TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

Kasuala ka daladala kakiwashinda nitasema hatuna viongozi weledi bukoba kasuala kadogo hakaitaji hata mwezi wakitangaza tender na kukubaliana nauli routes na wafanyabiashara yaani mwezi Wa kwanza hauishi bila daladala ila Nina hofu kama wameshindwa kuhamisha stendi ya bugabo sijui sijui watawexa ka swala mji utabikia hivi hivi bila maendeleo yoyote yaani fyu!! Bukoba tunaishi kama hatuna serikali majumba mazuri lakini miundombinu ovyo kabisa

Sent from my VF685 using JamiiForums mobile app
 

Unajua tatizo ni kwamba ndugu zetu nyinyi mlioko hapo mmekuwa mkiishi na hawa viongozi wenu kwa kuwanyenyekea na kuwabembeleza mno kiasi kwamba wala hawana hofu na nyie. Kunatakiwa sahivi kuweka hizo tabia pembeni na kuvaa sura ya mbuzi, natamani binafsi ningekuwepo hapo hiyo ofisi ya mbunge tungeitia kufuri kwanza. Hatuwezi kuendelea kuwa na mabwanyenye tukafika hata siku moja, hawa watu wanaharibu maisha yenu wakati wao washafanikiwa tayari, na wengine hawana expectations kama nyie mlio kwenye 20/30's. Kucheka na hawa jamaa ni kuendelea kupoteza fursa, hii ofisi hakika inahitaji kufungwa mpaka jamaa aje na majibu ya maana, huu upuuzi iwe mwisho.

We need to change our minds, mnaogopa nini? Uoga wenu ndio umaskini wenu and you don't need to be afraid of facing the reality. Nyinyi wananchi hapo hamna haja ya kudeal na manispaa, nyinyi hasira zenu mnatakiwa kumface mbunge. Anawajibika kwenu moja kwa moja, kinachoitajika ni kuamua tu.
 
Hatua za miradi mikubwa ya ujenzi zinaendelea vizuri sana japo kwa umakini na wakati mwingine kimya kimya kukwepa masnitch wasitibue

Basi hakuna umuhimu wa hii thread. Maana lengo la Tushirikishane ni mwananchi kuhusishwa kwenye process nzima
 
Basi hakuna umuhimu wa hii thread. Maana lengo la Tushirikishane ni mwananchi kuhusishwa kwenye process nzima
Teh teh teh! Umenifufahisha sana mkuu, hao ndo viongozi wetu bwana. Ujanja ujanja na maneno ndo kila kitu yaani wanatuchukulia kama vitoto vidogo hivi. Hawa jamaa ni majipu, na narudia kusema hawa jamaa wakiongozwa na ofisi ya mbunge Lwakatare, ni majipu makubwa mno.
 
BUKOBA MANISPAA YANG'AA MATOKEO YA KIDATO CHA PILI



Mkoa wa Kagera umeanza kurejesha heshima yake katika elimu ndugu zangu. Tumeshuhudia mkoa ukishika nafasi ya 5 katika matokeo ya darasa la saba 2016, shule 2 kutoka kagera zimeingia katika top 10 ya matokeo ya kidato cha nne. Na shule ambayo imeongoza katika matokeo ya kidato cha nne kwa miaka miwili mfululizo (au zaidi) inapatikana mkoani kwetu[emoji4]

Tukaze buti, tuhimize wawekezaji wengi zaidi katika elimu na hasa ktk elimu ya ufundi na form 5 na 6
 
Ijapokuwa wenye viburi vyao vya madaraka wanatutukana na kutukejeri lakini hiyo haitatukwamisha katu, Kagera tukiamua tunaweza sana kwani tangiapo hatujawahi kusaidiwa na hao "viburi" na wala hatuwategemei kwa lolote. Tunajiweza pamoja na wote wanaotuombea mzuri tutapigana kiume na tutashinda. Tunawapongeza sana wale wote wanaojitoa kuhakikisha elimu inschanua upya
 
Mh. Mwakyoma ambaye ni diwani wa Bakoba akishirikiana na wananchi wenzake kutengeneza barabara inayotoka Bunena kuelekea Karobela beach ili kufungua beach hiyo. Ujenzi wa barabara unafanyika kwa pesa za mfuko wa jimbo na nguvu ya wananchi.

Hongera sana Mh. Mwakyoma na watu wa Bakoba.

.com/mobile-gallery/6be5086a1ac87c06158012b7dcd5e61f.jpg[/IMG]
 


Moja kati ya malengo ya mradi wa TUSHIRIKISHANE ni kuboreshwa kwa mfumo wa ushirikiano kati ya wananchi na viongozi katika kutekeleza sera na ahadi za wakati wa uchaguzi.

Je unafikiri nini kinakwamisha ushirikiano wa wananchi wa Bukoba na viongozi?
 
Asante dada kwa updates.
 
Siasa na ubinafsi mwingi kwa viongozi
 
Hatutaweza kujadiri na kuwa na mipango ya maana mpaka pale tutakapoweza kumpata mbunge mwenye kuelewa kwanini yuko pale
 
Juzi meya kupitia jukwaa hili amenukuriwa akisema barabara za mjini tayari tenda imetangazwa na ujenzi uko mbioni.. Tunaomba uthibitisho wa usahihi endapo kweli hiyo tenda ishatangazwa ili tuachane na siasa
 
Ningekuwa naweza hii thread ningeifuta ili isiwepo kwani inatia kinyaa sana
 
Hongera sana wadogo zetu fm4 kwa kuirudisha historia ya mkoa wa Kagera, Mungu ibariki Kagera
 
KATIKA HISTORIA; Tunaona Henry Stanley alivyogundua Bukoba kama anavyoeleza Kjekshus Helge - Ecology Control

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…