KUTELEKEZWA KWA SOKO LA BUGASHANI - BUHEMBE
099611a83668304ea4228251.jpg[/IMG]
Soko hili lilizinduliwa rasmi mwaka 2012 lakini mpaka sasa miaka minne baadaye halijaweza kutumika hivyo kupelekea kuwa gofu.
Ujenzi wa soko ulitokana na mapendekezo ya wananchi katika vikao vya mitaa na kata, lakini wananchi hawa wa Buhembe wameshindwa kutumia soko hilo kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo usalama wa mali zao kwakua soko liko wazi pande zote na halina milango. Kero ya mvua pia imekua sababu ya wananchi wa Buhembe kutokutumia soko lao kwakua mvua zinaingia ndani pamoja na kukosekana kwa umeme.
Kutokana na hali hiyo, wafanyabiashara wamelazimika kujenga vibanda nje ya soko hilo kama inavyoonekana kwenye picha. Lakini pia wengine wameendeleza sehemu ya barabarani na kutengeza soko lisilo rasmi na hivyo kusababisha mvutano kati yao na watendaji wa mitaa na kata na halmashauri kwa ujumla.
Ili kuweza kutumia soko lao, wananchi wa Buhembe wameiomba halmashauri kuboresha hali ya soko hilo kwa kuweka kuta ili mvua isiingie na milango kwaajili ya usalama wa mali zao ombi ambalo halijaweza kushughulikiwa ndani ya miaka minne. Katika bajeti ya 2016/2017 pia kero ya soko hili haijazingatiwa.
Kama soko hili lingeendelezwa lingeweza kuhudumia sehemu kubwa ya kata Nshambya na Kahororo, kata yote ya Buhembe na Nyakato. Lingeweza pia kuhudiaa Bukoba vijijini na baadhi ya sehemu za Missenyi. Lakini pia lingekua fursa kubwa ya kiuchumi kwa wa watu wa ukanda huo kutokana na uwepo wa Chuo Kikuu cha Josia Kibirah maeneo jirani, Chuo cha ualimu Nkindo, shule za Mugeza, Ihyungo, Nyakato, Steven ambazo ni bweni na nyingine kadhaa. Lingeweza kusaidia kukuza biashara kwa upande huo na kupanua mji haraka zaidi.
Kwahivyo, Soko la Bugashani lililoko kata ya Buhembe ni RASILIMALI MFU nyingine katika manispaa ya Bukoba