TUSHIRIKISHANE Mjadala wa Mipango ya Maendeleo kwa Jimbo la Bukoba Mjini

TAARIFA JUU YA TATIZO LA MAJI NDANI YA MANISPAA YA BUKOBA.

1. Ieleweke kuwa miaka yote BUWASA hakuwa na mtandao wa maji katika kata zote za manispaa ya bukoba, kata ambazo mpaka sasa ziko ktk mtandao wa maji ya BUWASA ni kata 10.5, kata 3.5 ambazo haziko ktk mtandao wa BUWASA ni *kahororo, buhembe, nyanga na 0.5kagondo* hivyo maeneo hayo kutokuwa na maji si ajabu japo ni kero.

2. Kata zinazopata shida ya mgao wa maji kwa sasa ni zile za ukanda wa juu, *kitendaguro, ijuganyondo, kibeta na rwamishenye* kwa nini? Kwa sababu ikumbukwe kulikuwa na agizo la mkuu wa nchi kwa Tanesco kuwakatia huduma ya umeme wadaiwa wote, na BUWASA ilikuwa ni moja wapo, umeme ulipokatwa awali uliathili huduma ya maji kwa manispaa nzima mpaka BUWASA walipofanya juhudi za kulipa sehemu ya deni lililosaidia huduma ya maji kupatikana kwa mjini kati, lkn Tanesco wakagoma kuwarejeshea umeme wa kuendesha mitambo kusukuma maji kwenda matanki ya kata za ukanda wa juu mpaka sasa.

Kwa nini buwasa inashindwa kulipa deni lote? Ni kwa sababu kwanza deni ni kubwa na kulikuwa na makubaliano kati ya BUWASA na serikali kuwa, kwa sababu gharama ya umeme wa kuendeshea mitambo mipya ni kubwa mno kiasi kwamba kama gharama yote itabebwa na BUWASA basi gharama ya bills za maji inaweza kuwa mara mbili ya ilivyo sasa hivyo serikali ikaahidi kuchangia gharama za umeme na BUWASA nusu kwa nusu, lkn pia kuna deni la umeme linalotakiwa kulipwa na mkandarasi wa mradi wa bunena kwa umeme alioutumia wakati wa ujenzi wa mradi ambalo linahesabika kwa BUWASA, mkandarasi yuko tiyari kulipa deni hilo atakapokuwa amekamilishiwa malipo yake ya kazi toka kwa mamlaka husika na akisha lipa deni hilo na serikali kuongeza luzuku zake basi umeme utarejeshwa na mitambo kusukuma maji bila shida yoyote, lkn pia BUWASA na wao wanazidai taasisi za serikali pesa nyingi hivyo na wao pesa nyingi iko nje kwa wadeni.

BUWASA haikukaa kimya kwa sababu inajua maji ni uhai, ilikimbia na kwenda kufufua chanzo cha maji cha kagemu kwa gharama zisizopungua mil 21 na ndicho ambacho kinasaidia kufanya mgao wa maji kwa kata za ukanda wa juu zenye kero ya maji kwa sasa.

HABARI NJEMA

Wafadhili wamekubali kupanua mradi wa usambazaji wa maji ndani ya manispaa ya bukoba, hivyo kata nufaika na mradi huo zitakuwa ni kata za *kahororo na maeneo ya kashai kisindi, buhembe, na nyanga* ambazo hazikuwa zimefikiwa na mtandao wa maji tangu awali, mkataba kati ya BUWASA na mkandarasi unafanyika ndani ya siku chache zijazo.

Hivyo kama mradi utakuwa umekamilika na tatizo la umeme kutatulika, tatizo la maji itakuwa historia ndani ya manispaa nzima ya bukoba.

Kuhusu uwezo wa mradi wa bunena ni kwamba ule mradi una nguvu ya kusukuma maji mpaka nje ya mipaka yote ya manispaa ya bukoba hivyo kinachosubiliwa ni kumalizia deni la umeme na upanuzi wa mtandao wa BUWASA kwa maeneo ambayo hayakuwa yamefikiwa tangu historia.

Binafsi na kama ofisi ya Mbunge jimbo la bukoba mjini tupende kutoa shukrani za dhati kwa mamlaka ya maji bukoba BUWASA kwa juhudi zao za kuboresha huduma za maji ndani ya manispaa yetu ya bukoba.

