakia hivi hivi tu na barabara za vumbi majengo ya mkoloni sokochoo stendivumbi wenyemji wakifurahia miji ya wengine na wakiiendeleza huku wakijisifia
Inasikitisha sana mkuu, hatuna cha kujivunia. Tumezidiwa hadi na Kahama.
 
MWONEKANO WA BARABARA ZA BUKOBA, JANUARY 2017

9b9153239171646ea9090c791dccf079.jpg
28ae585684e1d8e7a2103bd3f9f0a9a1.jpg
9c2cecc5993a10037f5818e88bd30abe.jpg
b7c25918c43f5a6c8f1adee5a84d20a7.jpg
70f02501c13d82eb1928cda39a717240.jpg
660503cfea791e54991eb71d241102e8.jpg
 
Inasikitisha sana mkuu barabara kama vile kijiji au
Mji Wa bukoba hata hauna hata daladala za mjini mpaka daladala za wilayani zifanya kazi hiyo nimeshuhudia Leo daladala za mutukula kamachumu na muleba wakifanya biashara hiyo kabla kwanza vyao yaani wahaya matajiri na mashomire tunashindwaje Kununua daladala hata moja mil 200 wakati wahaya wanafanya sherehe za harusi za kifahari mpaka mil400 wahaya tubadilike vinginevyo mwafaaaaaa
 
Nimekuwa Bukoba kwa wiki tatu ila ajabu sijaona mradi mkubwa wa maana unaotekelezwa, mbunge wetu na madiwani sijui wamekwama wapi au ni sarakasi za serikali kuu kwasababu ya Halmashauri kuwa chini ya upinzani!! Inasikitisha sana. Twafaa
Binafsi napenda mawazo na matendo yaliyo ya maana na kasi kutoka kwa Lwakatare na wenzie lakini kwa mwendo huu ni wehu tu ...kama suala ni kuendelea na wapinzani basi kocha abadirishe timu. Kuendelea na Lwakatare ni wehu. Alishachoka na amechoka kiakili kitambo sana. Sikutegemea ku flop kiasi hiki kwa Lwakatare, huu ni wehu. Kama CDM haimuandai mtu mwingine mwenye akili na aliye vocal kwa ajiri ya 2020 basi na Lwakatare wasimrudishe kwetu kwani ni wehu. Kama wanampenda sana Lwakatare wampeleke huko Kilimanjaro wampe jumbo huko huko, huu ni wehu
 
Mji Wa bud hata hauna hata daladala za mjini mpaka daladala za wilayani zifanya kazi hiyo nimeshuhudia Leo daladala za mutukula kamachumu na muleba wakifanya biashara hiyo kabla kwanza vyao yaani wahaya matajiri na mashomire tunashindwaje Kununua daladala hata moja mil 200 wakati wahaya wanafanya sherehe za harusi za kifahari mpaka mil400 wahaya tubadilike vinginevyo mwafaaaaaa
Hawashindwi kwasababu hawana pesa, na suala la kuwa na dala dala za trip za mjini si suala la tajiri, ni suala la wataalamu wa hapo manispaa,hao nao ni majipu tu hamna kitu. Hawana ubunifu japo wengi wao ni magraduates
 
Binafsi napenda mawazo na matendo yaliyo ya maana na kasi kutoka kwa Lwakatare na wenzie lakini kwa mwendo huu ni wehu tu ...kama suala ni kuendelea na wapinzani basi kocha abadirishe timu. Kuendelea na Lwakatare ni wehu. Alishachoka na amechoka kiakili kitambo sana. Sikutegemea ku flop kiasi hiki kwa Lwakatare, huu ni wehu. Kama CDM haimuandai mtu mwingine mwenye akili na aliye vocal kwa ajiri ya 2020 basi na Lwakatare wasimrudishe kwetu kwani ni wehu. Kama wanampenda sana Lwakatare wampeleke huko Kilimanjaro wampe jumbo huko huko, huu ni wehu
Nina wasiwasi na u-kada wako. Tukiweka siasa pembeni huwezi kuhukumu kazi ya mtu kwa mwaka mmoja hasa kwa miradi mikubwa. Hata Rais bado anajipanga kutekeleza sera ya viwanda. Kama vipi tupe mbunge ambaye ameonyesha vitu vikubwa vinavyoshikika ndani ya mwaka mmoja.
 
