TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

Watu Wa kyebitembe na nshambya na migera wamefikia hatua ya kuomba hiace ya safari za bk to mtukula iwasafirishe asubuhi wakienda town na wanalipa 500 tu kutoka kyebitembe wakati kwa bodaboda unalipa 1000 SAA nyingine 1500 kwenda town na ile daladala inafanya Mara mbili au tatu asubuhi kabla ya kuanza safari zake na anapiga hela kama mnaona kazi nunua daladala 5 tu zinatosha kama majaribio waone kama watakosa watu wakusafiri maana usafiri Wa bodaboda ni mgumu na unatozo kubwa tunaomba manispaa ifanyie kazi hilo halmashauri itakosaje kuwahimiza watu kuwekeza katika biashara hiyo au watafute milioni 200 kwa ajili ya hilo swala linaonekana do go lakini linaweza ingizia halmashauri kipato na kuongeza ufanisi Wa kuleta maendeleo
Shukran ndugu, hii nimeifahamu leo. Kyabitembe hapaendeki, miundombinu iko katika hali mbaya sana@
 
Kama unataka kufahamu vizuri cheki pale mbele ya kamzunguko ka kisoda pale karibia na one way asubuhi utaona daladala ikishusha watu pale
 
NDIZI BUKOBA; FURSA YA BIASHARA KWA MBEYA NA IRINGA

Leo nimeenda soko la Mabibo na jamaa yangu. Soko Zima hakuna Ndizi za Bukoba Sokoni nilipoulizia ndizi bukoba nikaoneshwa ndizi za Mbeya wao wanauza ndizi za mbeya kwa jina la Ndizi bukoba nilipowabana wakaniambia ukweli kuwa hizi ndizi za Mbeya ila Tunauza kwa kuwaambia wateja wetu kuwa ni Ndizi bukoba...Wanachofanya wafanya biashara Wanauza Ndizi za Mbeya kwa Mgongo wa Jina la Ndizi Bukoba.....Then Unanambia Bukoba ni Maskini kumbe kuna watu wanatumia jina la bukoba kuingiza kipato....Bukoba ndizi zimetoweka karagwe, Muleba, Tanzania iliwategemea ..hivi Zao la Ndizi limekumbwa na Ugonjwa Wa MNYAUKO kama Ukimwi kwa binadamu hautibiki kweli????

-Mastawil Fahamy
Ukivuka mipaka ukaingia Uganda utashangaa migomba inanawili. Iweje km150 zilete tofauti kiasi hicho angali ni aina moja ya kijiografia? Wataalamu wenu wamewahi kwenda Uganda ama mkawashauri waende kujifunza huko?
 
Mwisho wa siku maneno matupu hayatouvunja mfupa, matendo yatahukumu yenyewe, asante kwa mnaokuja na idea za kipi kifanyike kwa sababu inaonyesha mnajielewa na mnaelewa kuwa maendeleo ni jukumu la kila mtu na sio mchezo wa ngoja tuone kama atatoboa.

Siasa zinaendelea lakini siasa za maji taka zilikoma baada ya uchaguzi kuwaibua washindi na washindwa.

Hatua za miradi mikubwa ya ujenzi zinaendelea vizuri sana japo kwa umakini na wakati mwingine kimya kimya kukwepa masnitch wasitibue, tuendelee kuomba uzima muda sio mrefu moshi utaanza kufuka kwa mbali kuashiria moto kuwaka.

Wenye mioyo safi na nia njema kwa jimbo la Bukoba mjini tuendelee kushirikiana na kuleta hoja za kujenga na si majungu, fitna na vijembe.

Shiriki kwa vitendo kuhamasisha maendeleo ya jimbo lako sio porojo tu za kuufurahisha umma, maneno matupu hayatouvunja mfupa.

Alamsiki
Sasa kama vitu vinakwenda kwa usiri hawa wananchi mliowaambia kila wakati kushirikishana na kupeana taarifa itakuwaje? Mnawafanyaje kwanza kumaliza kiu yao ya kupata habari na pili kuwaamini kwamba kweli uko mafichoni mliko mambo hayajakwama bali yanaendelea?
 
