instanbul
JF-Expert Member
- Jun 26, 2016
- 12,037
- 17,212
Kasuala ka daladala kakiwashinda nitasema hatuna viongozi weledi bukoba kasuala kadogo hakaitaji hata mwezi wakitangaza tender na kukubaliana nauli routes na wafanyabiashara yaani mwezi Wa kwanza hauishi bila daladala ila Nina hofu kama wameshindwa kuhamisha stendi ya bugabo sijui sijui watawexa ka swala mji utabikia hivi hivi bila maendeleo yoyote yaani fyu!! Bukoba tunaishi kama hatuna serikali majumba mazuri lakini miundombinu ovyo kabisaM
Mh.katibu wa mbunge, usipende kutuchanganya. Hivi kwanini nyie viongozi wa Bukoba ni wagumu kuelewa kiasi hiki? Tumekupa utaratibu jinsi haya mambo yanavyokwenda, haihitaji uwe umefika chuo kikuu. Na kama hiki kitu ni kigeni kwenu kiasi hiki basi nendeni mikoa jirani mkajifunze huko, kwanini mnakuwa wabishi hivi hata kujifunza hamtaki, why so stubborn?
Sasa mnataka kila kitu tuwaoneshe sie, hata nyinyi kwenda kujifunza kwingine tuwaambie sie, nyie ni viongozi wa aina gani bwana? That's why mji wetu hausongi tatizo ni watu wasiokuwa na exposure ya kutosha still, they don't want to learn. If you don't change your way of thinking then you don't fit to our current mission, mnasumbua mno nyie viongozi na msitake tuwaite mizigo.
Tumekwambia na tunakutuma sasa kwasababu sisi ndo mabosi wenu. Mwambie mbunge wako akae na uongozi wake watangaze routes na pili muitishe vikao na wamiliki wa daladala ili waweze kuzifahamu hizo routes na waanze kutoa huduma kwa wananchi mara moja. Nyinyi mnawasaidiaje wananchi wakati hamko tayari kupambana kwa ajiri ya mnaowaongoza, mnatetea masrahi ya nani? Hamjaona hata mikoa mingine daladala zikilazimishwa vituo na routes, sasa nyinyi mnakaa tu hata kukaa vikao na wamiliki mnashindwa.
Hiyo manispaa kama inawashinda ni vyema mkawatangazia wananchi, huu siyo mda wa kubembelezana na kusumbuana. Mmechelewa kiasi gani mpaka Leo ama bado hamuoni? Yaani vitu vikubwa vinawashinda hayo mamiradi yamekwama hata hivi vidogo navyo vinawashinda kweli, are you serious? Hivi kuongoza mlilazimishwa ama mliomba wenyewe, itumikieni jamii mnayoiongoza kwa weredi na kujituma na kila mmoja atimize wajibu wake.
Sent from my VF685 using JamiiForums mobile app