Hawashindwi kwasababu hawana pesa, na suala la kuwa na dala dala za trip za mjini si suala la tajiri, ni suala la wataalamu wa hapo manispaa,hao nao ni majipu tu hamna kitu. Hawana ubunifu japo wengi wao ni magraduates
Shida za hapo manispaa wengi si wenyeji na wana hulka ya kuchukia wenyeji Wa mkoa sijui kama wana nia yoyote ya kuendelaza mji huu.sisi wenyewe ndo wakujiogarnize na kuleta kero zote za mji na kuzitatua wenyewe ukiona imefikia hatua tunaambiwa tubebe misalaba yetu twafaa ujue serikali haina nia yoyote ya kuendeleza mkoa huu
 
Binafsi napenda mawazo na matendo yaliyo ya maana na kasi kutoka kwa Lwakatare na wenzie lakini kwa mwendo huu ni wehu tu ...kama suala ni kuendelea na wapinzani basi kocha abadirishe timu. Kuendelea na Lwakatare ni wehu. Alishachoka na amechoka kiakili kitambo sana. Sikutegemea ku flop kiasi hiki kwa Lwakatare, huu ni wehu. Kama CDM haimuandai mtu mwingine mwenye akili na aliye vocal kwa ajiri ya 2020 basi na Lwakatare wasimrudishe kwetu kwani ni wehu. Kama wanampenda sana Lwakatare wampeleke huko Kilimanjaro wampe jumbo huko huko, huu ni wehu

Ni kweli usemacho mkuu, Nilisema mapema kuwa Lwakatare hawezi kutusaidia na hayupo kutusaidia zaidi ya familia yake. Alikuwa ameshachoka sana kimwili na kiakili, tulihitaji mbunge shupavu na wa kujitoa. Tumuombe Mungu tufike salama.
 
Happiness Essau huu mzunguko hivi hakuna namna ya kuufanya ukawa wa kuvutia kwa bustani nzuri? Au tunasubiria msaada wa wahisani!! Kama maua yapo, maji ya kutosha,samadi ipo sasa kwanini tusipambe kamji ketu japo kamechoka?
9c2cecc5993a10037f5818e88bd30abe.jpg
Bila shaka wameiona na kuichukua hoja yako wataifanyia kazi ndugu Chachu Ombara. Niwakumbushe tu kuwa mbunge, naibu meya na katibu wa mbunge wamo humu.
 
Nimekuwa Bukoba kwa wiki tatu ila ajabu sijaona mradi mkubwa wa maana unaotekelezwa, mbunge wetu na madiwani sijui wamekwama wapi au ni sarakasi za serikali kuu kwasababu ya Halmashauri kuwa chini ya upinzani!! Inasikitisha sana. Twafaa
Bukoba tujilaumu kwa upofu wetu kuendelea kuchagua watu kwa majina na ushabiki wa kiitikadi bila kujali ni mustakabari maisha ya sasa na vizazi vijavyo. Tunawachagua wachumia tumbo sio wapenda maendeleo.
 
KAGERA TUNATOKAJE HAPA ...?
Mkoa Wa Kagera Tunahitaji Mikakati Imara ya kutuvusha. safari yetu bado ni Ndefu Sana....Tulipotoka, Tulipo na Tunakoelekea.........
Kabla ya Tetemeko la Ardhi mkoa Wa kagera lilotuachia Majeraha
Miezi 2 kabla ya Tetemeko la Ardhi. ilitoka Ripoti iliyoonesha Mkoa wa kagera kuwa miongoni mwa mikoa 3 Maskini Nchini.......
Ilikuwa ni ishara ya kutuamsha sisi Wananchi na viongozi wetu Wa kisiasa na watendaji kujitathimini wapi tumejikwaa na kuibua Mijadala ya kimaendeleo.......

