TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

Waliingia choo cha kike wakakutana na usanii wa kuzungusha mikono. Wazee wa "mabadiriko" na sasa sijuhi hapo Bukoba kama kuna hata vidariri vya hayo "mabadiriko' waliyoyakimbilia pasipo kujua.

Lwaka ni bonge la msanii
Acheni propaganda uchwara. Huyo kagasheki alifanya kipi cha maana hapa bukoba mjini zaidi ya kila matanuzi, mtu ndege ya watu 13 anaikodi binafsi toka mwanza kuja hapa bukoba kila mara. Kwanza hakunaga mbunge anaefanyaga chochote Tanzania.Wote wanategemea miradi iliyopangwa na serikali. Kama bajeti ya miradi haijapita ktk Jimbo hata mbunge apige kelele vipi haisaidii maana bajeti za nchi hii ni ndogo na hazitekelezeki.
 
Jengeni sitendi kwanza kitu kinachomgusa kila mtu
 
Mimi na wewe hatubishani na hatuna haja, kikubwa ni kukubaliana kwamba mji wetu umerudi nyuma kwa mwonekano na unarudi nyuma kwa kasi. Sasa mie na wewe tunakubaliana kufanya nini kwa ajiri ya mji wetu badala ya kulumbana kusiko na tija? Wanasiasa achana nao kwasababu hitaji lao ni kula na miaka 5 ni mingi kwao, wanavuna na wanakula milele. Mimi na wewe ndo tunhangaika na tunachanganywa na hawa mabwana matumbo
 
Ni mara kumi ingeongozwa na CCM kuliko hawa macoward wa Ukawa.
 
Kikubwa tusubirie hiyo reli ya SGR tuone italeta impact gani kwa jiji la mwanza.Ikileta impact nzuri mwanza na sisi bukoba tutaona mabadiliko kwetu. Vifaa vya ujenzi wa makazi na vifaa vya ujenzi wa miundombinu yetu vitafika hapa kwa wingi na kwa gharama nafuu.Tetemeko lilituathiri sana kutokana na ujenzi duni wa makazi yetu unaochangiwa na gharama kubwa za kununua vifaa bora vya ujenzi.Mji hujengwa na watu wake. Wabunge hawa Kazi yao kubwa ni kutunga sheria na Kuipigia kelele serikali ktk upatikanaji wa maji, umeme, hospital na miundombinu kama barabara na anga.Vyote hivi vinategemea bajeti ya serikali na serikali yetu vyanzo vya bajeti ni vya aibu Sana Sana japo nchi hii Ina kila Kitu.Watanzania tungekuwa tunajielewa tungedai katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.Hii ingekuwa silaha yetu. Kama nchi Ina kila Kitu na mambo yanaenda kwa mwendo wa kobe chama kilicho madarakani kwenye kura kinapigwa chini kinawekwa kingine. Lkn hii ya hata ukipiga kura ama usipige chama kinashinda ni laana kwetu.
 
Mh. yawezekana wewe ni mwanasiasa na na unayaona matatizo yetu kisiasa sana sijuhi unamwogopa nani ama una hofu ya nani. Unawezaje ukayakubali matatizo yako eti kisa hakuna reli, uko sawa kweli? Yaani wewe unaridhika hapo mjini kuwa mashimo hivyo utafikiri ni maandaki ya kambi, mjini kumekuwa kama zizi la nguruwe halafu huoni kama ni tatizo. Yaani hiyo kata ya bilele ina diwani lakini mitaa ni michafu kama machungoni na bado unafikiri ni kukosekana kwa SGR! Pathetic sana, nimeshindwa kukutafakari jinsi unavyoyaona maisha.
 
Hivi huku haya yalilenga nini kama hamkuwa na ya kufanya na kuwaambia wananchi?
 
Mbunge na timu yako mna hoja za kujibu kwa wapiga kura wenu. Mshahara wa bunge mle lakini mkae mkijua hapo mwisho. Tutawasihi CDM watafute damu zingine mpya tuwape kura. Hata wapinzani mmekuwa wasindikizaji bungeni mnanywea kama kipande cha mkate kwenye chai. You are simply vocaless!
 
Ndugu zangu kwanza naomba nianze kwa kumshukuru Mungu wetu kwa kuendelea kutupigania wana Kagera. Tunapitia magumu mengi lakini tunazidi kukomaa pia. Tunakomaa kwa vyote, kiakili na kifikra pia. Tuendelee kupambana na kusaidiana sisi wenyewe na hii ndo njia pekee ya kuuinua mkoa wetu wa Kagera.

Nirudi kwenye mada, ndugu zangu majuma kadhaa huko nyuma nilitoa ahadi kwenu. Niliwahaidi kuanzisha blog yetu kwa ajiri haswa ya kutusaidia kuongea yoote yanayotuhusu kama mkoa. Ninapenda kuwajuza kwamba sasa mambo yako tayari na yameiva, niliwahaidi na nimetekeleza. Blog tayari imeshaanza kazi na inatumia jina la ...kaitabakwetu.blog, lakini pia tumeifungulia page fb kwa jina hilo hilo la kaitabakwetu ...kwa ajiri haswa ya mkoa wetu wa Kagera.