Tuwaombe wananchi wawe wavumilivu kwa muda wakati ambapo mipango ya kutatua kero ya maji ikiendelea kwa msukumo wa hali ya juu kupitia ofisi ya Mbunge Jimbo la Bukoba mjini.

Asanteni sana kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakionyesha ushirikiano na ofisi ya Mbunge jimbo la Bukoba mjini kwa kutoa taarifa ya kero mbali mbali ndani ya jamii zetu, na sisi tutasimama kidete kuhakikisha tunashirikiana vyema na taasisi husika kwa kuweka msukumo na kuhakikisha huduma bora kwa jamii zinaimarika.

Asanteni sana,

BUKOBA ITAJENGWA KWA UPENDO, USHIRIKIANO NA MSHIKAMANO BAINA YETU.

Imetolewa na Ofisi ya Mbunge jimbo la Bukoba mjini.
 
Kuna mahala hapajaeleweka, kwahiyo muda wa mradi wa Tushirikishane umekwisha kwa miezi tisa kufika kikomo inakuwaje yale yaliyoletwa kwenye mradi huo hatima yake nini? Na maana yake hamhitaji ushauri tena? Mbona ofisi ya mbunge haiongelei tena miradi mikubwa ya stand na soko katika taarifa yake?
 
Kwa niaba ya wasafiri wote mkoani Kagera hasa wale wa masafa ya mkoani na maeneo mengine ya mbali, natoa pongezi kubwa sana kwa wamiliki na madereva wa mabasi makubwa. Hakika mnajitahidi kwa kuvumilia hari ya uchafu wa stand ya Bukoba. Hamjakata tamaa kwa udogo na uchakavu wa stand yenu na hii iko wazi kwa kila mja.

Nimeshangazwa na idadi kubwa ya mabasi makubwa tena ya kisasa kabisa yanayolala stand kwa ajiri ya safari za alfajiri. Sikutarajia wala kudhani, haka ka stand ni ka hovyo na kachafu kweli kweli lakini kenye sifa moja kubwa. Sifa ya kuhudumia magari mengi sana, achia mbali yale yanayoingia na kutoka kuelekea Uganda n.k na zile dala dala ndogo za ruti fupi fupi. Hakika magari ni mengi sana na mnastahili pongezi. Makampuni ya Frester, Bunda, Sabuni, Satco, ArushaXpress, Nbs, Ilyana, Ota Classic, Prince Muro, Falcon, Friends, n.k mnastahili kupigiwa mizinga ya heshima.

Niwapongeze na wasafiri pia kwa kujitahidi kuyatumia mabasi haya, kwa namna yanavyojaa inaonesha kabisa mnakidhi mahitaji na mategemeo ya wamiliki. Hakika wasafiri wanaoingia na kutoka ni wengi kweli kweli, si ajabu ukakuta kila basi liko level seat kwa kila ruti. Hongereni sana. Kitu kimoja cha ajabu na kinyama ni hali mnayoachiwa ili kuendelea kufanyia kazi zenu.

Haingii akilini kituo kinachopokea magari kiasi hiki kikaachwa na kufanana na uwanja wa vita vya msituni. Kituo ambacho abiria akifika anatamani miguu yake isiguse chini kwa kuhofia uchafu na mavumbi yaliyoko pale. Haishangazi kumwona mtu akishuka tu chini na kuanza kupiga chafya nyingi na kutafuta kitambaa cha kujiziba puani ili asiathiriwe na mavumbi, hili ni jambo la hovyo katika usafiri wa Bukoba na ndio hari halisi iliyoko hapa.

Yaani mapato na ushuru wote mnaoupata katika stand hii yenye basi na dala dala za kutosha mmeshindwa kudizaini hata sehemu nyingine ya kuhamishia stand kwa mda wakati mkiendelea na kubishana kwenu juu ya kyakailabwa? Hizi tozo zote kutoka katika stand hii mnazipeleka wapi? Haya mapato yana uharari gani kama hayarudi kuhuudumia eneo husika? Absard!

Kwa pamoja tunawakaribisha wageni lakini mchukue tahadhari mkifika stand, kuweni na viatu visivyotimua vumbi na msisahau kubeba vitambaa kwa ajiri ya kujipangusa na kujifutia mavumbi mkitua mjini Bukoba. Karibuni wageni wetu, sisi ndo nshomile katika dunia hii.
 
