MAFANIKIO YALIYOFIKIWA KATIKA KIPAUMBELE CHA MIKOPO KWA WANAWAKE NA VIJANA
MATEGEMEO SACCOS (VIJANA)
1. Mpaka sasa vimekopeshwa vikundi 19 na vi3 vinasubili.
2. Marejesho yako vizuri kutokana na mikataba yao kuwa na mkazo mkubwa na faini kwa wazembe.
3. Pesa hiyo inakopeshwa kwa kipindi kisichozidi miezi sita unatakiwa kuwa umemaliza marejesho na riba ni 5% tu.
4. Changamoto ni kwamba pesa haipo ya kutosha kiasi kwamba wanachoomba vikundi hawapati kiasi sahihi kwa vile wanalazimika kuzigawagawa ili kuwapatia wote.
5. Mwezi January ndiyo mara ya mwisho *MATEGEMEO SACCOS* kupokea pesa za manispaa ili hali ilisemekana zitakuwa zikipelekwa kila mwezi.
6. Mwisho wameomba tuzidi kuhamasisha umma hasa vijana wafuate utaratibu wa vikundi ili wakapate mkopo uwasaidie kujikwamua.
WANAWAKE TUINUANE SACCOS.
Vikundi vilivyokwisha nufaika na mikopo ni 11 na vinavyotarajiwa kukopeshwa mwezi huu ni vi 3.
Pesa zilizokwishaelekezwa na manispaa kwa saccos hii ni jumla ya Tshs. 40,227,000/=.
Mara ya mwisho kupokea fedha za halmashauri ni tarehe 03/03/2017 ambapo wamepokea kiasi cha fedha Tshs. 6,172,657.50/=
Marejesho si haba na si ya usumbufu sana kwa sababu vikundi vilihakikiwa vizuri kabla ya kupewa mikopo hivyo ufuatiliaji ni mwepesi.
CHANGAMOTO.
1. Vikundi vingi vilivyosajiliwa na manispaa ni vikundi hewa, hivyo yalikuwepo mazoea ya kuchukua mikopo ya halmashauri kirahisi na kuitafuna na kupotea, kwa sasa kikundi kinahakikiwa vilivyo hivyo kuondoa mianya ya wapiga dili.
2. Siasa zinaingilia ufanisi wa shughuri nzima ya utoaji mikopo, wanasiasa katika maeneo yao wanawasukuma wananchi wakaombe mikopo hata kama hawana sifa na vigezo vya kukopeshwa wanasiasa wanataka kusimamia makundi hayo yapewe pesa kwa masrahi yao ya kisiasa hata kama vikundi hivyo havikidhi vigezo.
3. Taarifa zinazotolewa na manispaa kwa umma kuhusu mikopo ni za kimalengo lakini ni tofauti na uhalisia, pesa hazipelekwi kwa wakati na hata cheki zinapokuwa zimesainiwa kunakuwa na uzungushwaji mpaka kuipata, wakati huo wananchi hawayajui wao wanachotaka ni pesa na wanakuwa wameshaelezwa kuwa pesa inapelekwa kila mwezi jambo ambalo sio kweli.
4. Riba iliyopangwa na manispaa ni ndogo ukilinganisha na garama ya uendeshaji wa huduma kwa vikundi.
5. Vikundi vinakuwa na wanachama wengi na pesa inayokuwepo inakuwa kidogo kiasi kwamba haziwatoshi, mf. kikundi cha watu 20 unawapa mil 2 au 3 zinakuwa kidogo sana na vikundi vinakuwa ni vingi na vyote vinahitaji. Na kingine ni kwamba pesa hazipelekwi kila mwezi.
6. Kwa sababu za msingi bila shaka, manispaa imezitaka saccos hizi ziwasilishe majina ya vikundi vilivyoomba mikopo ili yajadiliwe kwenye kamati ndogo ya mikopo ya manispaa na kupitishwa kupata mikopo, saccos kwa mjibu wa sheria za ki ushirika wana miongozo yao namna ya kuvijua vikundi, sifa na vigezo na zinaouwezo wa kwenda mpaka maeneo ya waombaji ili kujiridhisha kabla ya kukopesha, hivyo hawaoni sababu ya vikundi hivyo kupitiwa na kujadiliwa tena jambo ambalo linaweza kuua ufanisi wa huduma kwa sababu kamati inaweza kupendekeza kinyume. Majadiliano juu ya jambo hili bado yanaendelea ili kupata muafaka.
MAONI
1. Saccos hizi kama zilivyoaminiwa na kupewa mikataba basi ziachwe huru kutekeleza huduma kwa wananchi kwa kuzingatia vigezo na masharti, kuingiliwa na wanasiasa kwa kutaka vikundi flani vipewe kipaumbele hata kama havikidhi vigezo kutaua ufanisi wa huduma.
2. Halmashauri kuingilia utaratibu wa saccos katika kuvipitisha vikundi kupata mikopo kunaweza kuleta mwanya wa kuchomeka vikundi hewa hivyo kusababisha upotevu wa pesa za serikali jambo litakalosababisha wadhamini wa saccos kupoteza mali/dhamana zao ili kufidia pesa zilizopotea.
3. Uhamasishaji na uelimishaji kwa wananchi kuunda vikundi halali uendelee ili kuchukua nafasi ya vikundi hewa lukuki vilivyosajiliwa manispaa ili umma mkubwa unufaike na mikopo hiyo.
4. Pesa zielekezwe kwa wakati kwenye saccos ili kukidhi uhitaji wa vikundi.
5. Riba ya 10% isitafsiriwe kwa kigezo cha muda, kama ulivyo mkataba baina ya halmashauri na saccos ni kwamba riba itakuwa 10% kwa mwaka na kama ni miezi 6 itagawanyika kwa mbili na kuwa 5% na kama ni miezi 3 itakuwa 2.5%. Saccos inaomba 10% iwe uniform bila kujali muda.
Imeandaliwa na Katibu wa Mbunge
Alex Xavery