Bahati mbaya hilo lilipita kama mengine yanavyopita likaja na tetemeko la Ardhi likajadiliwa kama mengine yaliyopita........

Kila aliyeongea maneno 10 kuanzia wananchi Wa kawaida hadi viongozi Wa kisiasa hakuna hata neno moja liloelekeza nini kifanyike (way forward, solution) zaidi ilikuwa ni kuadithia historia ya tatizo na kulalamika basi.....

Je ni kweli mkoa Wa kagera tulipaswa kuwa miongoni mwa mikoa 3 maskini nchini. Huenda ni Umaskini wetu ndio unatufanya kutegemea misaada kujenga choo, nyumba, jiko vilivyobomoka kutokana na tetemeko la Ardhi......

Hapa tatizo la msingi ni Umaskini wetu kagera ndio Tatizo......swali kwa nini sisi ni maskini na Tunatokaje kwenye kadhia hili ya Umaskini???

Mkoa Wa kagera Unaundwa na wilaya 8 kiutawala..

Wananchi wengi 85% Wanajishughulisha na kilimo. Kilimo cha biashara na chakula... Hivyo wananchi wengi ni Wakulima wadogo wenye mashamba ya wastani Wa hekta 1.5

Zao kuu la biashara ni kahawa na Ndizi baadhi ya Maeneo. Zao la kahawa linakabiliwa na changamoto nyingi zikiwezo za msululu Wa kodi karibu kodi 26 kwenye zao la kahawa ambazo mh Rais ameagiza ziondolewe,

Zana duni zinazotumiwa na wakulima Wa kahawa, Udhaifu Wa chama cha Ushirika kinachosimamia zao kahawa......

Zamani zao la kahawa liliwawezesha wakulima hawa wazee wetu kusomesha watoto wao kuendesha maisha yao baada ya mauzo lakini sasa hivi hali ni tofauti.......

Wapo wafugaji wakubwa na wadogo Wa kibiashara na kilimo...

Wapo Wavuvi wadogo na wakati katika ziwa Victoria, ziwa ikimba na mto Ngono......bado nao wanakabiliwa na changamoto ya zana za kizamani za kuvuli kama mitumbwi, nyavu..Uvuvi haramu unaopelekea samaki kupungua haraka..

Wapo Wafanyabiashara wadogo na wakubwa....Wa mazao ya kilimo na vifaa vya madukani...

Wapo wajasiriamali wadogo ( boda boda, machinga, mama ntilie, Fundi Uashi, Ujenzi, Gereji, Seremala, fundi wa ushonaji n.k hawa nao wanazo changamoto zao nyingi....

kwanza kutorasmishwa kazi zao hivyo kwenye Sera na mipango hawajadiliwi kuhusu changamoto ya mitaji, maeneo rafiki ya kufanyia biashara na kazi zao na masuala ya kodi kwao..........

Tunatokaje hapa hilo ndilo la msingi....

1. Halmashauri zetu zote lazima zibuni vyanzo vipya vya Uzalishaji hasa vile vyanzo vyenye chani ya Uzalishaji ili kutoa Ajira kwa vijana na kuongezea Mapato Halmashauri zetu..mfano Halmashauri ya Bukoba Vijijini Kuna Ziwa ikimba na MTO Ngono Tunaweza kuyatumia maeneo haya kuvutia kilimo cha Mpunga kwa kutoa mikopo maalum kwa ajili ya project hiyo au kilimo cha miwa halmashauri ikaingia Uwekezaji Wa Ubia au join venture ili kuwekeza kiwanda cha kati cha kuzalisha sukari angalau Tani 20 kwa siku......tutazalisha ajira na kuongeza mapato ya halmashauri...

2. Halmashauri zote zirasmishe shughuli za hawa wajasiriamali ili waingizwe kwenye mipango ya kibudget na mazingira rafiki ya kufanyia kazi...hawa watu wakichangamka na biashara yao kuchanganya watalipa kodi kwenye halmashauri zetu hivyo tutaongeza mapato......