Matatizo madogomadogo yanayoweza tatuliwa haraka mjini bukoba
1.mzunguko Wa ndizi mawe yake kuanza kutoa maji.
2. Ujenzi Wa parkings za magari na sehemu za wapita w kwa miguu
3.ushawishi Wa wafanyabiashara kuanzisha mfumo Wa daladala mjini bukoba.
4. Kutengeneza mitaro vizur kwa kuwekea calvats
5.upanuzi Wa barabara za katikati ya mji yaani lami ifike kwenye majengo kama ilivyo rwamishenye ce nter
Ujumbe viongozi wetu fanyeni mambo madogomadogo kwanza na yanayoonekana hapo ndo mtapata fedha za kufanya mikubwa moshi na iringa walifanya hivyo na walifanikiwa fuateni mfano
Nakuunga mkono mkuu, Hivi swala la daradara siioni kama kuna ugumu kwa sababu uongozi hauitaji pesa zaidi ya kukaribisha wawekezaji na kuwapa utaratibu
 
MRADI WA DARAJA LA ENEO LA KYABITEMBE

Nimelazimika kuandika kidogo kuhusu mradi wa daraja la Kyabitembe.
Kyabitembe ni eneo lililo katika mtaa wa Bunkango kata ya Nshambya Manispaa ya Bukoba.
Mimi ndiye diwani wa sasa wa kata hii baada ya uchaguzi wa 2015.
Mwaka 2014 halmashauri ya manispaa ya Bukoba ilipata fedha Sh. 200,000,000.= kupitia serikali kuu ili iweze kujenga daraja katika mto Kanoni ili ku link eneo la Kyabitembe (kata ya Nshambya) na kata ya Rwamishenye. Ilikuwa pia ijengwe barabara ya lami kilometa moja kila upande. Hata hivyo tokana na mgogoro wa madiwani waliokuwepo 2010/2015 pamoja na mbunge wa wakati huo kugomea vikao, Jambo hili lilishindikana na menejimenti ilihamisha pesa za mradi huo na kupeleka kwenye mradi wa kujenga maabara za shule za kata tokana na agizo la Rais la kutaka kila shule iwe na maabara kabla ya mwezi June 2015. Na kwa sababu halmashauri haikuwa na bajeti ya kujenga maabara hizo, walitumia pesa hiyo. Na hilo lilififisha kabisa mpango wa ujenzi wa daraja hili.

Wanaoufahamu Mji wa Bukoba umegawanywa na mto Kanoni na kufanya mawasiliano kati ya baadhi ya kata na kata nyingine kuwa mgumu au kulazimika kuwa na mzunguko mkubwa ili uifikie kata nyingine. Nitatoa mfano wa kata yangu ya Nshambya ili uvuke kwenda kata ya Rwamishenye unalazimika kutumia vivuko vya miti au vyuma vilivyolazwa juu ya mto kuvuka. Vile vile hata kwenda kata ya Hamugembe urahisi ni kutumia vivuko hivi maana ndio short cut vinginevyo utalazimika kuzunguka sana. Na katika eneo langu la uwakilishi kuna vivuko vya miti kama saba hivi. Na vivuko hivi kwa sababu ni vya miti au vyuma vilivyowekwa kwa wananchi kujitolea nguvu zao wenyewe mara nyingine kwanza uharibika kwa kuoza lakini pili sababu nyingine kubwa ni kuzolewa na maji mvua inapokuwa nyingi kupita kiasi. kwa hili la pili usumbufu mkubwa utokea kwa wananchi wa Kyabitembe na mtaa wa Migera ambao ni mtaa ulio jirani na Kyabitembe na ambao pia unaotenganishwa na Rwamishenye kwa mto huu huu.
Kuna rekodi ya vifo vya watoto hasa wanafunzi na watu wazima vilivyotokea tokana na kuvuka wakati mto huu Kanoni unapofurika tokana na mvua kunyesha kupita kiasi. Kwa kutambua adha hii Halmashauri ya manispaa ya Bukoba walilazimika kuja na mradi wa kujenga daraja kubwa la kudumu na kuuita mradi wa Daraja la Kyabitembe na si vinginevyo.

KWA NINI UITWE MRADI WA DARAJA LA KYABITEMBE?