Kwa idadi ya pikipiki zilizopo mjini na ufinyu wa mji wa bukoba kuweka daladala unajipigisha. Mpaka mji upanuke
Mie nafikiri wewe kama ni mhusika basi usaidie tu kutoa vibari vya njia hizo na watu wafanye biashara. Atakayeona inalipa ataendelea na atakayeshindwa atajitoa mwenyewe ijapo siamini katika kushindwa. Daladala inashindwaje kufanya kazi wakati abiria wapo wa kutosha kiasi hicho?

Kuendelea kufikiri eti hailipi ni kuwakwamisha raia kufikia mahitaji yao, liache soko liamue. Vinginevyo ni yale yale baadhi ya watoa maamuzi kuendelea kuwa sehemu ya matatizo yaayowakabili wananchi, msifanye hivyo bwana waacheni wenye pesa waweke daladala zao mjini.

Hivi huu mji wa bukoba ni mdogo kwa lipi? Ama bado unataka mtu asafiri kwa mguu tokea
1. Itahwa - Rwamishenye?,
2. Kashura - Kashai?,
3. Kahororo - Rwamishenye?
4. Kibeta - Mafumbo?
5. Rwamishenye - Nyakanyasi?
6. Buyekera - Bugabo?
Ni kwanini maeneo haya msianzishe routes?

Kwanini mnataka kuwatesa wananchi eti kisa hamuamini kama inawezekana? Wekeni njia zote za usafiri iwe mjini ama pembezoni na suala la nani atumie nini libakie kuwa chaguo la abiria, msiingilie na kuhujumu uhuru wao.

Ni wakati wa kuruhusu mawazo na fursa mbali mbali kwenye mji wetu, kuendelea na mawazo ya kuudogosha mji wetu ndo kuendelea kuubana zaidi ili usikue na hilo halitakiwi tena. Hii hofu ya nini na inatoka wapi?
 
Hii sijaielewa vizuri, kwani kuna wafanya biashara wameomba kufanya bishara katika hizo njia wamekataliwa!!? Au ni kipi kinaendelea hapo make mwenyewe silielewi vizuri hili japo nitalifuatilia kwa pande zote mbili, mamlaka na wafanya biashara
 
Wapendwa, ndugu Alex Xavery ndiye katibu wa Mbunge. Hii ndiyo sababu anajibu hoja zenu humu kwa niaba ya mbunge
 
Kuna ishu nimeiweka hapo juu kuhusu study tour Uganda juu ya kilimo cha migomba, tutaomba ufafanuzi
 
Hii sijaielewa vizuri, kwani kuna wafanya biashara wameomba kufanya bishara katika hizo njia wamekataliwa!!? Au ni kipi kinaendelea hapo make mwenyewe silielewi vizuri hili japo nitalifuatilia kwa pande zote mbili, mamlaka na wafanya biashara

Mkuu tunajaribu kuona ni kwanini hatuna usafiri wa hivi na wakati abiria wapo karibu kila hizo ruti. Na hii ni kutokana na madai ya mdau mmoja aliyekerwa na kukosekana kwa daladala mjini Bukoba. Yawezekena kukawa hakujawa na waombaji, namaanisha (wamiliki) lakini kwa vile abiria tayari wapo na wanateseka basi nyie kama uongozi wa manispaa mnaweza mkaona njia ya kuzungumza na wamiliki wa daladala ama kupitia chama chao ili waone haja ya kuanza kutoa huduma hiyo.

Na siamini kwamba uhitaji haupo, na pia siamini kabisa kwamba abiria hawapo, hivyo lichukueni na msaidie vikao vyenu vitoe baraka ili abiria wasaidike. Ukisoma michango ya Alex wajina wako hapo juu utaona kabisa wananchi wanaumia kwa kukosa daladala ruti za ndani ya mji
 
TAARIFA YA MRADI DECEMBER, 2016

Utangulizi

Tushirikishane ni mradi unaowahusisha viongozi wa kuchaguliwa (mbunge na madiwani) serikali (halmashauri) na wananchi katika kurahisisha upatikanaji wa maendeleo. Wadau wakuu wa mradi huu ni Halmashauri ambayo ndiyo kitovu cha mipango ya maendeleo na utekelezaji wake, Mbunge ambaye ni msimamizi wa serikali (halmashauri), Jamiiforums ambao ni wasimamizi wa mradi na Wananchi.