3. Hivyo mabadiliko yoyote ya kuleta Mapinduzi ya kilimo kagera yanapaswa kuwa ni ya kubadilisha Mashamba Mashamba kuwa ya kisasa hivyo ni muhimu kila Halmashauri kuwa na trekta za kukodisha wakulima kwa gharama nafuuu ili kubadili kilimo cha jembe la mkono kwenda kilimo cha kisasa...

4. Kuwapatia wakulima Elimu ya kilimo bora kupitia kwa Maafisa kilimo, mashirika binafsi kwa njia ya semina au shamba darasa kwa mashamba ya mifano ya kilimo.......

Pia itolewe elimu ya kulima mazao mbadala kama Alzeti, na Mtama ni mazao yanayoweza kustawi maeneo mengi mkoa Wa kagera. Kuhimiza kupanda miti na kutolima kwenye vyanzo vya maji ili kupunguza sababu za kibinadamu zinazochangia mabadiriko ya tabia ya nchi na kupelekea Ukame maeneo mengi.....

5. Kuanzishwe mfumo Maalum Wa kukopesha wananchi maskini Mifugo kama Ng'ombe baada ya kuzaa anarudisha Ndama jike ili kukopa wengine. Utaratibu huu ulikuwepo katika mkoa Wa kagera miaka 90 chini ya shirika moja kutoka nchini Sweden... Mfumo huu uliwasaidia sana wananchi maskini katika mkoa wetu Wa kagera kwa kuwakopa mifugo hasa mbuzi na Ng'ombe....

6. Sekta ya Uvuvi bado hatujaitendea haki tuna fursa ya kujenga mabwawa makubwa ya samaki tukapata samaki Wa kutosha kwa ajili ya biashara kupitia project za halmashauri au mikopo maalum kwa ajili uwekezaji Wa ufugaji Wa samaki Wa mabwawa lakini wavuvi vijana ni muhimu kupatiwa mikopo ya nyavu zile zinazoruhusiwa na serikali na mitumbwi ya kisasa inayotumia mashine badala ya mashine za kizamani za makasia hivyo vijana watapanuka kimtaji na halmashauri zetu zitaongeza mapato pia....

7. Kila mwanasiasa anayeiongelea mkoa Wa kagera kati ya Maneno 10 angalau maneno 4 yawe ya kuonesha njia ya nini kifanyike kila sekta (way forward, solution)......tunguze blaa blaa wananchi wanaumia.....

8. Huduma za kijamii bado sio za kuridhisha jitihada zinahitajika Elimu, Afya. Mfano katika manispaa ya Bukoba mjini Elimu. Wilaya ya Bukoba mjini matokeo ya kidato cha nne 2015 . Bukoba mjini ina shule 26 zilizofanya mtihani kidato cha 4 jumla ya Wanafunzi 2218 division 1 =186=8%
Division 11=301=14% division 111=362=16%
Division iv =919=41%
Division O =450=20%
Lazima mbunge Wa bukoba mjini na halmashauri wawe na mikakati maalum kuhakikisha kiwango cha ufaulu kwa hawa watoto Wa mamantilie, watoto Wa machinga, Fundi selemara na bodaboda watoto wao wanafaulu ili waje kuzisaidia familia zao....

Huduma ya Afya bado sijaona mikakati ya wanasiasa na halmashauri za kuhamasisha wananchi kujiunga kwenye bima za Afya ili kupunguza kiasi kikubwa cha fedha wanachotumia kupata huduma ya Afya.......

9. Ni muhimu kila jimbo kuwa na kombe la mpira na baadae kuwa na kombe la mkoa Wa kagera hii itasaidia kuibua vipaji vya vijana kila jimbo hadi mkoa tutauza wachezaji wetu kwenye timu za kitaifa....tunaweza kumtaka kila mbunge agharamie kombe la jimbo na fainali za mkoa zikasimamiwa na ofisi ya mkuu Wa mkoa.....

10. Ni muhimu kuunganisha rasirimali watu Wa mkoa Wa kagera ambao wengi wao wana ukwasi mkubwa lakini wanaishi nje ya mkoa Wa kagera tunahitaji uwekezaji wa viwanda vidogo vidogo na vya kati lazima fursa za mkoa Wa kagera zitangazwe kwa kiasi cha kutosha....