Mradi huu umeitwa jina la Kyabitembe sababu mnufaika mkuu katika mradi huu ni Kyabitembe na sio eneo jingine.
Watu wa Kyabitembe wamekuwa wakipata huduma zao Rwamishenye maana ni karibu sana na wao. Wanafunzi wa Kyabitembe usoma shule za Rwamishenye, Wakina mama na watoto wao wamekuwa wakipata huduma za Afya katika kituo cha afya Rwamishenye na watu wengine wamekuwa wakipata huduma za kununua vyakula na vitu vingine Rwamishenye maana ndio eneo lililo karibu sana nao kuliko eneo jingine.
Watu wa Rwamishenye huja Kyabitembe matembezi tu kwa rafiki zao na hakuna wanafunzi wa Rwamishenye wasomao Nshambya kwa sababu shule ya msingi na sekondari za kata ya Nshambya ziko mbali na eneo hili, wala hakuna wanaokuja matibabu Nshambya kwa sababu hospiatali ya Nshambya bado ni zahanati tu isiyoweza kuwahudumia kama kituo cha afya cha Rwamishenye kinavyoweza kuwahudumia ingawa hospitali hii inategemewa kuwa hospitali ya wilaya (manispaa) katika siku zijazo. Watu wa Rwamishenye kwa ujumla ni wanufaika kwa kupata biashara zao kununuliwa na watu wa Kyabitembe.

MAENDELEO YALIVYO SASA KATIKA UJENZI WA DARAJA LA KUDUMU LA KYABITEMBE
Mimi kama diwani wa kata ya Nshambya, Naibu Meya na mjumbe wa Kamati ya fedha na uongozi baada ya kuona adha ya wananchi ninaowawakirisha katika eneo la Kyabitembe na pia kuona hoja iliyokuwa ikitolewa na CAG kuhusiana na fedha zilizohamishwa kufanya shughuli nyingine badala ya ujenzi wa daraja, nilikuwa nikisukuma hoja katika vikao vya kamati kuhakikisha fedha zilizochukuliwa zinarudishwa na mradi wa kujenga daraja unafufuliwa upya.
Kwanza tulipanga kukopa fedha toka NMB sh. bilioni 1 ili tupate fedha hizo sh milioni mia mbili na zitakazo baki zimalizie maabara maana maabara nyingi hazijamalizika ujenzi wake. Mpango huu ulionekana kwenda vizuri.
Hata hivyo mwaka jana serikali ilichukua baadhi ya vyanzo vya halmashauri ikiwemo property tax (kodi za majengo) na kusababisha cash flow ya halmashauri kutokuwa nzuri na kufanya mpango wa kukopa usiendelee maana halmashauri isingeweza kulipa tena mkopo huo.
Jambo hili lilitusukuma kufanya uamuzi wa kuwa tunatenga fedha kidogo kidogo katika mapato yetu ya ndani (own source) ili tufike mahali ambapo tutakusanya fedha hizo na kuanza ujenzi wa daraja hilo. Hadi mwezi June 2017 tumeshaweka sh.40,000,000 toka katika makusanyo ya ndani na tumekuwa na azma ya kuhakikisha tunaendelea kufanya hivyo kila mwezi ili tufikishe lengo letu.
Pia katika mwaka wa fedha 2017/2018 tumetenga tena sh.200,000,000 katika bajeti zetu ili tuone tunafanikisha mpango huu maana sh. 200,000,000 haziwezi kutosha kukamilisha mradi huu.

MAFURIKO YA TAREHE 08/04/2017

Mji wa Bukoba hususani manispaa ya Bukoba mnamo tarehe 08/04/2017 ulizingirwa na maji baada ya mto Kanoni kufurika na kuleta maafa makubwa ikiwemo kuanguka nyumba na kuharibika kwa mali mbali mbali. Kata ya Nshambya pia ilikuwa mhanga wa mafuriko hayo.
Katika eneo la Kyabitembe vivuko vyote vya waenda kwa miguu vipatavyo vitatu vilizolewa na maji na kusababisha adha kwa wavukaji kwa miguu kutoka Kyabitembe kwenda Rwamishenye. Wanafunzi wanaosoma Rwamishenye kutokea eneo la Kyabitembe, wafanya biashara wanaofanya shughuli zao Rwamishenye tokea Kyabitembe na hata wanaonunua vyakula Rwamishenye tokea Kyabitembe walipata adha kubwa. Ikumbukwe kwamba bila kuvuka mto huu wa Kanoni mtu ulazimika kuzunguka mwendo wa saa nzima wakati kwa kuvuka mto tu inakuchukuwa dakika tano hadi 10 kufika Rwamishenye.

