TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

Dada haya yanayosemwa ya tangazo la Ded ni kweli juu ya pesa 1.6bn kwa ajiri ya miradi, ni miradi gani hiyo iliyokusudiwa na mbona hata wewe mwenyewe hujawahi kutuweka wazi hapa kwenye bango lenu la Tushirikishane ili Tushirikishane?
Hiyo pesa ni kweli, unaweza kutembelea website ya manispaa kwa ufafanuzi zaidi. Na taarifa ya miradi utaipata huko pia. Isipokuwa hizo pesa hazihusishi stand na soko ndiyo sababu sijazileta hapa

[emoji4]
 
Kwa hiyo mnaanza lini au mtazila
 
Hiyo pesa ni kweli, unaweza kutembelea website ya manispaa kwa ufafanuzi zaidi. Na taarifa ya miradi utaipata huko pia. Isipokuwa hizo pesa hazihusishi stand na soko ndiyo sababu sijazileta hapa

[emoji4]
Ehh kwani kuna tatizo gani kubwa linalotuaibisha bukoba kama stendi,soko na barabara zilizo chini ya viwango mnataka kulipa mishahara kwanza na posho?
 
We unaleta siasa kwani CCM wameongoza manispaa kwa muda gani? Walifanya nini
 
We unaleta siasa kwani CCM wameongoza manispaa kwa muda gani? Walifanya nini
Siasa zishabadilika mkuu, huoni hata CCM wenyewe hawaamini kinachowatokea? JPM ana sera yake nje ya chama lakini kupitia chama. Nisikuchoshe sana, kama unaifurahia hari iliyoko endelea kuogelea
 
Hivi kwa nini thread hii haichangamuki? Ukimya Wa wanakagera ndio unafanya miradi isitekelezwe kwa haraka tubalike
 
Ukarabati wa Barabara Eneo la Stand Kuu ya Mabasi

Pichani ni karabati wa barabara eneo la stand kuu ya mabasi ukiendelea. Eneo hilo limekua na hali mbaya na kutopitiki kwa muda mrefu sasa kutokana na kuwa na mashimo mengi na makubwa yaliyokua yakisababisha picha mbaya ya mji. Aidha, mashimo hayo yalitokea miezi michache tu baada ya ukarabati wa mwisho wa barabara hiyo kufanyika hapo mwaka jana na yamechukua muda mrefu kidogo kushughulikiwa.

Ninapongeza jambo hili. Na nimatarajio yangu kuwa ukarabati wa sasa utakuwa wa tija!
 
Kwa hapo tunashukuru,ila wasitengeneze nusu barabara lami ifike kwenye majengo na mitaro itengenezwe vizuri na kuwekewa kalvati nZr ikiwezekana wafunue barabara zote mjini kati na zitengenezwe kama kashozi road ilivyo au ile ya rwamishenye ili kuondoa vumbi na kufanya bk kuwa modern hapo nitafurahi sana
 
Kinatengenezwa kipande kidogo kwanza lakini mashimo yapo mpaka Rwamisenye. Barabara ya Kashura pia imeathirika sana na mashimo. Kwa kifupi barabara zote kuu zinazoingia mjini zimeathiriwa na mashimo isipokua ya Kashozi
 
Unaweza ukanieleza ujenzi Wa stendi unaanza lini maana hata kama barabara hiyo itatengenezwa wingi Wa magari ya kutoka stendi,miundombinu mibaya ya maji toka stendi barabara itaharibika tu baada ya muda mfupi una habari yayote kuhusu stendi
 
Wanahitaji kupanua mji
 
Wanahitaji kupanua mji
Mimi naona stendi ikishatolewa hapo na kuelekeza kyakairabwa mji utapanuka tu tena mji umeshaanza kufika hiko kabla stendi haijawekwa pia usafiri ukiwa mzr toka sehemu za mbali kama kisindi,ihungo,kahororo,itahwa na katoma mji utapanuka tu maana baada ya tetemeko na mafuriko watu wanatafuta sehemu salama za kujenga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…