Kila kiongozi kuanzia ngazi ya serikali ya mtaa, Diwani na mbunge lazima wawe na mpango mkakati strategic plan ya eneo lake la uongozi na namna anavyoshirikisha wananchi na fursa ya rasirimali watu wenye uwezo kufanikisha plan hizo za kiuchumi na kijamii.

Credit: Fahami Matsawili
 
HISTORIA YA KANISA LA CATHOLIC JIMBO LA BUKOBA KWA UFUPI

Maaskofu wa kwanza hadi Timanywa

89bf85530eb8d76ac759eb3598b69334.jpg
46cdc95eb1902962fcb4db8fb44a4ccc.jpg


Walipadrishwa mpaka kufikia 1998
89411bd2e457d0b1311d7b48ab60b67d.jpg
034ff02daab017256e77ddf050d4364b.jpg
3fb0a84ef47473469592be7ae97bf873.jpg
72c8791675c02504f07350c216805a9a.jpg
77167982f80286e6d1b695e7531ff7e5.jpg


-Ramadhan Kingi
 
KATIKA HISTORIA NA MZEE RAMADHANI KINGI

Kutoka kulia Marehemu Mzee Hassan Goronga kiongozi wa Tanganyika Fedration of Labour Jimbo la Ziwa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere TANU na wa mwisho kushoto ni mama Goronga. Nimeiweka picha hii kama kutoa picha halisi ya Jimbo la Ziwa ambalo sasa ni Kagera ili "bali igulu" wasiendelee kuubeza Mkoa wa Kagera kama wanavyotaka! Lazima Mkoa upewe heshima yake hasa katika harakati za kuutafuta Uhuru wa nchi hii!

eb6168b3e135aeb008ee3138caf87455.jpg


Sio siri TANU haikuwa name chochote iliwategemea wanaharakati wake
Je kuna kumbukumbu gani kumhusu Mzee Rweikiza ? Huyu aliitoa nyumba yake ya kudumu iwe Ofisi ya TANU hadi Leo IPO!
Mhindi Shah na Patel kuitoa nyumba yao ya ghorofa kuwa ofisi ya TANU hadi Leo waliomo hawajui kama walipewa bure jengo hilo miaka ya 1966!
 
Asante kwa kumbukumbu, Kumbe Goronga naye ana kahistoria kadogo. Nilizoea kupita pale kwake nikielekea shule Tumaina SM.
 
TAARIFA YA KIKAO CHA TATHMINI YA MAENDELEO YA MRADI WA TUSHIRIKISHANE KILICHOKAA TAREHE 2 DECEMBER, 2016 KATIKA UKUMBI WA MANISPAA BUKOBA

Kikao kilihudhuriwa na Meya, Mbunge, Naibu Meya, Afisa Habari wa Jamiiforums, Katibu wa Mbunge, Waandishi wa Habari na Wananchi wa jimbo la Bukoba. Mstahiki Meya alitoa taarifa ya maendeleo ya vipaumbele vyote vinne vya mradi, kuanzia August mpk October) ambayo ipo hapa katika mkanasha (rejea taarifa ya August - October). Aidha, mstahiki meya aligusia hatua mpya zilizofikiwa katika zoezi la urasimishaji makazi na kupatikana kwa vyeti vya tathmin ya kimazingira ya mradi wa soko kuu, soko la Kashai na stand mpya.

Hivyo, zifuatazo ni hatua zilizokua zimefikiwa katika vipaumbele vya mradi hadi mwisho wa mwezi November.

1. Ujenzi wa Soko Kuu

Halmashauri ya Manispaa imefanikiwa kupata barua ya awali ya mkopo kutoka TIB Development Bank. Katika hatua ya sasa Halmashauri inaendelea na jitihada za kukamilishaji masharti ya mkopo ikiwa ni pamoja na kukamilisha andiko la mradi. Halmashauri imemuajiri Mshauri-mwelekezi aitwaye OGM consultant kwa ada ya TZS 50 milioni kukamilisha andiko.