Tokana na adha hii uongozi wa wilaya wa Chama CHADEMA ukiongozwa na mwenyekiti wa wilaya ulitembelea eneo hilo ukiambatana na madiwani, mimi na mstahiki Meya ili kuona adhari hii na kuona tunaweza kufanya lipi ili kuwasaidia wananchi wa Kyabitembe waweze kuvuka kirahisi. Tuliuona uharibifu mkubwa uliotokea na kupanga mikakati namna ya kusaidia.
Katika eneo hilo tulikuta tayari wananchi wenyewe wameshatengeneza kivuko kimoja cha muda cha miti.
Mimi kwa kushirikiana na uongozi wa mtaa wa Bunkango ambako ndiko eneo ya Kyabitembe liliko, tulianza mikakati ya kuona tunapata miti mingine mikubwa na kuongeza vivuko zaidi. Nilimuendea mkurugenzi wa manispaa na kumuomba kibali ili tupate miti zaidi na alitupa miti iliyokuwa eneo la omumwani ambayo ilikatwa na kusombwa na gari ya manispaa niliyoiomba mwenyewe.

Pia moja ya kivuko kilichoharibika kilikuwa kimetengenezwa na vyuma ambavyo maji hayakuvipeleka mbali.
Mimi diwani kama pia member wa kamati ya fedha pamoja na mstahiki Meya tuliishawishi kamati ya fedha ikubali kutembelea eneo hilo na kujionea uharibifu, tena itoe wataalamu wa idara ya ujenzi ili watathimini na kushauri namna bora ya kujenga kingo katika mto ambazo zitasaidia vyuma hivi visizolewe tena na maji na kisha kamati ikubali kutoa fedha za dharura ili tujengee vizuri nguzo imara zitakazoshikilia vyuma hivyo. Nililazimika kutumia ushawishi mkubwa maana hapakuwa na bajeti kwa ajili ya shughuli hii.
Manispaa ilikubali, ikatangaza tenda na kisha shughuli za ujenzi kuanza na kwa sasa bado zinaendelea.
Napenda kusisitiza kwamba nimekuwa nikifanya haya kwa kusaidia watu wa eneo la uwakilishi wangu bila kutafuta sifa (cheap popurality).
Hata hivyo kumekuwa na upotoshaji wa radio moja hapa mjini kuhusu masuala ya Kyabitembe. Ningependa niweke wazi kwamba daraja hilo linaitwa daraja la Kyabitembe maana wanufaika wakuu ni Kyabitembe na si vinginevyo, na kwamba nitaendelea kupigania haki za wana Kyaabitembe nikiwa kama mwakilishi wao na kwamba sisi madiwani katika manispaa tulikubaliana madiwani kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa maana nia yetu ni kuhakikisha kwamba mwananchi ndiye anapata manufaa bila kujali vyama vyetu.

UCHOCHEZI WA RADIO HIYO ISIYOONA JEMA LINALOFANYIKA KATIKA MANISPAA YA BUKOBA NA UKOME.

JIMMY A. KALUGENDO
DIWANI KATA NSHAMBYA NA NAIBU MEYA.
 
Sasa litakamilika lini

Sent from my VF685 using JamiiForums mobile app
 
Nakupongeza walau kwa kuweza kulitambua jukwaa hili na kulitumia. Endelea kuwajibika kwa ajiri ya mnaowaongoza lakini ni vizuri na wenzio wakatambua umuhimu wa mawasiliano kupitia majukwaa kama haya. Inaumiza sana mnapoamua kujiweka kando na mitandao hii juu ya kuongelea maendeleo na nyie mkijiweka kando.

Tukuulize tu, mipango ya stand na soko mliishia wapi wewe kama n. meya na mjumbe kamati ya fedha?
 
Mkuu swala la soko na stendi hawatoagi majibu hawa watu.
 