Utekelezaji wa mradi unaanzia Halmashauri ambayo inasimamia miradi yote na inayotokana na vipaumbele vyetu ambavyo ni (1) Ujenzi wa Stand Kuu ya Mabasi, ujenzi wa Soko la Kuu na Soko la Kashai (2) Urasimishaji Makazi (3) Mikopo kwa Wanawake na Vijana, na (4) Bima ya Afya. Pia inatoa taarifa kwa kila hatua inayofikiwa katika vipaumbele vyote. Mbunge katika mradi ni daraja kati ya manispaa na wananchi katika kuweka msukumo wa utekelezaji na kutoa taarifa kwa wananchi. Halmashauri na mbunge wanawajibika moja kwa moja kwa wananchi. Jamiiforums ni mfatiliaji wa shughuli zote za mradi (utekelezaji wa vipaumbele) inatoa taarifa kwa wananchi juu ya mradi

TATHMINI YA MRADI YA MIEZI MITANO (5)

Mafanikio

(i)Utekelezaji wa mradi ulianza kwa changamoto ya upatikanani wa taarifa, awali ofisi ya mbunge na mbunge kwa ujumla hawakuwa wakielewa wajibu wao katika mradi hivyo ushirikiano wao haukua wa kuridhisha hivyo kusababisha ugumu katika kupata taarifa. Baada ya miezi mine (4) ya utekelezaji wa mradi, ofisi ya mbunge na mbunge walielewa wajibu wao na kuweza kushiriki vyema katika kutoa taarifa ya mradi

(ii)Swala la halmashauri kutoa taarifa kwa wananchi ni mtambuka na mradi umekua ukisisitizo hilo kwamaana ya kwamba taarifa ni mali ya wananchi hivyo inapasa ziwafikie ili waweze kushiriki. Lakini pia, ushirikishwaji wa wanannchi katika maswala ya maendeleo yao ni dira ya halmashauri ya manispaa ya Bukoba. Mradi umejitahidi kuwaelimisha viongozi wa halmashauri ikiwemo na mbunge juu ya swala hili na kuna mafanikio yameanza kuonekana mfano;

(iii)Mbunge na naibu meya wameanza kutoa taarifa mbalimbali na kuongelea maswala yanayohusu manispaa kupitia akaunti zao za facebook

(iv)Mbunge ameahidi kufanya mkutano kwa kila mwezi kwa kualika vyombo vya habari ili kutoa taarifa

(v)Mbunge ameahidi kuhakikisha kila kikao cha baraza la madiwani kuwa kinatangazwa katika vyombo vya habari na magari ya matangazo ili wanachi wafahamu na kuhudhuria

(vi)Mbunge ameahidi pia kuwa kila kikao cha baraza la madiwani kitakua kikieushwa katika televishen ya Bukoba (Bukoba Cable Network) ili wananchi ambao hawataweza kuhudhuria kikao hicho waweze kufahamu nini kinaendelea

(vii)Ushiriki na ufatiliaji wa wananchi wa mradi huu unazidi kuongezeka, mfano nisipoweka taarifa katika mkanasha kwa muda kadhaa watu wanaulizia sababu za kufanya hivyo. Na pia idadi ya watu wanaochangia na hata kupitia mkanasha wetu imekua ikiongezeka

(viii)Viongozi wamefahamu kuwa wananchi wanauwezo na nafasi ya kuwahoji kupitia mradi huu

(ix)Mkutano wa BUMUDECO 2017 ni moja ya mafanikio ya mradi pia

Changamoto

(i)Bado kunachangamoto ya meya wa manispaa kukubali mradi vyema na kushiriki vyema hasa katika swala la taarifa

(ii)Msukumo na ushawishi wa mbunge kwa halmashauri katika utekelezaji wa vipaumbele bado hauridhishi

