TAARIFA YA MRADI DECEMBER, 2016
Utangulizi
Tushirikishane ni mradi unaowahusisha viongozi wa kuchaguliwa (mbunge na madiwani) serikali (halmashauri) na wananchi katika kurahisisha upatikanaji wa maendeleo. Wadau wakuu wa mradi huu ni Halmashauri ambayo ndiyo kitovu cha mipango ya maendeleo na utekelezaji wake, Mbunge ambaye ni msimamizi wa serikali (halmashauri), Jamiiforums ambao ni wasimamizi wa mradi na Wananchi.
Utekelezaji wa mradi unaanzia Halmashauri ambayo inasimamia miradi yote na inayotokana na vipaumbele vyetu ambavyo ni (1) Ujenzi wa Stand Kuu ya Mabasi, ujenzi wa Soko la Kuu na Soko la Kashai (2) Urasimishaji Makazi (3) Mikopo kwa Wanawake na Vijana, na (4) Bima ya Afya. Pia inatoa taarifa kwa kila hatua inayofikiwa katika vipaumbele vyote. Mbunge katika mradi ni daraja kati ya manispaa na wananchi katika kuweka msukumo wa utekelezaji na kutoa taarifa kwa wananchi. Halmashauri na mbunge wanawajibika moja kwa moja kwa wananchi. Jamiiforums ni mfatiliaji wa shughuli zote za mradi (utekelezaji wa vipaumbele) inatoa taarifa kwa wananchi juu ya mradi
TATHMINI YA MRADI YA MIEZI MITANO (5)
Mafanikio
(i)Utekelezaji wa mradi ulianza kwa changamoto ya upatikanani wa taarifa, awali ofisi ya mbunge na mbunge kwa ujumla hawakuwa wakielewa wajibu wao katika mradi hivyo ushirikiano wao haukua wa kuridhisha hivyo kusababisha ugumu katika kupata taarifa. Baada ya miezi mine (4) ya utekelezaji wa mradi, ofisi ya mbunge na mbunge walielewa wajibu wao na kuweza kushiriki vyema katika kutoa taarifa ya mradi
(ii)Swala la halmashauri kutoa taarifa kwa wananchi ni mtambuka na mradi umekua ukisisitizo hilo kwamaana ya kwamba taarifa ni mali ya wananchi hivyo inapasa ziwafikie ili waweze kushiriki. Lakini pia, ushirikishwaji wa wanannchi katika maswala ya maendeleo yao ni dira ya halmashauri ya manispaa ya Bukoba. Mradi umejitahidi kuwaelimisha viongozi wa halmashauri ikiwemo na mbunge juu ya swala hili na kuna mafanikio yameanza kuonekana mfano;
(iii)Mbunge na naibu meya wameanza kutoa taarifa mbalimbali na kuongelea maswala yanayohusu manispaa kupitia akaunti zao za facebook
(iv)Mbunge ameahidi kufanya mkutano kwa kila mwezi kwa kualika vyombo vya habari ili kutoa taarifa
(v)Mbunge ameahidi kuhakikisha kila kikao cha baraza la madiwani kuwa kinatangazwa katika vyombo vya habari na magari ya matangazo ili wanachi wafahamu na kuhudhuria
(vi)Mbunge ameahidi pia kuwa kila kikao cha baraza la madiwani kitakua kikieushwa katika televishen ya Bukoba (Bukoba Cable Network) ili wananchi ambao hawataweza kuhudhuria kikao hicho waweze kufahamu nini kinaendelea
(vii)Ushiriki na ufatiliaji wa wananchi wa mradi huu unazidi kuongezeka, mfano nisipoweka taarifa katika mkanasha kwa muda kadhaa watu wanaulizia sababu za kufanya hivyo. Na pia idadi ya watu wanaochangia na hata kupitia mkanasha wetu imekua ikiongezeka
(viii)Viongozi wamefahamu kuwa wananchi wanauwezo na nafasi ya kuwahoji kupitia mradi huu
(ix)Mkutano wa BUMUDECO 2017 ni moja ya mafanikio ya mradi pia
Changamoto
(i)Bado kunachangamoto ya meya wa manispaa kukubali mradi vyema na kushiriki vyema hasa katika swala la taarifa
(ii)Msukumo na ushawishi wa mbunge kwa halmashauri katika utekelezaji wa vipaumbele bado hauridhishi
(iii)Viongozi wa kuchaguliwa halmashauri ya manispaa ya Bukoba ni waonga wa kuongea na wananchi kwanjia ambazo ni rafiki na zinafikika kwa wengi kama mitandao ya kijamii. Mfano, kuna ambao wako kwenye magroup ya WhatsApp lakini hawawezi kueleza wala kujibu chochote. Tunao mkanasha wetu maalum wa Jamiiforums lakini wameshindwa kuutumia kuzungumza na wananchi waliowachagua. Viongozi wengine hawafahamu kabisa wala hawatumii mitandao ya kijamii
(iv)Njia za utoaji taarifa kwa wananchi bado ni za kizamani, haziendani na kasi ya teknolojia iliyopo. Mfano ni website ya halmashauri ambayo imetoa taarifa kwa mara ya mwisho 2012
TAARIFA
1. Ujenzi wa Soko Kuu
Matarajio katika ujenzi wa soko ilikua mpaka kufikia Disemba zabuni iwe imetangazwa na mshindi ametangazwa tayari. Pia tulitarajia kuwa wafanyabiashara wawe tayari wamehamishiwa katika soko la muda ili kupisha ujenzi. Ila haijawa kama matarajio yalivyokua kwa maana hata mazungumzo na muwekezaji hayajakamilika bado kwa maana bado andiko halijakamilishwa kutokana na halmashauri kushinwa kulipa ile million 50 iliyoitajika na mshauri OGM ili kukamilisha andiko. Lakini pia mbia na namna ya kupata 30% ya pesa inayotakiwa kutolewa na halmashauri bado haijafahamika
2. Ujenzi wa Stand
Bado taratibu zinafanywa ili kukaribisha wawekezaji wadogo wadogo kujenga kwa kufuata ramani na kwa mkataba maalum na halmashauri. Matarajio ilikua zoezi hilo litangazwe Disemba hii
3. Ujenzi wa Soko la Kashai
World Bank wamekubali kufadhili ujenzi wa soko hili. Matarajio ilikua ni zabuni kuwa imetangazwa na mzabuni kupatikana ifikapo kabla ya kuisha Disemba hii, lakini bado mabo hayo hayajafanyika
4. Mikopo kwa Wanawake na Vijana
Vijana na wanawake wanaendelea kupata mikopo katika SACCOS zilizoainishwa
5. Urasimishaji Makazi
Zaidi ya nyumba 1300 zimekwisha pata mchoro toka mradi uanze na zoezi la uchukuaji data (mipaka ya viwanja kwaajili ya mchoro wa TP) na kuhamasisha uchangiaji linaendelea
6. Bima ya Afya
Zoezi hili limekwama kwasababu mbunge hajaelekeza, kuhimiza halmashauri jinsi rahisi ambayo tulikubalia katika utekelezaji wa hili zoezi. Lakini kwa muda uliobaki inawezekana kufikia malengo kama litafanyika
HITIMISHO
Utekelezaji wa vipaumbele vingi umekua ukisuasua lakini bado kuna muda wa kufikia malengo kama kutakua na jitihada za ziada katika kufanikisha yote.
Imetolewa na
Afisa Habari - Bukoba[/QUOTE