Tushirikishane mikoa mingine imefanikiwa hasa kigoma,na nzega mtujuze bukoba kilichoshindikana nini mbunge haonekani

Sent from my VF685 using JamiiForums mobile app
 
Tena mwenye app hii ni Wa bkb lakini mradi huu umeshindikana kulikoni

Sent from my VF685 using JamiiForums mobile app
 
Tushirikishane mikoa mingine imefanikiwa hasa kigoma,na nzega mtujuze bukoba kilichoshindikana nini mbunge haonekani

Sent from my VF685 using JamiiForums mobile app
Kama nzega hakika wamefunika ukitembelea uzi wao ni bampa to bampa Nzega wapo vizuri bukoba nendeni nzega mkajifunze
 
Hao jamaa wajifunze wakati wao wana madigirii yao? Wao ni watu wa kushindwa tu majigambo mengi kumbe wamejaa upumbavu tu vichwani mwao. Hakuna walichoweza eti juzi ghafla wanakuja kutwambia muda wa "tushirikishane wa miezi tisa umeisha". Muda umeisha lakini ukiuliza walichofanikiwa kati ya vipaumbele vyao hakipo hata kimoja, ni porojo tu. Waliopewa majukumu wala hawajitambui, vichwa vyao wanafugia nywele tu na kutembeza majungu. Wamewafukarisha wananchi kwa ujinga wao na tamaa zao

Ni mara mia mkakaa bila ya kuwa na viongozi kuliko hawa anywa gongo na walevi wa madaraka
 
Waendesha mradi watoe miezi tisa mingine tuone pengine mda ulikuwa mdogo
 
Ofisi ya mkoa, wilaya, halmashauri na mbunge wao yote ni majipu. Mh.rais anasisitiza watu tulipe kodi lakini kulipa kodi zetu halafu zikaliwa na watu wa aina hii ya viongozi walioko hapa mkoani ni wizi wa aina yake pia. Pesa zetu za kodi zinaliwa bure na haya majipu kitu ambacho kinashangaza kwanini kinatokea katika huu utawala
 
Hivi zilikuwa mbwembwe au yaani sijaona manufaa ya mjadala huu tujuze mmekwama wapi maana bila stendi,soko sijaona kama mmefanya kitu kumbukeni hii
669a2f12048f9950a9e7838e6d358600.jpg
7cfa4266e826c532147480a9850ce9a1.jpg
9536e2adb9af752842a93717b3f7730a.jpg
8f9a1e8377a48ae42124bc4250693c3d.jpg
manufaa yaliyotakana na mjadala ni
2d62a100bc3be4ab525f65ab13d813cb.jpg
c7c1301b5ee71ed930d2764110b35202.jpg
e9c553fe81ea6f2281980acda35fe54f.jpg
5f7f283284cd67cbf75c4e74031be899.jpg
f30a5ec74f952a915e8e1c3aa39eb1db.jpg
ea953bd466b9646bb9a0da5b58b5524a.jpg
8f8450b569a951c4cc86c0616db0c7ef.jpg
badala ya yafuatayo
f1388756d7478d046ceac13ef7c517a4.jpg
2349ba18747dd6f90cf092fb61d439fd.jpg
tafakarini mchukue hatua au mlikuwa mnatuchezea tu shida uko wapi

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Siku nyingine mkianzisha mijadala muwe mnaweka hitimisho,mafanikio na matatizo sio kuishia mitini yaani tulianza bukoba ,kigoma walishafanikiwa na nzega sijui bukoba ililogwa na nani

Post sent using JamiiForums mobile app
 
Miezi tisa iliisha kwa majungu na mbwembwe. Yaani Bkb hata akija malaika hapo hatoboi kwa umbwiga ulioko hapo. Nawaona ndugu zangu wengi badala ya kuweka vikao na kujadiliana haya mambo kama wananchi wao kutwa wako fb wanaweka vipicha vyao na kuishia kusalimiana, matatizo yote hayo na bado mnatanua fb kuongea umbea wakati mji wenu ni kama machinjioni!!?? Ukiona watu wanaendekeza sana starehe na mambo ya mzaa kiasi kile wakati jahazi lao linazama basi ujue uwezo wao wa kufikiri uko chini ya wastani. They are simply abnormal. Akili zetu watu kutoka mkoa huu sahivi zinatia mashaka makubwa sana na uenda kweli tatizo la utapiamlo linalosemwa kila siku limetuathiri sana

Ni kweli viongozi ni mizigo ila wananchi ni magunia ya misumali kwa sahivi
 
Back
Top Bottom