(iii)Viongozi wa kuchaguliwa halmashauri ya manispaa ya Bukoba ni waonga wa kuongea na wananchi kwanjia ambazo ni rafiki na zinafikika kwa wengi kama mitandao ya kijamii. Mfano, kuna ambao wako kwenye magroup ya WhatsApp lakini hawawezi kueleza wala kujibu chochote. Tunao mkanasha wetu maalum wa Jamiiforums lakini wameshindwa kuutumia kuzungumza na wananchi waliowachagua. Viongozi wengine hawafahamu kabisa wala hawatumii mitandao ya kijamii

(iv)Njia za utoaji taarifa kwa wananchi bado ni za kizamani, haziendani na kasi ya teknolojia iliyopo. Mfano ni website ya halmashauri ambayo imetoa taarifa kwa mara ya mwisho 2012

TAARIFA

1. Ujenzi wa Soko Kuu

Matarajio katika ujenzi wa soko ilikua mpaka kufikia Disemba zabuni iwe imetangazwa na mshindi ametangazwa tayari. Pia tulitarajia kuwa wafanyabiashara wawe tayari wamehamishiwa katika soko la muda ili kupisha ujenzi. Ila haijawa kama matarajio yalivyokua kwa maana hata mazungumzo na muwekezaji hayajakamilika bado kwa maana bado andiko halijakamilishwa kutokana na halmashauri kushinwa kulipa ile million 50 iliyoitajika na mshauri OGM ili kukamilisha andiko. Lakini pia mbia na namna ya kupata 30% ya pesa inayotakiwa kutolewa na halmashauri bado haijafahamika

2. Ujenzi wa Stand
Bado taratibu zinafanywa ili kukaribisha wawekezaji wadogo wadogo kujenga kwa kufuata ramani na kwa mkataba maalum na halmashauri. Matarajio ilikua zoezi hilo litangazwe Disemba hii

3. Ujenzi wa Soko la Kashai
World Bank wamekubali kufadhili ujenzi wa soko hili. Matarajio ilikua ni zabuni kuwa imetangazwa na mzabuni kupatikana ifikapo kabla ya kuisha Disemba hii, lakini bado mabo hayo hayajafanyika

4. Mikopo kwa Wanawake na Vijana
Vijana na wanawake wanaendelea kupata mikopo katika SACCOS zilizoainishwa

5. Urasimishaji Makazi
Zaidi ya nyumba 1300 zimekwisha pata mchoro toka mradi uanze na zoezi la uchukuaji data (mipaka ya viwanja kwaajili ya mchoro wa TP) na kuhamasisha uchangiaji linaendelea

6. Bima ya Afya
Zoezi hili limekwama kwasababu mbunge hajaelekeza, kuhimiza halmashauri jinsi rahisi ambayo tulikubalia katika utekelezaji wa hili zoezi. Lakini kwa muda uliobaki inawezekana kufikia malengo kama litafanyika

HITIMISHO

Utekelezaji wa vipaumbele vingi umekua ukisuasua lakini bado kuna muda wa kufikia malengo kama kutakua na jitihada za ziada katika kufanikisha yote.

Imetolewa na

Afisa Habari - Bukoba
 
Hii sijaielewa vizuri, kwani kuna wafanya biashara wameomba kufanya bishara katika hizo njia wamekataliwa!!? Au ni kipi kinaendelea hapo make mwenyewe silielewi vizuri hili japo nitalifuatilia kwa pande zote mbili, mamlaka na wafanya biashara
Fanya hima kabisa maana tunateseka mno sisi watu Wa kyebitembe kahororo kyakairabwa na kibeta miguu imeshapata kutu kwenda mjini hasa asubuhi bodaboda nayo kazi kwanza zinaogopesha wanavyoendesha na nauli hata ya kuzidi ya kwenda kemondo mbona miji mingi wanaweza ambayo ni midogo kuliko bk tena sio kazi kubwa tu ni suala la kuweka route tu mfano kutoka kahororo na kyakairabwa sijui Wateja watakosa kama nauli itakuwa 1000 au mia nane na namnq hivyo mji utapanuka maana mtu anaweza jenga nje ya mji akiona kuna usafiri mzuri Wa kwenda mjini yaani kutoka nshambya kwa bodaboda sh1000 sawa na kutoka bk kemondo msiwe na hofu wekeni route tu muone kama haitawezakana mbona zamani zilikuwepo za rwamishenye na kibeta yaani moshi wana daladala wakati mji una 59 sq na bkb in 80 upi mji mkubwa
 