Pia halmashauri itatakiwa kuchangia asilimia 30 ya ghalama za mradi kama mubia

Kukamilishwa kwa masharti ya TIB Bank kutawezesha mradi kuendelea na hatua inayofuata ambapo zabuni ya ujenzi itatangazwa.

2. Ujenzi wa Stand

Mradi huu bado uko katika hatua za awali. Halmashauri inafikiri kukaribisha wawekezaji wadogo ambao watajenga sehemu zao za biashara kwa mkataba. Mipango itakapokamilika, Meya atatangaza kwaajili ya watu kuomba mnamo December, 2016.

3. Ujenzi wa Soko la Kashai

Kama ilivyo katika mradi wa Stand Kuu, mradi wa ujenzi wa soko la Kashai bado uko katika hatua za awali. World Bank watafadhili ujenzi wa soko hili



4. Mikopo kwa Wanawake na Vijana

zoezi hili limekua gumu kutokana na urasimu uliopo katika SACCOS mpaka kupelekea madiwani kuomba Mikopo itolewe kwa mkurugenzi jambo ambalo limeonekana kukwama kwasababu ya changamoto za ukusanyaji rejesho la mikopo na kuwa ni kukiuka taratibu za serikali. Utaratibu mzuri wa kutoa mikopo kupitia SACCOS unawekwa


5. Urasimishaji Makazi

-Mtaa wa Mtoni na Nyakanyasi kata Bakoba nyumba 1000 tayari zimepata mchoro ambao umeshapitishwa na kamati ya Mipango Miji na Mazingira na kupelekwa wizarani kwaajili ya taratibu nyingine za kupata namba za viwanja

-Kata ya Miembeni eneo lote la mtaa wa Nyamkazi lenye nyumba 284 limeshapata mchoro na umekwishakupitishwa katika kamati ya Mipango Miji na Mazingira

-Kata kahororo vimefanyika vikao katika mtaa wa Kyaga na tayari zimekwisha kusanywa shilling million 7 kwaajili ya zoezi la urasimishaji makazi

-Zoezi la uchukuaji data (mipaka ya viwanja kwaajili ya mchoro wa TP) linaendelea Kashai


5. Bima ya Afya

Zoezi hili halijaanza kama tulivyokua tumekubaliana kwasababu si agenda kuu katika halmashauri. Bima ya afya imekua haiongelewi katika vikao vya baraza, haizungumziwi pia katika mikutano ya kisiasa. Aidha kuna mpango wa kitaifa wa kutoa bima ya afya kupitia halmashauri.

Utekelezaji wa kipaumbele hiki kama tulivyokua tumekubaliana katika kikao ilikua ni ofisi ya Meya, Mbunge, Idara ya Maendeleo ya Jamii na Idara ya Afya kwa kushirikia na Wagani kuandaa mikutano ya kata na kualika mashirika mbalimbali yanayotoa bima ya afya kwa gharama nafuu katika kata zote ili kutoa elimu, kuhamasisha na kuunganisha wananchi katika bima ya afya

Aidha, kakao hicho kilitumika pia kuelimisha viongozi juu ya umuhimu wa kutoa taarifa na kushirikisha wananchi katika maswala yote ya maendeleo kwa maana taarifa si mali yao bali ni mali ya wananchi. Viongozi walielimishwa pia juu ya njia mbali mbali za kisasa za kuwafikishia taarifa wananchi ili kuachana na mifumo na njia za kizamani ambazo kwa zama hizi zimepoteza tija sana.

ab78276185bb620a8d428e4e8b68fd5f.jpg
d147894313cff9f9d076881094b12e21.jpg
7f974e5047c43d0b5b4aee7218e1a5bb.jpg
a1ca4cd4be865b7a5377187290e2ec42.jpg
2eadabc5ca0db407ca20d3ade2e0eb96.jpg
33a18be176f03e3e1e164fbab3071afe.jpg
d67238de5416a6a59cd1680abe55899c.jpg
08c4755b851b314dfd3ffd884b3ebfb0.jpg
 
Back
Top Bottom