Ombi langu ni moja, kwasababu mie siko hapo mkoani nahitaji mtu mmoja aliye tayari tuone namna ya kuyaongea na kuyaweka hewani yale yote tunayoona yanatugusa kama mkoa. Nikimpata huyu naamini kazi itakuwa imesha na hazma yetu ya kuuongelea mkoa wetu itakuwa successful 100%

Asanteni Sana. Mwije twombeke eyaitu ichwena amoi. Munyegele inywena!
 
Mtafute uyo afisa habari tunayemuona hapa au kwakua ni mwajiriwa wa JF hawezi fanya kazi na wewe ebu ongea naye
 
Napata mashaka kama hakika umesoma nlichoandika.Sijui uwezo wako wa kuelewa ukoje.Rudia tena kusoma naona unajichanganya.
 
Safi
Mtafute uyo afisa habari tunayemuona hapa au kwakua ni mwajiriwa wa JF hawezi fanya kazi na wewe ebu ongea naye
Safi mkuu japo niliwahi kumtrace na akaonesha ushirika lakini namba yake sina na hata nilivyojaribu kum pm hakuweza kurespond tena

Any way, ntajitahidi tena nione kama naweza kuongea tena nione
 
Napata mashaka kama hakika umesoma nlichoandika.Sijui uwezo wako wa kuelewa ukoje.Rudia tena kusoma naona unajichanganya.
Sawa mkuu, tuendelee na mengine tuijenge Kagera yetu.
 
Napata mashaka kama hakika umesoma nlichoandika.Sijui uwezo wako wa kuelewa ukoje.Rudia tena kusoma naona unajichanganya.
Sawa mkuu, tuendelee na mengine tuijenge Kagera yetu.
 
Wananchi wanaotumia barabara ya Kashozi wamelalamikia adha ya ufinyu wa barabara ya hiyo hasa eneo ilipokua shule ya msingi ya Tumaini ambayo iliamishwa kutokana na upanuzi wa uwanja wa ndege. Malalamiko hayo yametokana na kuzungushiwa senyenge eneo hilo ilipokuwepo shule na hivyo kufanya eneo la watembea kwa miguu na wamachinga kuwa finyu kiasi cha kulazimisha watembea kwa miguu kutumia njia ya vyombo vya moto. Aidha, meneja TANROADS ameishauri halmashauri kuhamisha wamachinga kutoka katika eneo hilo ili libaki kwa matumizi ya watembeao kwa miguu pekee.
 
Hiki kizazi kilichoko hapo Bukoba kina matatizo vichwani mwa watu. Ni sala tu zinazoweza kuwasaidia walau kuweza kujitambua, wanakula stahiki yao
 
CCM wangeweza kumweka mama Tibaijuka hapo manispaa nina uhakika atashinda na atatusaidia sana vinginevyo sioni mtuwingine mkoani kwetu wa kutusaidia. Tunafanya kazi ya kupeleka ma dumbs tu bungeni masaa yote wako kimya kama vile hawana meno mdomoni
 
DODOMA 9/06/2017.

Wabunge wa Mkoa wa Kagera wamefanya kikao na Mhe Balozi wa Uingereza Bi Sara Cooke kujadiliana juu ya misaada kwa maendeleo ya mkoa hususan ujenzi wa shule ya sekondari ya Ihungo iliyoharibika katika tetemeko la tarehe 10/09/2016. Serikali ya Uingereza inajenga shule hiyo upya kwa msaada wa Shs bilioni 6 uliotangazwa tarehe 2/01/2017 wakati. Bi Cooke alipokuwa mgeni rasmi wa mhe Rais John Pombe Magufuli alipotembelea mkoa wa Kagera kuwafariji wahanga wa tetemeko la tarehe 10/09/2016. Balozi huyo amethibitisha kwa Mwenyeji wake aliyemkaribisha katika kikao hicho Prof Anna Tibaijuka ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wabunge wa Mkoa wa Kagera kwamba Uingereza pia itajenga nyumba za walimu katika shule ya sekondari ya wasichana ya Rugambwa zilizoharibiwa na tetemeko. Itakumbukwa kwamba tarehe 2/01/2017 baada ya ziara ya Rais Profesa Tibaijuka alimsindikiza Balozi huyo akaione pia shule ya Rugambwa iliyoathirika kwa tetemeko. Juhudi hizo sasa zimezaa matunda.
Profesa Anna ni mmojawapo wa wasichana waliosoma shule ya Rugambwa ilipofunguliwa mwaka 1965.

Wahe Wilfred Lwakatare (Bukoba Manispaa) na Innocent Bashungwa (Karagwe) wapo katikati. Nd. Sylvester Ernest Afisa Mwandamizi wa Siasa Ubalozi wa Uingereza yu kulia.

Taarifa ya Aidan Mapala

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…