Lakini kaa ukijua halmashauri haina magari ya abilia kwa ajili ya biashara hivyo ni mpaka wamiliki wa Magari waamue na sio kuwalazimisha, na kuna mmoja kashauli halmashauri iwekeze kwenye hiyo sekta, ni wazo na wataalam wanaweza kusaidia kwa hilo kama inaruhusiwa au inawezekana
 
Wekeni route muone hiyo ndo kazi yenu na kuhamasisha wafanyabiashara hii ndo kazi wafanyabiashara wanafikiri labda hairuhusiwi
 
Mambo ya stendi na soko tumuombe Mungu tu maana kuna usiasa mwingi na maneno mengi nashauri kuanza Mara moja na mtaa ujenzi lini tarehe ngapi na vitamalizika lini porojo hizi tumesikia hata kipindi kile cha ccm
 
Fanya hima kabisa maana tunateseka mno sisi watu Wa kyebitembe kahororo kyakairabwa na kibeta miguu imeshapata kutu kwenda mjini hasa asubuhi bodaboda nayo kazi kwanza zinaogopesha wanavyoendesha na nauli hata ya kuzidi ya kwenda kemondo mbona miji mingi wanaweza ambayo ni midogo kuliko bk tena sio kazi kubwa tu ni suala la kuweka route tu mfano kutoka kahororo na kyakairabwa sijui Wateja watakosa kama nauli itakuwa 1000 au mia nane na namnq hivyo mji utapanuka maana mtu anaweza jenga nje ya mji akiona kuna usafiri mzuri Wa kwenda mjini yaani kutoka nshambya kwa bodaboda sh1000 sawa na kutoka bk kemondo msiwe na hofu wekeni route tu muone kama haitawezakana mbona zamani zilikuwepo za rwamishenye na kibeta yaani moshi wana daladala wakati mji una 59 sq na bkb in 80 upi mji mkubwa
Hivi hawa viongozi wao wanaishi wapi jamani ama ndo wale wasiokaa hata na majirani. Hivi hata kama hawaoni hata kusikia hawasikii kwamba wananchi wao mji mzima wanaumizwa na kukosekana kwa huduma hii kweli? Ni kweli hili hawalijui?
 
M
Lakini kaa ukijua halmashauri haina magari ya abilia kwa ajili ya biashara hivyo ni mpaka wamiliki wa Magari waamue na sio kuwalazimisha, na kuna mmoja kashauli halmashauri iwekeze kwenye hiyo sekta, ni wazo na wataalam wanaweza kusaidia kwa hilo kama inaruhusiwa au inawezekana

Mh.katibu wa mbunge, usipende kutuchanganya. Hivi kwanini nyie viongozi wa Bukoba ni wagumu kuelewa kiasi hiki? Tumekupa utaratibu jinsi haya mambo yanavyokwenda, haihitaji uwe umefika chuo kikuu. Na kama hiki kitu ni kigeni kwenu kiasi hiki basi nendeni mikoa jirani mkajifunze huko, kwanini mnakuwa wabishi hivi hata kujifunza hamtaki, why so stubborn?

Sasa mnataka kila kitu tuwaoneshe sie, hata nyinyi kwenda kujifunza kwingine tuwaambie sie, nyie ni viongozi wa aina gani bwana? That's why mji wetu hausongi tatizo ni watu wasiokuwa na exposure ya kutosha still, they don't want to learn. If you don't change your way of thinking then you don't fit to our current mission, mnasumbua mno nyie viongozi na msitake tuwaite mizigo.

Tumekwambia na tunakutuma sasa kwasababu sisi ndo mabosi wenu. Mwambie mbunge wako akae na uongozi wake watangaze routes na pili muitishe vikao na wamiliki wa daladala ili waweze kuzifahamu hizo routes na waanze kutoa huduma kwa wananchi mara moja. Nyinyi mnawasaidiaje wananchi wakati hamko tayari kupambana kwa ajiri ya mnaowaongoza, mnatetea masrahi ya nani? Hamjaona hata mikoa mingine daladala zikilazimishwa vituo na routes, sasa nyinyi mnakaa tu hata kukaa vikao na wamiliki mnashindwa.

Hiyo manispaa kama inawashinda ni vyema mkawatangazia wananchi, huu siyo mda wa kubembelezana na kusumbuana. Mmechelewa kiasi gani mpaka Leo ama bado hamuoni? Yaani vitu vikubwa vinawashinda hayo mamiradi yamekwama hata hivi vidogo navyo vinawashinda kweli, are you serious? Hivi kuongoza mlilazimishwa ama mliomba wenyewe, itumikieni jamii mnayoiongoza kwa weredi na kujituma na kila mmoja atimize wajibu wake.
 
TAARIFA YA MRADI DECEMBER, 2016

Utangulizi

Tushirikishane ni mradi unaowahusisha viongozi wa kuchaguliwa (mbunge na madiwani) serikali (halmashauri) na wananchi katika kurahisisha upatikanaji wa maendeleo. Wadau wakuu wa mradi huu ni Halmashauri ambayo ndiyo kitovu cha mipango ya maendeleo na utekelezaji wake, Mbunge ambaye ni msimamizi wa serikali (halmashauri), Jamiiforums ambao ni wasimamizi wa mradi na Wananchi.

Utekelezaji wa mradi unaanzia Halmashauri ambayo inasimamia miradi yote na inayotokana na vipaumbele vyetu ambavyo ni (1) Ujenzi wa Stand Kuu ya Mabasi, ujenzi wa Soko la Kuu na Soko la Kashai (2) Urasimishaji Makazi (3) Mikopo kwa Wanawake na Vijana, na (4) Bima ya Afya. Pia inatoa taarifa kwa kila hatua inayofikiwa katika vipaumbele vyote. Mbunge katika mradi ni daraja kati ya manispaa na wananchi katika kuweka msukumo wa utekelezaji na kutoa taarifa kwa wananchi. Halmashauri na mbunge wanawajibika moja kwa moja kwa wananchi. Jamiiforums ni mfatiliaji wa shughuli zote za mradi (utekelezaji wa vipaumbele) inatoa taarifa kwa wananchi juu ya mradi

TATHMINI YA MRADI YA MIEZI MITANO (5)

Mafanikio

(i)Utekelezaji wa mradi ulianza kwa changamoto ya upatikanani wa taarifa, awali ofisi ya mbunge na mbunge kwa ujumla hawakuwa wakielewa wajibu wao katika mradi hivyo ushirikiano wao haukua wa kuridhisha hivyo kusababisha ugumu katika kupata taarifa. Baada ya miezi mine (4) ya utekelezaji wa mradi, ofisi ya mbunge na mbunge walielewa wajibu wao na kuweza kushiriki vyema katika kutoa taarifa ya mradi

(ii)Swala la halmashauri kutoa taarifa kwa wananchi ni mtambuka na mradi umekua ukisisitizo hilo kwamaana ya kwamba taarifa ni mali ya wananchi hivyo inapasa ziwafikie ili waweze kushiriki. Lakini pia, ushirikishwaji wa wanannchi katika maswala ya maendeleo yao ni dira ya halmashauri ya manispaa ya Bukoba. Mradi umejitahidi kuwaelimisha viongozi wa halmashauri ikiwemo na mbunge juu ya swala hili na kuna mafanikio yameanza kuonekana mfano;

(iii)Mbunge na naibu meya wameanza kutoa taarifa mbalimbali na kuongelea maswala yanayohusu manispaa kupitia akaunti zao za facebook

(iv)Mbunge ameahidi kufanya mkutano kwa kila mwezi kwa kualika vyombo vya habari ili kutoa taarifa

(v)Mbunge ameahidi kuhakikisha kila kikao cha baraza la madiwani kuwa kinatangazwa katika vyombo vya habari na magari ya matangazo ili wanachi wafahamu na kuhudhuria

(vi)Mbunge ameahidi pia kuwa kila kikao cha baraza la madiwani kitakua kikieushwa katika televishen ya Bukoba (Bukoba Cable Network) ili wananchi ambao hawataweza kuhudhuria kikao hicho waweze kufahamu nini kinaendelea

(vii)Ushiriki na ufatiliaji wa wananchi wa mradi huu unazidi kuongezeka, mfano nisipoweka taarifa katika mkanasha kwa muda kadhaa watu wanaulizia sababu za kufanya hivyo. Na pia idadi ya watu wanaochangia na hata kupitia mkanasha wetu imekua ikiongezeka

(viii)Viongozi wamefahamu kuwa wananchi wanauwezo na nafasi ya kuwahoji kupitia mradi huu

(ix)Mkutano wa BUMUDECO 2017 ni moja ya mafanikio ya mradi pia

Changamoto

(i)Bado kunachangamoto ya meya wa manispaa kukubali mradi vyema na kushiriki vyema hasa katika swala la taarifa

(ii)Msukumo na ushawishi wa mbunge kwa halmashauri katika utekelezaji wa vipaumbele bado hauridhishi

(iii)Viongozi wa kuchaguliwa halmashauri ya manispaa ya Bukoba ni waonga wa kuongea na wananchi kwanjia ambazo ni rafiki na zinafikika kwa wengi kama mitandao ya kijamii. Mfano, kuna ambao wako kwenye magroup ya WhatsApp lakini hawawezi kueleza wala kujibu chochote. Tunao mkanasha wetu maalum wa Jamiiforums lakini wameshindwa kuutumia kuzungumza na wananchi waliowachagua. Viongozi wengine hawafahamu kabisa wala hawatumii mitandao ya kijamii

(iv)Njia za utoaji taarifa kwa wananchi bado ni za kizamani, haziendani na kasi ya teknolojia iliyopo. Mfano ni website ya halmashauri ambayo imetoa taarifa kwa mara ya mwisho 2012

TAARIFA

1. Ujenzi wa Soko Kuu

Matarajio katika ujenzi wa soko ilikua mpaka kufikia Disemba zabuni iwe imetangazwa na mshindi ametangazwa tayari. Pia tulitarajia kuwa wafanyabiashara wawe tayari wamehamishiwa katika soko la muda ili kupisha ujenzi. Ila haijawa kama matarajio yalivyokua kwa maana hata mazungumzo na muwekezaji hayajakamilika bado kwa maana bado andiko halijakamilishwa kutokana na halmashauri kushinwa kulipa ile million 50 iliyoitajika na mshauri OGM ili kukamilisha andiko. Lakini pia mbia na namna ya kupata 30% ya pesa inayotakiwa kutolewa na halmashauri bado haijafahamika

2. Ujenzi wa Stand
Bado taratibu zinafanywa ili kukaribisha wawekezaji wadogo wadogo kujenga kwa kufuata ramani na kwa mkataba maalum na halmashauri. Matarajio ilikua zoezi hilo litangazwe Disemba hii

3. Ujenzi wa Soko la Kashai
World Bank wamekubali kufadhili ujenzi wa soko hili. Matarajio ilikua ni zabuni kuwa imetangazwa na mzabuni kupatikana ifikapo kabla ya kuisha Disemba hii, lakini bado mabo hayo hayajafanyika

4. Mikopo kwa Wanawake na Vijana
Vijana na wanawake wanaendelea kupata mikopo katika SACCOS zilizoainishwa

5. Urasimishaji Makazi
Zaidi ya nyumba 1300 zimekwisha pata mchoro toka mradi uanze na zoezi la uchukuaji data (mipaka ya viwanja kwaajili ya mchoro wa TP) na kuhamasisha uchangiaji linaendelea

6. Bima ya Afya
Zoezi hili limekwama kwasababu mbunge hajaelekeza, kuhimiza halmashauri jinsi rahisi ambayo tulikubalia katika utekelezaji wa hili zoezi. Lakini kwa muda uliobaki inawezekana kufikia malengo kama litafanyika

HITIMISHO

Utekelezaji wa vipaumbele vingi umekua ukisuasua lakini bado kuna muda wa kufikia malengo kama kutakua na jitihada za ziada katika kufanikisha yote.

Imetolewa na

Afisa Habari - Bukoba[/QUOTE

Dada asante. Ukiisoma vizuri taarifa hii utagundua jambo moja kubwa, ofisi ya mbunge kwa ujumla wake na wakiwa chini ya chama chao, ni JIPU. Ni majipu.
 
Back
Top Bottom